MWANAHARAMU
JF-Expert Member
- Dec 12, 2021
- 5,350
- 13,622
Kila nchi ina mamlaka ya kuamua itakacho,lakini pia maulamaa wa kila nchi hutoa maelekezo ya vazi la staha ni lipi,maana dini ya kiislamu haijataja vazi bali imetaja vazi la staha,sasa mabingwa wa dini kwa kila nchi wanaweza kuelezea vazi la staha ni lipi na ni lazima watatofautiana tu.Tajikistan, Azerbaijan na Kosovo ambazo ni nchi zenye waislamu wengi zimepiga marufuku uvaaji hijab!
Makubazi ni aina viatu hupendwa kuvaliwa na watu wa mashariki ya kati ambao ni waarabu,waajemi na wayahudi na haijalishi wana imani gani ya diniVipi MAKUBAZI???
Hili vazi la hijab ambalo huvaliwa zaidi na wanawake wengi wa dini ya Kiislamu na Waarabu ni vazi la kidini(uislamu) au la utamaduni wa Waarabu?
View attachment 3333245
Mimi nilikua najaribu tu kujibu swali ulilouliza kuhusu hijabu,na nimejibu kwa uelewa wangu! Kwamba je ni vazi la kidini au kitamaduni?Mbona Tajikistan nchi ya Kiislamu wamepiga marufuku uvaaji hijab katika umma?
Hijab ni vazi la kidini au la kiarabu?Hijabu ni nn? kujistiri sio lazima iwe hijabu ,hata ukichukua kanga zile kama huku Tanga basi ni kujistiri...Hijab hizo ni kama mavazi hayana kosa kwa vile hayavunji mila za kujistiri... Wengine hatujawahi kuwaona dada zetu wakivaa hizo zaidi ya kanga ya kupitisha kichwani.
Uislamu ni applicable anywhere hata wale wamasai wanaweza kuvaa zile shuka kichwani ikawa ni stara ya kufunika kichwa Hijab ,Abaya ni version hazina katazo wala hazina maudhi ...Wewe tu uelewa wako juu ya jambo hilo.Tajikistan, Azerbaijan na Kosovo ambazo ni nchi zenye waislamu wengi zimepiga marufuku uvaaji hijab!
1 Wakorintho 11:5-6 (Agano Jipya)
“Lakini kila mwanamke aombaye au atabiriye bila kifuniko kichwani, hufedhehesha kichwa chake; maana ni sawa na yeye aliyenyolewa. Kwa maana mwanamke asipofunika kichwa, na akatwe nywele pia; lakini ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele au kunyolewa, na afunike kichwa.”
Ndio,kufuata utamaduni wa mtu mwingine,ambao hauna athari hasi kwako si vibaya,ni jambo zuri sana,,Kwani unaweza kuutenganisha uislam na uarabu?
Hilo ni vazi la kitamaduni la kiarabu kama ilivyo kanzu. Kwahiyo hawa akina Mwamedi na Mwajuma wa huku Buza wamepewa dini na utamaduni wa mwarabu waufuate.
Vazi la kusitiri mwili ni la aina gani? Vigezo vya vazi la kusitiri mwili vinawekwa na nani? Ni vya aina moja kwa binadamu wote duniani?Ndio,kufuata utamaduni wa mtu mwingine,ambao hauna athari hasi kwako si vibaya,ni jambo zuri sana,,
Hivi naomba niwaulize kuna mtu asiyependa kuvaa vazi linalomstiri mwili wake!!??awe mwanaume au mwanamke,!!,, Kwa hata kufuata haifai uende tu kama hayawani usiyejitambua,bali wafuata kwa kuwa ni jambo zuri kwako.
Nyie wakristo ni watu wa ajabu sana. Kwa hivyo hapo umefurahi kusikia wamepiga marufuku uvaaji wa hijabu. Hao viongozi waliopiga marufuku sio waislamu na kama wakijiita waislamu basi ni wanafiki kwani muislamu wa kweli hawezi kupiga marufuku amri ya Mwenyezi Mungu. Hijabu ni amri ya Mwenyezi Mungu kwa wanawake waumini na sio kwa waarabuTajikistan, Azerbaijan na Kosovo ambazo ni nchi zenye waislamu wengi zimepiga marufuku uvaaji hijab!
La mhimu ni kustiri mwili,sasa vigezo vyaweza tofautiana kati ya nchi na nchi,,lkn mwislamu ni mhimu na lazma kwa mwanamke kujistiri pia kichwani, angalau kwa kanga.Vazi la kusitiri mwili ni la aina gani? Vigezo vya vazi la kusitiri mwili vinawekwa na nani? Ni vya aina moja kwa binadamu wote duniani?
View attachment 3333293
Huyu amesitiri mwil
Kila mtu abaki na dini yake na hakuna haja ya kuingilia dini za watu wengineWakristo wengi huwa wanawapenda waislamu ambao hawavai hijabu, ambao hawasali swala tano, ambao wanakunywa pombe n.k. ila ukiwa muislamu unayevaa hijabu, unaswali na unatii maamrisho ya dini yako basi Wakristo wengi hawakupendi.
Hii inasababishwa na kwamba ndani ya nafsi zenu mnaona husuda kwa kuwaona waislamu wanafuata dini yao kikamilifu hali ya kuwa nyinyi mna dini yenu lakini hamuifuati.
Kila mtu abaki na dini yake