Hii Yanga ya Zahera imeanza kunipa wasiwasi

Ulimakafu

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Posts
31,248
Reaction score
13,244
Toka mechi za majaribio mpaka hizi za kimashindano timu yangu ya Yanga SC chini ya Mwinyi Zahera imeanza kunitia shaka sana, tena sana tu. Zahera naona alianza kupotea maboya toka msimu ulopita kwa jjinsi alivyoshughulikia suala la Yondani na Kakolanya na pia kumpa unahodha Ajibu.
Kwa hii timu ya sasa nayaona haya:
1. Timu haina mpangilio/muunganiko toka nyuma hadi mbele
2. Hatuna m(wa)shambuliaji wa kutegemewa-mtu wa kumaliza mechi
3. Timu ya kwanza imejaa wageni wa nje wasio na uwezo mkubwa
4. Kocha mbishi sana na hataki kubadilika
5. Si busara kumpa unahodha mgeni na wenyeji wazoefu wapo
6. Kocha anakosa mbinu za kufanya wakati mechi inaendelea hasa tukiwa tumefungwa
7. Kuna wachezaji hawakustahili kuachwa au kuuzwa; Kamusoko, Tambwe, Makambo hata Ajibu
8. Kocha kapunguziwa majukumu sasa afanye kazi yake
9. Timu haina wachezaji wenye 'fighting spirit', wapo wapo tu
10. Timu haina kiongozi ndani ya dimba-nahodha anapwaya
11. Kocha ni bingwa wa visingizio wakati tatizo ni lake
12. Zahera kwa sasa kashika kitasa kilichoandikwa Exit Door ( In Edo Kumwembe's voice).

Kwa sasa yangu ni hayo tu.
 
Mwinyi Zahera ni fungu la kukosa. Ningekua mimi ndiyo Mshindo Msolla, ningefanya kila liwezekanalo kumfyekelea mbali. Point nyingi ulizoziandika, zina ukweli kwa 100%. Haiwezekani mpaka ligi inaanza, bado kocha anafanya majaribio ya kikosi.
 
Subirini kipaumbele ni kuchukua ubingwa wa afrika so hayo ya Ruvu Shooting siyo kipaumbele
 
Mwinyi Zahera ni fungu la kukosa. Ningekua mimi ndiyo Mshindo Msolla, ningefanya kila liwezekanalo kumfyekelea mbali. Point nyingi ulizoziandika, zina ukweli kwa 100%. Haiwezekani mpaka ligi inaanza, bado kocha anafanya majaribio ya kikosi.
Kweli kabisa mkuu, yaani huyu bwana anatupa presha na matusi toka upande wa pili.
 
Umesema timu imejaa wageni, sasa kwa nini kulalama? Kuhusu fighting spiritacha uongo. Tumeona walivyopambana Botswana. Tusiipime timu kwa mechi za awalimaadam ni wachezaji wapya. Mpira sio muujiza mkuu, kila jmbo linatokea kwa utaratibu.
 
Umesema timu imejaa wageni, sasa kwa nini kulalama? Kuhusu fighting spiritacha uongo. Tumeona walivyopambana Botswana. Tusiipime timu kwa mechi za awalimaadam ni wachezaji wapya. Mpira sio muujiza mkuu, kila jmbo linatokea kwa utaratibu.
Sawa mkuu, wageni waliopo ni wa kawaida sana.tunataka wawe ni viwango vya juu ya wazawa.
 
Kipindi cha Cannavaro huu ujinga wa kupoteza poteza kwa Ruvu Shooting haukuwepo.
 
Ukweli timu ya wananchi imetushinda tutafute mtu tumpe hisa tupate mautam hao Akina moringa ni aina ya wachezaji Ambao wanatokana na bakuli tunalochangia ila ukweli mpira pesa
 

Nakubaliana na wewe kwenye 1, 2, 3, 7 na 9.....Jana nimeangalia asilimia 90 ya Mechi...Makambo na Tambwe hawakupaswa kuuzwa/kuachwa...timu haina continuity kutoka msimu uliopita...Yaani kuna timu 'mpya' yenye wachezaji waliokusanywa kutoka maeneo mbalimbali..it is a shame... kwa kikosi cha jana kilichoanza kilikuwa na wachezaji watatu tu wa msimu uliopita...Yondani, Tshishimbi na Feisal...huwezi kushinda katika hali hii....Mimi siyo kocha lakini nafahamu timu ikiwa na wachezaji karibu wote wageni ni ngumu kushinda...Kwa hakika kulikuwa na kosa la kiufundi...Yanga kwa kikosi cha jana ilipaswa iwe na wachezaji angalau sita wa msimu uliopita... Halafu wachezaji wa Yanga niliwaona kuwa hawana determination...hawana dhamira ya ushindi...baadhi yao hawakimbilii mipira bali wanataka mipira ifike au itue miguuni mwao....kingine yule beki namba mbili (Mustafa) alikuwa anachelewesha mashambulizi kwa tabia yake ya kurudisha mipira nyuma...
 
Halafu hawa wageni walikuja na kichwa kimewavimba wakijua mpira wa Bongo mteremko.
 
Yanga 1-1 Kariobangi Sharks
Yanga 1-1 Township R
Township 0-1 Yanga
Yanga 0-1 Ruvu Shooting.
Kwa jinsi matokeo yalivyo kwenye mechi hizo 4 Ambazo 3 ndio game za mashindano unapata majibu kuwa safu ya ushambuliaji haiko sawa.
Haiko sawa kwa maana wote kule mbele ni wageni hawana muunganiko mzuri tofauti na eneo la ulinzi ambalo lina wageni + wenyeji ndio maana timu hairuhusu magoli hovyo.
CHA MSINGI NI..?
Je viungo wachezeshaji na winga wanapika nafasi za magoli lakini washambuliaji wanapoteza?
Au washambuliaji wanafata mipira nyuma sana baada ya viungo kushindwa kazi yao na kufanya mbele kukosa nguvu??
Jibu litabaki hakuna muunganiko mzuri wa kushambulia kuanzia katikati kwenda mbele... Kiungo namba 8 NA WINGA ZOTE ya juu na chini wanatakiwa kupika nafasi za maana sio blaa blaa ilimradi tu mpira umeenda mbele bila uelekeo sahii na lawama zinabaki kwa washambuliaji.. Sasa hii ni kazi ya kocha kuweka watu sahihi au kurekebisha.
Kwa mechi hiz chache walizocheza Yanga namuona BALAMA ana nafasi kubwa.
 
Anafungwa na Ruvu anaenda kuisema simba, hapo kwa Makambo, nakazia kwa herufi kubwa
 
Yaani ni aibu kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…