Hiki kiswahili ni cha wapi?

Hiki kiswahili ni cha wapi?

Agogwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2013
Posts
2,742
Reaction score
3,000
Nilikua nasikiliza redio moja hivi ya FM nikasikia maneno yafuatayo
"full mzuka"
"Akampa vitasa"
"Kiroho safi"
"Arachuga"
"Mzeya"
"Amesepa"
hii lugha itakuwa inafananaje baada ya miaka kumi?
 
Hata kamusi ya kiswahili... itaandikwa namna hiyo.
 
nahs kama mtu alokufa miaka ishirini ilopita arudiwe na uhai miaka kumi ijayo hataweza kuelewa waswahli wanazungumza nini
 
kiswahil cha mjini wenyewe wanajiita wajanja
 
"Kama vipi kisanue" maana yake nini?
 
Hii Elimu ya ccm itawasababishia hata kamus ya kiswahili ibadirike.
 
Niko ful mzuka kinomaa.....kiroho safiii....ngoja nisepe kiaina.....
 
"Kama vipi kisanue" maana yake nini?

Nadhani kisanue inatokana na neno sanuka. Sanuka maana yake ondoka kwa haraka au muda huo huo pasipo kupoteza muda au wakati.

Sasa kisanue imekaa kama kitenzi au kielezi hivi kwa mawazo yangu.
 
hawa jamaa was redo mawingu wamechangia kias kikubwa kuharibu kiswahili mfano jamaa anaejiita kijukuu watangazaj wengi wanamuiga
 
Hapa Jf nimejifunza maneno mawili mapya "papuchi" na "mgegedo"
 
"Tisha mbaya" !!!!?????? unahitaji bakora
 
[kila jambo huja nakuondoka lugha uzaliwa na kufa QUOTE]
hiki ni kiswahili cha mtaani kwa lugha fasaha niite lugha isyo rasmi lakini ni maneno ambayo yanazungumzwa katika maeneo ya mjini na wanaopenda sana ni vijana kwani uisi ni kwenda na wakati
 
kama mwandishi wili a habari unatakiwa kuisadia jamii kukua kimadili lakini si kupotosha maadILI
 
Back
Top Bottom