GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
- Thread starter
- #41
Nimeona akina Zembwela na Kitenge wameanza kuzinanga ofisi walikotokea, eti wanasema mkia hauwezi kutikisa ng'ombe ila ng,ombe ndiye anatikisa mkia.
Hawa jamaa ilibidi wajiepushe sana na maneno ya taarabu kuzisema kwa mafumbo media walikotokea kwa sababu hawajui kesho yao itakuwaje.
Tena kama kitenge inabidi amshukuru sana dj Majizzo aliyemtoa radio one kwa sababu yeye ndoto yake ilikuwa ni kuzeekea radio one, media nyingine nazo zilikuwa zinadhani kumtoa radio one labda haiwezekani.
Nasikia hata siku majizo anatoa wazo la kumtoa radio one, wenzake walidhani kama anaota hivi.
Kwa kinachoendelea, hata radio uhuru wakivunja kibubu wanaweza kumng'oa yeyote yule na sisi wasikilizaji tutahahama tu.
Wakati ukimtuhumu Kitenge kwa ' Kukunanga ' kule alikotoka na Wewe unaonyesha siyo mfuatiliaji wa mambo hasa haya ya Kihabari kwani ni jana tu Saa 1 Kamili za Usiku Mtangazaji wa Michezo wa Efm aitwae Maziku wakati akiingia tu kuanza Kipindi alipiga Kijembe ambacho hata uwe ni Mjinga ( Ngumbaru ) au Mpumbavu ( Popoma ) vipi utajua tu kuwa alikuwa anakielekeza kwa Watangazaji wa Michezo wa Wasafi fm ambapo alitutaka Sisi Wasikilizaji wao tusihamishe Idhaa ya Efm na kwenda kuwasikiliza ' Matapeli ' na hii ya ' Matapeli ' aliirudia mara mbili.
Na taratibu naanza Kuona Vita kubwa inakuja na ambayo inaenda Kuzaa Uadui mkubwa kwa Watangazaji wa Michezo wa hizi Redio Mbili za Wasafi fm na Efm. Na kibaya zaidi kuna ambao pia walikuwa na Mahusiano ya Kimapenzi na wengine huku Mtangazaji Mmoja kwa Kike wa Redio fulani hapo ( naihifadhi ) akiwa na Chuki na Mwenzie kwakuwa amemuibia Mpenzi wake na Wawili hao walishaanza Kununiana hadi ikambidi Mmoja wao afanye Maamuzi magumu kama haya tunayoyaona sasa.