GE2025 Hiki ndio kilifanywa na wasimamizi wa uchaguzi ili kupata 98% ya kura za Samia

GE2025 Hiki ndio kilifanywa na wasimamizi wa uchaguzi ili kupata 98% ya kura za Samia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwenye vituo vingi watu hawakujitokeza kupiga kura kutokana na wananchi wengi kujiapiza kutoka kwaajili ya maandamano kupinga uchaguzi huo dhalimu. Kwenye sehemu ambako watu walijitokeza kwenye maeneo mengi walikuwa hawafiki 50.

View attachment 3497190

Sasa kufika jioni ambako wasimamizi walikuwa wanafanya majumuisho ya kura kwenye vituo husika na kuwasilisha kile walichopokea kwenye vituo vyao, wasimamizi wakuu walitoa order ya karatasi zilibaki zote zijazwe.

View attachment 3497191

Yaani kama ulikuwa na karatasi 40 unaambiwa zote utiki kwa Samuya na wabunge, madiwani wa CCM. Ukikataa kufanya hivyo unatishiwa maisha au hata kuharibiwa kazi yako, hivyo kwa hata hao wachache waliojuta kusimamia uchaguzi walishiriki udhalimu huyo na Samuya akatangazwa kushinda kwa asilimia hizo!

Ila unajua nini, hii haitapita hivi hivi, wananchi tutajibu haya yote yaliyofanyika. Samuya na genge lako mjue tu siku zenu zimeisha, Mungu asipoingilia tutamsaidia kuonesha njia kuhakikisha kila damu iliyomwagwa italipwa.

​
View attachment 3497192
View attachment 3497194
Uko sahihi kwa kiasi kikubwa. Na haya ni yaliyofanyika ndani kituo cha kupigia kura

Lakini, the fact ni kuwa kila kitu kilishapangwa mapema kwamba apate kura asilimia ngapi bila kujali watu watajitokeza kupiga kura au la!

Mimi ni shuhuda na nilikuwa msimamizi wa Moja ya kituo cha kupigia kura Kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga

Nilishiriki hatua zote kuanzia ktk kituo cha kupigia kura, kwenye kituo cha majumuisho katani (diwani) na jimboni (mbunge na kupata kura za Rais za Jimbo zilizotumwa kwa Tume HQ Ili kutangazwa)

👉Mpango (target) kitaifa wa INEC ulikuwa ni lazima Samia Suluhu Hassan apate ushindi wa kishindo (kama watambavyo wenyewe) wa kura asilimia 98, na hapa ni aidha watu wapige ama wasipige kura🤔🤔

👉Target hii ikawa broken into pieces na kupewa wasimamizi wa majimbo kuwa lazima Jimbo lako lifikie target hiyo. Mfano Jimbo letu lilikuwa na target hiyo hiyo ya 98% bila kujali watapiga kura au la🤔

👉Target hii ikashushwa kwa ma ARO (Assistant Returning Officers) wa Kata kuwa lazima Kata yako ije na ushindi wa 98% wa Samia bila kujali watapiga kura au hawatapiga..🤔

👉Hawa ma ARO wa Kata nao wakaishusha hiyo target kwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura. Kila kituo kilipewa target yake straight ikilenga hiyo hiyo 98% ya kura za Urais. Za mbunge na diwani, Hakukuwa na target maalumu lakini iwe isiwe msimamizi wa kituo cha kupigia kura hakikisha mbunge na diwani wa CCM anapata kura nyingi zaidi ya 90% bila kujali wamekuja au hawakuja kupiga kura🤔🤔

HALI KITUONI KWANGU ILIKUWAJE?​

1. Kituo changu Y kilikuwa na wapiga kura walioandikishwa 389

2. Mpaka kufikia saa 10:00 jioni muda wa kufunga kituo kisheria Hakukuwa na mpiga kura yeyote na waliokuwa wamefika na kupiga kura tayari waliokuwa 44 tu kati ya 389 sawa na 11.31%

KILICHOFUATA BAADA YA HALI HII​

👉Tuliletewa hiyo target ya kura za Rais kwamba, fanyeni vyovyote iwezekanavyo ionekane walipiga kura ni 365 na Samia apate kura 345 katika hizo!!

👉Kusema kweli ilikuwa kazi ngumu sana isiyowezekana kirahisi. Tulichofanya huku tukijua kuwa makaratasi ya kupigia kura hayana maana na kazi yoyote, tulichana kura zote kwenye vitabu na kutumbukiza kwenye masanduku. Hatukurekodi namba za wapiga kura kwenye vibutu kwa sababu muda ulikuwa hautoshi na shinikizo ya kuwasilisha matokeoharaka likiwa kubwa sana likiambatana na vitisho vya kila namna.

👉Tulichofanya ni kujaza takwimu (number) walizozitaka kwenye fomu za matokeo yao. Hatukujisumbua hata kidogo kuhesabu kura zile 44 halali zilizopigwa. Tuliona kuwa haikuwa na maana yoyote kwa kuwa matokeo yalikuwa tayari yameshaandaliwa!!

Hivi ndivyo mchezo huu hatari ulivyochezwa na hawa wahuni. Mimi binafsi naomba rehema na huruma ya Mungu Yehova anisamehe kwa kushiriki kutenda dhambi hii dhidi ya Watanzania wenzangu. Nina amani tele moyoni maana nimesamehewa na kufutiwa kabisa makosa haya!

👉Kama matokeo ya Urais yangekuwa yanajojiwa mahakamani, basi masanduku ya kura huko yalikohifadhiwa yamejaa uchafu mtupu usioendana hata kwa 0.001% tu na uhalisia wa matokeo yaliyotangazwa na INEC ya Mwambegele. Kwa UFUPI, Urais wa Samia ungekuwa nullified with immediate effect!!
 
Ni kweli kuna jamaa yangu alisema walipewa kazi ya kutiki karatas zote ambazo watu walijiandikisha lakini hawajujitokeza
 
Wewe Baki na ukweli wako nasi tubaki na ukweli wetu.

Waliosimamia uchaguzi ni ndugu na jamaa zetu.
Mimi mwenyewe nilisimamia uchaguzi hebu acha upumbavu wako, unaongea mambo ambayo hayapo
 
Maku kweli wewe, tuoneshe foleni ya kupiga kura iliyokuwa na hata wapiga kura 20 kwa wakati mmoja kwenye uchaguzi wa juzi!
Pumbavu sana wewe, pomole mkubwa, eti watu 20 pimbi wewe, sisi mstar mmoja ulikuwa na watu zaidi ya 150
 
Takwimu za kura zilitengenezwa kwenye ofisi za halmashauri siku kabla ya uchaguzi,walikuwa wanachukua mfano kata fulani wamejiandikisha watu fulani,takwimu zilitengenezwa haswa kwenye ngazi ya urais
 
Back
Top Bottom