Hii 'zoa zoa' na 'nyakua nyakua' ya Wasafi FM kwa watangazaji mahiri wa redio nyingine inamaanisha nini?

Hii 'zoa zoa' na 'nyakua nyakua' ya Wasafi FM kwa watangazaji mahiri wa redio nyingine inamaanisha nini?

Nimeona akina Zembwela na Kitenge wameanza kuzinanga ofisi walikotokea, eti wanasema mkia hauwezi kutikisa ng'ombe ila ng,ombe ndiye anatikisa mkia.
Hawa jamaa ilibidi wajiepushe sana na maneno ya taarabu kuzisema kwa mafumbo media walikotokea kwa sababu hawajui kesho yao itakuwaje.
Tena kama kitenge inabidi amshukuru sana dj Majizzo aliyemtoa radio one kwa sababu yeye ndoto yake ilikuwa ni kuzeekea radio one, media nyingine nazo zilikuwa zinadhani kumtoa radio one labda haiwezekani.
Nasikia hata siku majizo anatoa wazo la kumtoa radio one, wenzake walidhani kama anaota hivi.
Kwa kinachoendelea, hata radio uhuru wakivunja kibubu wanaweza kumng'oa yeyote yule na sisi wasikilizaji tutahahama tu.

Wakati ukimtuhumu Kitenge kwa ' Kukunanga ' kule alikotoka na Wewe unaonyesha siyo mfuatiliaji wa mambo hasa haya ya Kihabari kwani ni jana tu Saa 1 Kamili za Usiku Mtangazaji wa Michezo wa Efm aitwae Maziku wakati akiingia tu kuanza Kipindi alipiga Kijembe ambacho hata uwe ni Mjinga ( Ngumbaru ) au Mpumbavu ( Popoma ) vipi utajua tu kuwa alikuwa anakielekeza kwa Watangazaji wa Michezo wa Wasafi fm ambapo alitutaka Sisi Wasikilizaji wao tusihamishe Idhaa ya Efm na kwenda kuwasikiliza ' Matapeli ' na hii ya ' Matapeli ' aliirudia mara mbili.

Na taratibu naanza Kuona Vita kubwa inakuja na ambayo inaenda Kuzaa Uadui mkubwa kwa Watangazaji wa Michezo wa hizi Redio Mbili za Wasafi fm na Efm. Na kibaya zaidi kuna ambao pia walikuwa na Mahusiano ya Kimapenzi na wengine huku Mtangazaji Mmoja kwa Kike wa Redio fulani hapo ( naihifadhi ) akiwa na Chuki na Mwenzie kwakuwa amemuibia Mpenzi wake na Wawili hao walishaanza Kununiana hadi ikambidi Mmoja wao afanye Maamuzi magumu kama haya tunayoyaona sasa.
 
Tatizo la Tanzania ni ubunifu 0. Huyu kahamia huku kapeleka vipindi vyote vya EFM. EFM walikosea sana kutosajili miliki ya vipindi.

Wasafi iko party owned na owners wa CMG hivyo tusitegemee kuona wafanyakazi wa CMG wakinyakuliwa na Wasafi Media
Tatizo la Tanzania ni ubunifu 0. Huyu kahamia huku kapeleka vipindi vyote vya EFM. EFM walikosea sana kutosajili miliki ya vipindi.

Wasafi iko party owned na owners wa CMG hivyo tusitegemee kuona wafanyakazi wa CMG wakinyakuliwa na Wasafi Media
ni kweli Mkuu,mfano segment za kipindi kakopi neno la kwanza namba moja na neno la kwanza namba mbili,pia jogging
 
Hoja yako hii ni ' dhaifu ' na ' mfu ' kwelikweli Mkuu. Ukisema Diamond ambaye amekulia ' Uswazinyo / Uswahili ' na kwamba hana pia Elimu Kubwa mbona hushangai ' Tajiiri Mwandamizi ' nchini Said Salim Bakhressa ambaye anajulikana hana Elimu lakini ameajiri Wasomi watupu tena hadi Wazungu wa kutoka huko huko Ulaya na Marekani ambako kila Siku Mimi na Wewe ' tunakuota ' Kwenda na hadi hata kutaka ' Kuzamia ' katika Meli?

Na nani aliyekuambia kuwa Kusoma sana / Kuelimika mno ndiyo kuwa na Maisha mazuri na Kufanikiwa Kimaisha? Uwasilishaji wako umekaa Kichukichuki hivi hasa kwa Watu ambao labda wamejikuta ama wamezaliwa hayo maeneo yako tajwa ya Masaki na Oysterbay au wanaishi huko sasa na wala huhitaji Akili kubwa kuweza Kuling'amua / Kulijua hili.

