Hiki ni nini? Naombeni ushauri nachanganyikiwa. Nimekopa Milioni 14 natakiwa kurudisha Milioni 39

Easy money is expensive 🤐
 
Mikopo yote riba huwa kubwa kafri miaka ya kurudisha inavyokuwa mingi, mm nlikopa 20 mil nqrudisha 24,000,000/= ila makato yake sasa ni miaka 3 tu ila nakoma
Mtoa mada aliyemshauri aende huko(Bank hiyo)[emoji134] hahhhaha...mbona Bank za kawaida zina unafuu, pia mkopo unachukua siku mbili tatu kuingia, na hazina mambo mengi.

Hii tunaita lack of information.
 
Yaani Hapo ukitafuta Interest Rate ya mkopo wako ndo utajua umepigwa kinyama wamekugaragaza kikatili sana miksa magumashi kibao .

Umeingia kwenye mkataba kama wa chief mangungo
 
Utasaidikaje sasa hapo?
Humu kuna vijana walibarikiwa na walikaa darasani na wanatoaga elimu ya haya mambo ya mikopo vizuri kabisa anakufundisha kama mtoto mpaka unaelewa vyote ila sasa nyie ndo mnaokimbiliaga uzi wa kula kimasihara tu. Pole sana
 
Au ungeomba Mungu ww ndo ufe ili usilipe mkopo
 
Mkuu, ukikupendeza naomba muongozo wa Bank mojawapo yenye unafuu wa riba za mikopo, hata Kama ni Islamic Bank.
 
Basi loan ofisa anapiga hesabu anakuambia kwa pesa yako utauwezo wa kukopa sh mil 20 ambayo mkononi utapata mil 12....ukishasema tu tawire mpunga unaingia deni linasoma mil 40 kwakweli hicho kipengele namie huwa sijakielewa
MaAfisa mukopo wahun sana[emoji23]....wana take advantage za shida za watu, hawatoi maelezo ya kujitosheleza..ni wabinafsi.

Ila wako baadhi, ni very innocent.
 
Ila wafanyakazi [emoji119]

Mimi mfanyabiashara nikitaka kukopa lazima nikae chini na Loan officer anidadavulie kiunagaubaga mambo yote yaliyopo kwenye karatasi..

Yaani unaendaje kukopa bila kujua unarudisha nini? Interest rate yako na mwisho wa marejesho ni kiasi gani!
Faida ya ulichokopa itakua yako au ya Bank?

Pole una namna ilipe tu
 
Mmi nilichukua mkopo Kwa succoss 4ml Kwa maika 2 full burudan
Nakatwa 197470 per month

At the end ntalipa 4.75m

Watu ukiwaambia saccoss na vikoba hata hawaelewi

Mimi Nina vicoba viwili kila kimoja ninaweza kukopa 10M
Riba inarudishwa kwenye account yangu japo muda wa marejesho siyo mrefu sana ila napunguza stress Za kuneemesha mabank
 
Huo ni uongo uongo uongo tena nakuomba uufute mwenyew acha kuzalilisha t... ABC hapo lengo lako ni kuwaharibia biashara watu
 
Safi sana mkuu kam ningepata ushauri kama huu mwaka 2014 sijui ningekuaje
 
1. Mkuu inamaana huko ulipo hamna NMB au CRDB?

2. Halafu wewe ni mwalimu wa Aina gani? Inamaana hukuambiwa makato ni kiasi gani Kwa mwezi?

Ukakopa tu?

Pathetic

Wakati wenzio Kwa makato hayo wanakopa zaidi ya Milioni 20.
Umeongea kama vile muelewa kumbe hamna kitu,

Sasa Apo NMB na CRDB ndo unadhani mkopo kwa kipindi cha miaka 8 utakua tofauti?

Nenda bank nyingine waombe waununue mkopo wako na ubadilishe vigezo uombe kulipa ndani ya miaka miwili au mitatu. Riba itakua ndogo ila makato yatakua makubwa

Mfano, ukitaka kuilipa deni lote ndani ya mwaka, utalipa makadirio ya 16,240,000 utakua umeshamaliza kila kitu. Ila ndo ujue kila mwez marejesho yatakua mil 1 laki 3 na ushee..

Ongea na afisa mkopo wako akupe elimu zaidi na huduma zingine za mikopo zilizopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…