Kidagaa kimemwozea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 3,680
- 6,554
Huyu mdau anasemaje?
Jicho langu: TATIZO LA SIMBA LINAJENGWA NA VIONGOZI
Hakuna anayeweza kubisha kuwa simba ndiyo timu yenye wachezaji bora kwa sasa Afrika Mashariki, Simba inao wachezaji wa kila namna wanaoweza kutengeneza matokeo hata wale ambao hawapati nafasi mara kwa mara bado ni bora na tunaona viwango vyao!
Simba haijafanya vibaya kihivyo lakini viongozi simba lazima muliangalie hili mapema
MNAWAFANYA WACHEZAJI WACHEZE KWA PRESHA KUBWA
Tatizo hili linaondoa kabisa kujiamini miongoni mwa wachezaji na kujikuta wakifanya makosa sana hasa pale wanapotanguliwa goli au kuchelewa kupata goli la kuwa mbele.
Tatizo hili nimeliona kwa michezo zaidi ya minne ambayo simba hakupata ushindi.
Simba vs Ud Songo
Simba vs Mwadui
Simba vs Yanga
Simba vs Mtibwa
Kwa presha waliyonayo wachezaji wa Simba hata wakifungwa goli dakika za mwanzo kabisa hawawezi tena kurudi mchezoni, utawaona wachezaji wakicheza kwa presha, wanapoteza pasi hovyo! faulo za kutosha na kukosa kujiamini ikiwa ni pamoja na kukosa kutengeneza nafasi za magoli au kukosa magoli ya wazi.
Viongozi wa Simba kumbukeni kuwatia presha wachezaji hasa katika mitandao ya kijamii haiwasaidii; watieni moyo, hakuna mchezaji anayependa matokeo mabovu.
Aidha, kwa sasa ili kuinusuru Simba itawabidi kutafuta matibabu ya kisaikolojia kwaajili ya wachezaji ili warudishe kule kujiamini hata pale wanapokuwa nyuma waweze kupindua matokeo.
Leo sitaandika sana.
Masshele Emanuel