Ulimakafu
JF-Expert Member
- Mar 18, 2011
- 31,248
- 13,244
Toka mechi za majaribio mpaka hizi za kimashindano timu yangu ya Yanga SC chini ya Mwinyi Zahera imeanza kunitia shaka sana, tena sana tu. Zahera naona alianza kupotea maboya toka msimu ulopita kwa jjinsi alivyoshughulikia suala la Yondani na Kakolanya na pia kumpa unahodha Ajibu.
Kwa hii timu ya sasa nayaona haya:
1. Timu haina mpangilio/muunganiko toka nyuma hadi mbele
2. Hatuna m(wa)shambuliaji wa kutegemewa-mtu wa kumaliza mechi
3. Timu ya kwanza imejaa wageni wa nje wasio na uwezo mkubwa
4. Kocha mbishi sana na hataki kubadilika
5. Si busara kumpa unahodha mgeni na wenyeji wazoefu wapo
6. Kocha anakosa mbinu za kufanya wakati mechi inaendelea hasa tukiwa tumefungwa
7. Kuna wachezaji hawakustahili kuachwa au kuuzwa; Kamusoko, Tambwe, Makambo hata Ajibu
8. Kocha kapunguziwa majukumu sasa afanye kazi yake
9. Timu haina wachezaji wenye 'fighting spirit', wapo wapo tu
10. Timu haina kiongozi ndani ya dimba-nahodha anapwaya
11. Kocha ni bingwa wa visingizio wakati tatizo ni lake
12. Zahera kwa sasa kashika kitasa kilichoandikwa Exit Door ( In Edo Kumwembe's voice).
Kwa sasa yangu ni hayo tu.