Zanzibar 2020 Hii ya Wazanzibari kudai nchi yao imekaaje?

Zanzibar 2020 Hii ya Wazanzibari kudai nchi yao imekaaje?

mcoloo

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
918
Reaction score
1,402
Nimetizama clip moja ya kamanda wa ngome ya vijana wa ACT wazalendo akidai kuwa upigaji kura wa mwaka huu ndio wa mwisho kwa wazanzibari, akimaanisha kuwa hawatakubali tena kuwapigia kura viongozi wanaoandaliwa Dodoma.

Hizi sio dalili njema kwa muungano wetu. Inabidi vikao vya maridhiano vifanyike haraka sana ili kunusuru hatari inayoukabili Muungano.

Serikali ya CCM ifike mahali ikubali kusoma alama za nyakati, hawa watanzania wa leo si wale wa miaka mitano iliyopita. Ni jamii ya watu ambao wanataka wawe huru katika maamuzi yao ili mradi hayalengi katika kuvunja Sheria. Ni jamii ya watu wanaoelewa haki zao kuliko wale walio kuwepo miaka mitano iliyo pita.
 
Nchi yao tuwanyime kwanini tuwape tu,

Tugeukie koloni lingine la Ndaishimiye tumpe ugavana awe anawakilisha wenzie pale chamwino kwenye uapishaji ila wazenji tumewatawala sana tuwaachie na wenyewe waonje uhuru
 
Hivi kwa akili zenu mnafikiri mtaitawala Zanzibar miaka yote? ile ni nchi na wananchi wake wana haki ya kudai UHURU wao, yaani kuamua mambo yako bila kupangiwa na Tanganyika.

Kama ni Muungano hakuna anayekataa ila si wa kuazimishana ama kuingiza kinyemela mambo ambayo kimsingi hayakuwepo wakati wa makubaiiano ya awali ya waasisi., y
 
CCM na selikali yake walipaswa kusoma alama za nyakati na kuzitatua kero za muungano.
Badala yake wakajikita kuwadanganya wa Tanganyika kuwa Muungano wetu upo salama.

Huu uongo Haujengi, unabomoa.
Tatueni kero za Muungano kabla hujavunjika.
 
What comes around goes around.

Ni kwa jinsi ile ile ambavyo muungano huu ulivyokuja ndivyo ambavyo utavyoondoka vilevile. Watanganyika na Wanzabari wanataka utaifa na uhuru wao kamili.

Kama ni suala la aina ya muungano wanataka kufanyike kupitia maridhiano mapya na ya wazi yatakayo wahusisha wananchi wa pande zote mbili. Janja janja na ghiliba za CCM tupia kule.
 
Nchi ya Zanzibar ilishakufa sasa tunaongea lugha moja ya neno Tanzania
Hatupo tayari kurudi huko maana tulishapita........
CCM imejikita sasa katika kuendeleza nchi ya Jamhur ya Muungano wa Tanzania
 
Sirro alisema ataweka kambi Pemba sijajua anataka kufanya nini na kwa nini

Anamjuwa mdudu anaitwa popobawa?


Nakumbuka miaka ya early-mid 90's story za popo bawa zilikuwa at its peak. Kuna Mzimbabwe akatuuliza hiki popobawa ni kitu gani kwani? Rafiki yangu akamjibu, "its a magic f*cker!"
 
Nchi moja maraisi wawili ni udhaifu wa muunganiko.
 
Mleta maada andika baadhi ya wazanzibari na ukitaka kuwa specific andika baadhi ya wapemba waarabu kikao akina Maalim Seif and Co sio wapemba sababu hata Shein na Profesa Mbarawa ni wapemba lakini si sehemu ya huo ujinga
 
Hilo ni takwa la Wazanzibari wachache sana.. Wangekuwa wengi wenye takwa hilo, tungewapa ruksa kama Membe wajipime nje ya CCM (muungano) maisha yakoje!
 
Ukweli ni kwamba huu Muungano unalindwa na vyombo vya usalama tu. Ridhaa ya wananchi hakuna..... kama wanajiamini waweke kura ya maoni
 
hawataki utawala wa jiwe wanataka kuchagua viongozi wao tukae mezani tuujadili muungano
 
Back
Top Bottom