Hata mimi pia nilifuatilia hicho kipindi na nilimsikia huyo Daktari akisema hivyo. Tatizo jingine ni kwamba namna inayotumika kupima ugonjwa huu wa tezi dume sio nzuri kwa mwanaume, sababu ni lazima Daktari akuingizie vidole kwenye njia ya "haja kumbwa" ili aweze kuzigusa tezi hizo na kuhisi ukubwa wa tezi hizo. Hapo ndipo penye shida kubwa sana. Wanaume wachache sana wanakubali hicho kipimo, wengi wao wakifika hospitali na wakiambiwa inatakiwa wapimwe kwa namna hiyo huwa wanakataa na kuondoka.
Hata mimi pia kamwe siwezi kukubali kipimo kama hicho hata kama Daktari ni mwanamke. Ee, MUNGU BABA, pitishia mbali baala hili. Ameni.