Hiki kisa cha huyu mwanaume aliyetembea na shemeji yake kimenifunza.

Hiki kisa cha huyu mwanaume aliyetembea na shemeji yake kimenifunza.

Adi mauki kaingilia kati usifanye mchezo na physiological tougher ila wanaume mkomage na nyie mjifunze kukaa mbali na shemeji zenu mtaja kufa mdomo wazi kisa k japo mwanamke ndo alie muwekea mazingira ya kumtafuna


Mauki anasemaje kuhusu hilo swala..
 
B anatakiwa ahame kabisa huo mji .Huo ukimya utamfanya ateseke sana
 
Tufupishe story tufanye leo tena ni L clouds ni P af gea ni G mke ni a C bakwata ni D na mjumbe ni M wakati huo familia ni F mchumba wa B ni X
fiesta ni Z

ina maana A na B wamesoma na kukua pamoja...A kawah kupata kazi na kumuoa C...A na B ni marafiki wa kufa na kuzikana...A yuko njema anamsaidia B kwa mambo mengi...A anagundua C anampenda B akat ni mkewe...anawawekea mtego na kuwakuta wamebanjuana anamwambia C nimekuwekea 20k mezan ya matumiz....B na C wanasubir reaction ya A na A haonesh kujua lolote...B na C wanadata baada ya muda B anaenda kwa M anaeleza tukio...M anamuita A nae A anamwambia M hakuna lolote na kumsih B atulie....mda unapita B na C wanazid kuoneshwa upendo na A nae B anazid kudata anaenda kushtak kwa F nao F anamwita A nae A anajibu kama alivojibu kwa M linaisha maana F haioni kesi...Inatokea Z af A anamwambia B na C waende kwenye Z wanakubali ila mpaka Z inaisha B na C hawana raha...B anapeleka kesi kwa D nae D anamwita Af A anafanya yaleyale nae D haoni kesi...C anaona A ataniua anakimbia...anabaki B anamtafta G nae G anaipeleka kwa L ambayi ilo ni program ya P kwenye L kuna hekaheka na hapo ndo mtoa mada anajua kilichotokea...tutarud kwa mtoa mada tuendelee kidogo...A anakubali kutoa ukwel kwa G na anasema C alikua anampenda B hivo wakat huohuo B ana X...A hakuona busara kukosana na B akat huenda alitegwa na C...X anataka kuachana na B ila A anawapatanisha na wanaelewana .... kwa maana hio X anamuelewa sana A yajayo yanafurahisha...turud kwa mleta mada..mleta mada anaileta JF na mimi I AM SINA JAMBO nafupisha ...na nyie mnasoma



NB: Watu wengi wanaijua hii adhabu na wanahis ni ya kawaida lakini omba isikukute



I AM SINA JAMBO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana katika leo tena nimesikia kisa cha kusikitisha kiko hivi,
Kuna jamaa marafiki sana toka chuo wanasoma wote marafiki kiasi kwamba hadi wamekuwa kama ndugu na familia zao zimekuwa kitu kimoja.
Walipomaliza chuo wakapanga sehemu moja. A akafanikiwa kupata kazi nzuri kuliko B, akatangulia kununua gari kabla ya B na kumsaidia B kumpush naye apate usafiri.
Wakanunua eneo kwa pamoja mlandizi na kujenga nyumba kila mtu yake ambazo zimetenganishwa kwa ukuta.
A kaoa B ana mchumba lakini wanakuwa wana hang out kila sehemu pamoja. Sasa kwa maelezo ya B siku moja A kasafiri, yeye na shemeji yake wakatoka na kurudi usiku eti shetani akawapitia akamtafuna shemeji na usingizi ukawapatia wakalala, wanashtuka asubuhi A anaingia chumbani kumbe alirudi kimya kimya. A anawambia samahani mke wangu ela ya matumizi ya leo naweka mezani akaweka 20,000 halafu akatoka akaenda kazini.
B akatoka ndani akakimbilia kwake akijua jioni jamaa akirudi itakuwa mgogoro mkubwa sana lakini ajabu jamaa alirudi hajaongelea hilo swala akawa anacheka na anaonyesha kumjali na kumpenda mkewe kama kawaida.
Hapo hapo namwita mshikaji wale na kuchill kama kawaida. B akawa anatamani jamaa aseme neno jamaa hasemi neno hiyo hali ikawa inamtesa akaamua aende kujishtaki kwa mjumbe na kumueleza kisa chote. Mjumbe akamwita A na kumwambia kilichotokea, A akabisha kuwa yeye hajamfumania rafiki yake na mkewe na kama angemfumani na kungekuwa na tatizo wangelimaliza mbona maana yule ni zaidi ya ndugu kwake. kisha akatoka na kumfuata rafiki yake na kumwambia mbona umemwambia mjumbe mambo ya ajabu mimi sina tatizo na wewe.
Jamaa akazidi mshangaa A jinsi alivyokuwa ana behave yani kama hakuna kilichotokea. Siku ya Fiesta akawambia waende Fiesta dar jamaa anadai alikubari maana alikuwa anamuogopa A anashindwa mkatalia wakaenda pamoja na shemeji aliyemtafuna. Anasema yani ile show nzima hakuwa na raha hata kidogo.
Jamaa akaona hapa huyu jamaa au anapanga kuniua ikabidi aende BAKWATA aeleze kisa chote, Masheikh wakamuita A nako akakana kuwa hajawafumania. B akazidi changanyikiwa siku ya mwaka mpya pia akawatoa akaenda nao Bagamoyo anaonyesha ana furaha zote tu.
B anadai kazi hazaiendi chakula hakishuki anazidi kukonda, akaona bora amwambie dadake A hapo ilikuwa imepita week 3, dadake mshikaji akaongea na babake A. So kikaitishwa kikao cha familia, bado A akabisha kuwa yeye hajawafumania. B akampigia magoti asemehewe amemkosea jamaa msimamo wake ni kwamba hajamkosea na wala hajawafumania wala hakumbuki kitu ka hicho.
Jamaa kuona hivyo ikabidi akatoe taarifa polisi wakampa na RB kabisa kisha akamtafuta Gea Habibu ili watu wampe ushauri maana anasema jamaa anawatesa Kisaikolojia walau aseme chochote.
Sasa a alipohojiwa na Gea anadai kwamba yeye alikuwa ashamuona mkewe kuwa anampenda rafiki yake na alikuwa ashahisi kuna jambo linaendela. So hata siku ile ni sawa aliwatega kuwa kasafiri. Ila anadai kwamba yeye hana tatizo na rafiki yake anasema amuombe mungu tu amsamehe yeye hana tatizo na wala hapangi kumfanyia ubaya wowote.
Na akadai jana aliposikia redioni akajua ni rafiki yake na akadai rafiki yake ana mchumba mwaka huu anaoa. Mchumba wa rafiki yake alipojua akataka vunja mahusiano ila yeye mwenyewe jana kawakutanisha B na mchumba wake kawaweka sawa.
Aisee kuna watu wana mioyo aisee jamaa ana moyo ila sidhani kama everything gonna be the same again.
Duuh
 
Najiuliza kama b anahaha hivi je mke anayelala naye na kuishi naye kila sku. eti B anasema siku ya mechi ya simba A alienda chek mechi kwake alikuwa anatamani kufa
Nami nimejiuliza hili maana upande huo haujazungumziwa kabisa
 
Back
Top Bottom