Sasa kama umeanza kwa Kusema kuwa Diamond ametokea huko ' Uswazinyo ' pande za Tandale mbona hujiulizi kuwa hakuendelea Kukaa huko na badala yake amejenga maeno mengine ya Watu wenye ' Status ' zao nchini na hadi huko Masaki / Oysterbay pia ameshanunua ' Mijengo ' na anapangisha Watu?

Msomi Kuajiriwa na asiyesoma siyo tatizo na wala asiyesoma Kuajiriwa na Msomi siyo tatizo lakini ukweli utabaki pale pale kuwa hata kama huyu Tajiri asiye Msomi awe vipi lakini bado Kiuwelewa na Kimkakati hatoweza Kumfikia huyu Msomi Mwajirwa na Masikini. Mwisho kabisa tambua ya kwamba mgawa wa kila Ridhiki ni Mwenyezi Mungu pekee hivyo usije ukatokwa bure na Mishipa ya Shingo huku Mimacho ikikutoka kama Mijusi ya ' Balangulu ' kwasababu tu una Chuki zako na Waishio Masaki na Oysterbay. Kokote tu nchini Mtu ukiishi na kama ukijapanga vizuri unaweza kuyafurahia Maisha.

Umetafsiri tofauti sana na kile nilichoandika..
 
Biashara zao wanafanya na wale Abiria ambao huwa wanakuja mara kwa mara na Ndege yenye Jina ambalo pia kwa sasa linatumika na Klabu moja ' maarufu ' nchini Uingereza ( ambao zamani walikuwa na Mchezaji wao tegemeo aitwae Chogo Chemba ) na kila hii Ndege ikitua tu Mkoa wa Wazaramo au ule wa Wachagga utaona Watu wapo ' busy ' mno huku muda mwingine CCTV Camera zikizimwa, sehemu za Mizigo Mitambo huzimwa, wengine hata wasio na ' Diplomatic Status ' utawaona wanapitia VIP Lounges huku wenye Mamlaka ya ' Uangalizi ' wa hivyo Viwanja muhimu kwa ' Mizigo ' inayopeperushwa kiurahisi na Upepo wakiwa wanajifanya kama vile hawaoni Kitu. Hao Abiria wakishuka tu katika hiyo Ndege kimbia katika Hoteli moja ' maarufu ' Masaki ( ambayo Wanamuziki wengi wa Kikongo akina JB Mpiana, Koffi Olomide na Ngiama Makanda Werrason hufikia ) mkabala na ' Slipway ' utawakuta kisha Wenyeji wao ( ambao wengi wao ndiyo hawa unaowaulizia wakishirikiana na wenye Mamlaka baadhi ) hufika hapo kisha ' wanamalizana ' na ndani ya muda utaona ' Utajiri ' wao ukizidi Kuongezeka. Kwa leo naomba niishie hapa tafadhali.

Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer..

Nimeandika hapo juu kama mwenyewe unavyojiita, Majibu yako yamedhihirisha kabisa wewe ni "Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer.." Wengi hawawezi elewa hili, hata hii inaitwa Bongo Movie na Bongo fleva ina dark side nyingi sana kuanzia Kudanga, Ukuwadi, Ushoga na hili lingine naomba namimi niishie hapa..
 
Radio one waliwatenda vivyo hivyo RTD, EFM wakawatenda Radio one, EFM wakawatenda Mawinguni, BBC wakawatenda Radio one (japo wanasema walikua na mkataba retesi) mawingu na RTD.

Ukiwa kwenye duara linalozunguka jua ipo siku aliposimama mwenzio nawe utasimama papi hapo.
 
Hapo wamerisk naaamini wanalipwa pesa nyingi na maboss wanategemea return toka kwao....inamaana wasipoingiza ndo yale yale utasikia amerudi nyumbani...!sitegemei kipya kutoka kwa hawa jamaa coz michezo na ile ile hata ukiangalia ufanisi wao sijaona ubunifu wa kipindi zaidi wametohoa kutoka walipotoka.
Point yangu lazima uwajengee uzalendo wafanyakazi wako...siwasifii clouds but wameibrand cmg kiasi kwamba ni ndoto ya watangazaji wengi kufika pale...
 
Walianza na watangazaji ‘ mahiri ‘ sana wa michezo wakina Maulid Kitenge, Edward Kumwembe, Ahmed Abdallah, Yusuph Mkule, Mwanaidi Suleiman wakimjumuisha na yule mtangazaji waliyemkuta hapa wa michezo Ricardo Momo na jana tena wamemuongeza ‘ Mchambuzi ‘ wa michezo ambaye ndiyo alikuwa akiifanya Magic fm kuwa juu George Ambangile.

