makaveli10
JF-Expert Member
- Mar 27, 2013
- 31,583
- 92,670
Sio kwamba hujaelewa ila umeamua kujitoa akili, maelezo yangu yako wazi kabisa.Nielekeze ndugu yangu!
Hapo nimesoma nimeona kaandika suratul Nasri (Idhajaa anasirullahi wal fat hu) akaandika mpaka akaishia kwenye fii dinillahi..
Baada ya hapo akaandika jina la Mungu. Yaani ya Allah! Kaliandika mara 11. Yaani Ya Allah! Ya Allah mpaka idadi ikafikia mara 11.
Baada ya hapo akamalizia sehemu ya aya "Afuwaja".
Baada ya hapo akachora jedwali! Upande mwengine kaandika herufi ya waw ya kiarabu. Kisha akachora symbol kama ya ua.
Huko kwengine kwa upande mwengine wa jedwali kaandika " Allahumma" mara 4.
Kisha kwa chini akaandika maneno yafuatayo "Mola wangu wewe ndiye mpaji na mimi ni mwombaji......" maneno ya kuomba.
Chini yake hapo akamswalia Mtume kisha akaweka na vialama vya nyota na alama alama nyengine.
Umeweka tahadhari kuwa ni ushirikina. Nisaidie kwa hapo ushirikina kinamna gani? Kwa maana na mimi nikiona kama hayo mahali pengine niweze kuwaelimisha watu.
Nimeelezea kwanini hiyo ni shiriki, ama hujaona niliposema hiyo ni shiriki?
SOMA TENA.