Hijab ni vazi la kidini au utamaduni wa kiarabu?

Hijab ni vazi la kidini au utamaduni wa kiarabu?

Wanasema kanzu sio vazi la kidini linaweza kuvaliwa na yoyote, huwa naona wanaume wengi Wagalatia wanavaa kanzu ila sio rahisi kuona wanawake Wagalatia hasa watu wazima sana wamevaa hijab.
Kanzu ni moja la vazi la kabila la wahaya,tena mara nyingi huongezea na koti na hata kwa waganda.
 
😡😳hii kata vichwa ni kwa mujibu wa maandiko yao matakatifu???
 
Kila nchi ina mamlaka ya kuamua itakacho,lakini pia maulamaa wa kila nchi hutoa maelekezo ya vazi la staha ni lipi,maana dini ya kiislamu haijataja vazi bali imetaja vazi la staha,sasa mabingwa wa dini kwa kila nchi wanaweza kuelezea vazi la staha ni lipi na ni lazima watatofautiana tu.
Ni kweli kabisa. Quran imesisitiza vstara kwa wanawake na wanaume . Na wanawake wameambiwa wafunike vifuo vyao . Hayo mengine ni makubaliano ya maulamaa kutokana na mila zao huko. Sisi ni ku copy na kupaste kila kitu
 
Hili vazi la hijab ambalo huvaliwa zaidi na wanawake wengi wa dini ya Kiislamu na Waarabu ni vazi la kidini(uislamu) au la utamaduni wa Waarabu?
View attachment 3333245
Dini nyingi zimebeba mambo ya utamaduni wa watu wakafanya ni sehemu ya imani. Kwa Kakobe pale wanawake walikua wanavaa viremba kufunika vichwa sijui kama wanaendelea.
 
hapana,sio kweli waarabu kwanza hawakuwa na dini,aliyewaingiza uislamu ni mtume muhammad,hivyo uislabu na uarabu ni vitu tofauti
Acha uongo:
Kabla ya kuja kwa Uislamu katika karne ya 7 Miladi, Waarabu walikuwa na dini mbalimbali. Hapa chini ni muhtasari wa dini kuu zilizokuwa miongoni mwa Waarabu kabla ya Uislamu:

1. Upagani wa Kiarabu (Usanamu)​

  • Waarabu wengi walikuwa wapagani na waliabudu masanamu na miungu mingi.
  • Walimwamini Mungu mkuu (aliyeitwa Allah, maana yake "Mungu"), lakini pia waliabudu miungu midogo.
  • Miungu maarufu ilikuwa:
    • Hubal – mungu mkuu wa Kaaba huko Makka.
    • Al-Lāt, Al-‘Uzzā, na Manāt – miungu wa kike waliotajwa kwenye Qur'an (Surah An-Najm 53:19-20).
  • Masanamu yao yalihifadhiwa kwenye Kaaba.

2. Ukristo​

  • Baadhi ya makabila ya Kiarabu, hasa ya kaskazini kama Waghassani, walikuwa Wakristo.
  • Walifuata madhehebu ya Kikristo yaliyokinzana na Kanisa rasmi la Roma, kama vile Monofisite na Nestoria.
  • Ukristo uliathiri zaidi maeneo yaliyo karibu na Milki ya Kirumi ya Mashariki (Byzantine) na Ethiopia.

3. Uyahudi​

  • Makabila kadhaa ya Kiarabu, hasa katika maeneo ya Yathrib (Medina), Khaybar, na Yemen, walikuwa Wayahudi.
  • Makabila ya Kiyahudi yalikuwa kama Banu Qurayza, Banu Nadir, na Banu Qaynuqa.

4. Uzoroastra​

  • Ulifuatawa na Waarabu wachache, hasa wale waliokuwa chini ya athari ya Milki ya Wasasani ya Uajemi, hasa mashariki mwa Uarabuni kama Bahrain.
  • Uzoroastra ulikuwa dini rasmi ya Dola ya Uajemi.

5. Uhanif (Umoja wa Mungu kama wa Ibrahimu)​

  • Kulikuwepo na kundi dogo la watu waliokuwa waumini wa Mungu mmoja (wanaitwa Hanif).
  • Hawakuwa Wayahudi wala Wakristo, lakini waliamini katika Mungu mmoja, na walidai kufuata dini ya Ibrahim (Abrahamu).
  • Walikataa kuabudu masanamu.
 
Wakristo wengi huwa wanawapenda waislamu ambao hawavai hijabu, ambao hawasali swala tano, ambao wanakunywa pombe n.k. ila ukiwa muislamu unayevaa hijabu, unaswali na unatii maamrisho ya dini yako basi Wakristo wengi hawakupendi.

Hii inasababishwa na kwamba ndani ya nafsi zenu mnaona husuda kwa kuwaona waislamu wanafuata dini yao kikamilifu hali ya kuwa nyinyi mna dini yenu lakini hamuifuati.

Kila mtu abaki na dini yake
Kweli kabisa,waambie hao.😁💪💪
 
Kuna hijab na stara
Hijab ni vazi la kiislamu linatakiwa mwanamke akivaa lisionyeshe maumbile yake , viachie wazi paji la uso na viganja vya mkono
Wanawake wengi huvaa stara sio hijab
Mfano wa hijab ni wale wanaovaa majuba.
 
Back
Top Bottom