Hiki ni kiti cha dhahabu alichokalia Malkia Victoria wakati anaapishwa

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
1652567571409.png

Ilibidi miguu ya kiti itengenezwe mifupi kwasababu Malkia Victoria alikua mwanamke mfupi kwa umbo, wasingeweza kuweka miguu ya kiti mirefu na kumuacha Malkia akining’inia.

Baada ya Victoria alitawala mtoto wake Edward, nae alipokewa na mtoto wake George V aliyerithiwa na mtoto wake Edward ambae ilibidi aachie kiti baada ya kumuoa mwanamke wa Kimarekani tena aliyetalakiwa. Kitendo hiki kilisababisha Albert ambae ni baba yake Malkia Elizabeth kuapishwa kama Mfalme George wa sita.

Sasa hivi Malkia Elizabeth katika umri wa miaka 96 jua limezama na nguvu za kutawala zimemwishia. Mtoto wake Charles anajiandaa kuapishwa. Nimeona kiti cha enzi kimetolewa inawezekana kinapigwa msasa kwa maandalizi ya sherehe ya kusimikwa rasmi kwa Charles kama Mfalme.

Charles atataka miguu ya kiti iongezwe? Wakati kiti kinatengenezwa Uingereza ilikua na Madola 3/4 ya dunia, hivyo kupata dhahabu ya kutengeneza kiti cha Enzi haikua shida. Sasa hivi mambo yamebadilika. Hata dhahabu ikipatikana wana harakati watapaza sauti na kuhoji ulazima wa kutumia dhahabu kutengeneza miguu ya kiti cha Mfalme.

1662995494417.png
 
Incase akidondoka haya yafuatayo yameshaandaliwa.

Baada ya kifo cha Malkia mtu wa kwanza kupewa taarifa ukitoa wanafamilia na madaktari, atakuwa ni secretari wa Malkia mwenyewe Sir Christopher Geidt. Baada ya hapo atamtarifu waziri mkuu na baadae maafisa waandamizi wa serikali kwa kutumia sentensi THE LONDON BRIDGE IS DOWN taarifa hii ataituma kwa kutumia simu maalumu.

Baada ya hapo ofisi ya mambo ya nje itatoa taarifa kwa nchi zote wanachama wa jumuia ya Madola ambazo Malkia ndio kiongozi mkuu, vyombo vya habari vitatarifiwa kupitia Umoja wa vyombo vya habari, shirika la habari la Uingereza( BBC) na baada ya kupata taarifa hizo waendesha vipindi watalaazimika kupiga wimbo maalumu kama maandalizi ya kutoa habari hiyo! Kuna habari kuwa vyombo vya habari vya The Times na Sky News vimekuwa vikifanyia mazoezi oparesheni hiyo huku wakitumia jina Mrs Robinson badala ya Malkia Elizabeth II.

Baadae taarifa ikiwa kwenye karatasi itawekwa kwenye geti la kuingilia kasri la Buchngham ambayo ndo offisi kuu ya ufalme wa Uingireza na muda huo huo tovuti ya Buchngham itaweka taarifa hiyo na Bunge litaitishwa ikiwezekana ndani ya saa moja ambapo waziri mkuu atalihutubia bunge la makabwela( The House of Commons). Siku moja baada ya kifo cha Malkia Elizabeth II baraza maalumu kwa ajiri ya kumuidhinisha Mfalme au Malkia mpya litakutana katika kasri la S. James na jioni ya siku hiyo bunge litakutana kwa ajili ya kumuidhinisha Mfalme au Malkia mpya!

Utaratibu kama Malkia atafia nje ya Kasri la Kifalme la Buckngham Kama atafia kwenye kasili la Windsor ambalo ni sehemu ya Mali za ufalme au kwenye Nyumba ya Sundningham ambayo ni Nyumba binafsi ya Malkia Elizabeth II, basi mwili wa Malkia utapelekwa Buchngham kwa gari. Kama Malkia atafia nje ya Uingereza basi mwili utapelekwa Uingereza na kikosi cha “The No:32 (the Royal) Squadron” ambalo ni jeshi maalumu la anga kwa ajiri ya familia ya kifalme kupitia uwanja maalumu ulioko eneo la South Ruislip!! Kama Malkia atafia kwenye kasri la Balmoral liliopo Scotland mwili utapelekwa kwenye Cathedral ya mtakatifu Giles na baadae kuchukuiliwa na treni maalumu ya kifalme na kuletwa mjini London! Katika mazingira yoyote yale mwili utachukukiwa na kupelekwa katika kasri la Buckingham ndani ya siku 4.

Mwili wa Malkia utaagwa kitaifa katika eneo la “Westminster abbey” siku tisa baada ya kifo na baadae atazikwa kwenye Jeneza katika kanisa la Mtakatifu George lililopo kwenye Kasri la Windsor.
 
ulivomchorea kifo chake km jiwe ilivokuwaga
 
Je zoezi la kuchapisha noti mpya na stemp mpya zenye picha ya mfalme au malikia mpya hufanyika wakati gani baada ya umauti kumkuta malkia aliyeko mamlakani
 
Siku hizi watu hawasomi vitabu wako busy na umbea wa Whatsapp!

Na mzungu alitengeneza hizi whsp insta style na the likes plus malinks kuwakamata wavivu wa kiafrika wasioependa kusoma wenye kupenda summary badala ya details.
Na anatupiga sana kwa kutoyachimba maarifa
 
Back
Top Bottom