Na juzi tena katika kuonyesha kuwa hawana ‘ Masihara ‘ na kwamba wameingia katika ‘ Game ‘ hasa wamemnyakua mtangazaji ‘ mtundu mtundu ‘ Hillary Daud a.k.a Zembwela ambaye atakuwa katika kipindi cha asubuhi na nasikia tena kuwa wiki hii hii kuna watangazaji wengine ‘ mahiri ‘ wa kike na wa kiume wa vipindi vya burudani nao wanaenda kuwachukua.

Habari za chini chini ambazo ' nimepenyezewa ' ingawa bado sijazithibitisha zinasema kwamba baada ya Kumalizana na hao Watangazaji ' mahiri ' wa Michezo sasa wanahamia katika Watangazaji ' mahiri ' wa Vipindi vingine hasa vya burudani, vya kijamii na vile vya ' Kimahaba ' vya Usiku ambapo Redio ambazo kuanzia sasa zikae sawa kwani Watangazaji wake watake wasitake wanaenda ' Kuzolewa ' kama siyo ' Kunyakuliwa ' na Jeuri ya Wasafi Media Company ni hizi zifuatazo:

Ile iliyopo njia panda ya kwenda Coca Cola inatazamana na Taasisi ambayo Wafanyakazi wake wakisikia tu ' Majanga ' yoyote yametokea wao ndiyo huwa wa Kwanza kutokea eneo la tukio.

Ile iliyopo jirani na Mto Mmoja ambao huwa ukijaa hata Ofisi zao Maji hujaa na barabara ya kutoka Ubungo hadi Buguruni Sheli huwa haipitiki kabisa na Malori mengi hupita hapo hapo hadi Treni ya Mwakyembe pia.

Ile iliyopo jirani na Chuo Kimoja Wilayani Kinondoni ambacho Wanafunzi wake hasa wa Kike wakianza Masomo huwa na Nidhamu na Maadili ila baada ya miezi Sita ( 6 ) huanza kuwa ' Makahaba ' na kujiuza eneo la Mita chache na Geti Kuu la Chuo chao hicho

Ile iliyopo njia panda na barabara ya kwenda yalipo Makazi ya Mkuu wa Majeshi wa sasa CDF General Afande Mabeyo na hakuna DalaDala la Kawe ambalo huwa halipiti jirani nao na inatazamana na Eneo maarufu la Burudani na Starehe yenye Jina linalofanana na tarakimu moja iliyopo katika Sinema ya Mcheza Sinema Mkongwe James Bond.

Ile iliyopo eneo la Viwanda Mikocheni ambayo mwaka huu huu karibia 99.9% ya Wafanyakazi wake walitokwa na Machozi japo katika Familia yake sasa hivi ' Moto ' unawaka huko.

Ile iliyopo mkabala na Jengo Moja ( Hoteli ) eneo la Bamaga yenye jina la herufi ' K ' na ipo kwa nyuma yake tu hapo

Shikamooni Wasafi fm na Wasafi tv!

wanapora:
EFM
TIMES
CLOUDS
AZAM
EA RADIO

ndio sehemu zilizolengwa hizo kwa sasa, Pia mimi nachukuliwa kwenye kipindi cha Jioni before Sport court ndio tuko kwenye maongezi
 
Naliona hilo ila wasiwasi wangu tu ni kwamba vipi Siku moja Mtu anayewapa hii ' Jeuri ' yote CEO wao Msanii Nasib Abdul ' Diamond Platinumz ' ikitokea ' akafilisika ' itakuwaje? Tukumbuke kuwa hakuna Binadamu ambaye ameshahakikishiwa na Mwenyezi Mungu kuwa atakuwa ' Tajiri ' Milele na kwa hapa Tanzania tuna mifano mingi tu ya Watu ambao miaka ya nyuma ndiyo walikuwa na ' Jeuri ' na ' Nyodo ' hasa Kipesa ( Kiutajiri ) lakini leo hii wamekuwa ' Masikini ' hadi ukiwaona Mitaani wanatia Huruma na unaweza hata kutokwa na Machozi. Mmoja wapo kuna Kituo cha DalaDala eneo la Sinza kimeitwa kwa Jina lake.
Uwoga wa kimaskini huo uchukuee laki sita wakati kuna 1.5 kwa kazi ile ilee wachaaa kbs au unazanii walee wote hawanaaa akiliii mkuu
 
Wazoefu na Wataalamu wa haya mambo tusaidiane kidogo katika maswali haya..

Hizi redio na TV stations zinapataje faida kiasi cha kuweza kuendesha biashara na kuendeleza uwekezaji?.
Hata mimi nijue hilo
 
Chakufurahisha ni kwamba boss wa mawingu na yy yupo kwenye hicho kinachoendelea Hakuna jipya mbwembwe tu
 
Back
Top Bottom