Hiki ni nini? Naombeni ushauri nachanganyikiwa. Nimekopa Milioni 14 natakiwa kurudisha Milioni 39

Hiki ni nini? Naombeni ushauri nachanganyikiwa. Nimekopa Milioni 14 natakiwa kurudisha Milioni 39

Nimevumilia ila nimechoka acha niwaambie, ndugu walimu nimekopa ABC bank shilingi milioni 14 nikatwe kwa miaka nane sawa na miezi 96, nakatwa shilingi laki nne na elfu 14 kwa mwezi.

Nimeshangaa kukuta kwenye salary slip deni ni milioni 39😥😥😥, nimelia sana yaani nakopa 14M narudisha 39?
Mimi kwakua nilikua nina dharula ya haraka sana nilienda ABC maana niliambiwa kule hauzunguki sana na nilipofika niliongea nao tu muda ule ule nikajaza fomu nikaondoka mkopo ukaingia kesho yake, najuta sikupata muda wa wenda kusoma makubaliano na wala hawakunipa nakala yoyote!

Hii sio haki serikali iko wapi jamani?

Nifanyeje naombeni ushauri wenu.

View attachment 2744997
Easy money is expensive 🤐
 
Mikopo yote riba huwa kubwa kafri miaka ya kurudisha inavyokuwa mingi, mm nlikopa 20 mil nqrudisha 24,000,000/= ila makato yake sasa ni miaka 3 tu ila nakoma
Mtoa mada aliyemshauri aende huko(Bank hiyo)[emoji134] hahhhaha...mbona Bank za kawaida zina unafuu, pia mkopo unachukua siku mbili tatu kuingia, na hazina mambo mengi.

Hii tunaita lack of information.
 
Utasaidikaje sasa hapo?
Humu kuna vijana walibarikiwa na walikaa darasani na wanatoaga elimu ya haya mambo ya mikopo vizuri kabisa anakufundisha kama mtoto mpaka unaelewa vyote ila sasa nyie ndo mnaokimbiliaga uzi wa kula kimasihara tu. Pole sana
 
Mleta mada umenikumbusha miaka ile kipindi Corona ndo inaingia wakazusha kwamba watu watakufa wengi !
mwanaume nikajirusha bank kuvuta mkopo wa 7M fasta tena na riba kubwa halafu pesa yote nikakimbilia kuwekeza kwenye biashara yangu ya majeneza nikijua misiba itakuwa mingi nirudishe mtaji na faida matokeo yake watu wakawa hawafi halafu ikafika kipindi Corona ikawa kama haipo hivi yaani sintosahau mateso ya yale marejesho ya kila mwezi ilifika mahali nikawa sina ujanja wa kupata marejesho nikauza kagari kangu(kama kale ka Mr. Bean) ndo nikamaliza deni la mkopo mpaka leo hii sitaki kabisa kusikia kitu kinaitwa mkopo!
Au ungeomba Mungu ww ndo ufe ili usilipe mkopo
 
Kuna bank zinazojiendesha bila riba.

Yasingekukuta hayo.

Tatizo mmelazimishwa muogope kila mkisikia uislam.

Ktk huduma inayofahamika kama murahaba mnaweza kukubaliana na bank wananunua huduma kule unaokoenda kupeleka pesa.
Kwa kukuuliza kwa malipo kidogo kidogo na kwa bei juu kidogo.

Haiwezi kabisa kufikia ongezeko kama hilo
Mkuu, ukikupendeza naomba muongozo wa Bank mojawapo yenye unafuu wa riba za mikopo, hata Kama ni Islamic Bank.
 
Basi loan ofisa anapiga hesabu anakuambia kwa pesa yako utauwezo wa kukopa sh mil 20 ambayo mkononi utapata mil 12....ukishasema tu tawire mpunga unaingia deni linasoma mil 40 kwakweli hicho kipengele namie huwa sijakielewa
MaAfisa mukopo wahun sana[emoji23]....wana take advantage za shida za watu, hawatoi maelezo ya kujitosheleza..ni wabinafsi.

Ila wako baadhi, ni very innocent.
 
hahahahhaja Mpwayungu Village unaskia apa
Atafanya nini sasa....
Screenshot_20230908-194509.png
 
Ila wafanyakazi [emoji119]

Mimi mfanyabiashara nikitaka kukopa lazima nikae chini na Loan officer anidadavulie kiunagaubaga mambo yote yaliyopo kwenye karatasi..

Yaani unaendaje kukopa bila kujua unarudisha nini? Interest rate yako na mwisho wa marejesho ni kiasi gani!
Faida ya ulichokopa itakua yako au ya Bank?

Pole una namna ilipe tu
 
Mmi nilichukua mkopo Kwa succoss 4ml Kwa maika 2 full burudan
Nakatwa 197470 per month

At the end ntalipa 4.75m

Watu ukiwaambia saccoss na vikoba hata hawaelewi

Mimi Nina vicoba viwili kila kimoja ninaweza kukopa 10M
Riba inarudishwa kwenye account yangu japo muda wa marejesho siyo mrefu sana ila napunguza stress Za kuneemesha mabank
 
Huo ni uongo uongo uongo tena nakuomba uufute mwenyew acha kuzalilisha t... ABC hapo lengo lako ni kuwaharibia biashara watu
 
Deni lolote benki kama si kwa matumizi ya kibiashara ni hasara tupu!! Ili mtu afanikiwe kutokukopa benki inabidi awe na mkakati huo tangu mwezi wa kwanza wa ajira yake. Iko hivi: Amua kuishi kwa kadri ya kipato unachopata. Amua kuweka 250,000/= benki kama akiba ambazo uhesabu kuwa hazipaswi kuingia kwenye matumizi yako. Panga chumba cha bei rahisi kimkakati, kula kimkakati na vaa kimkakati. Ukifanikiwa zoezi hili kwa miaka 5 utakuwa una akiba ya sh 15,000,000/=.

Hapo unaweza kuanza kukopa toka kwenye akiba yako mwenyewe, na zoezi la kutunza 250,000/= kwa mwezi liwe endelevu muda wote uwapo kazini. Mkakati huu unawezekana tu kama ukiuanza mwanzoni kabisa mwa ajira yako. Usikubali kuiga maisha ya watu, unajua wenzio watakopa benki na kuanza kuendesha magari, kununua vitu vya kifahari nk, hao watakutisha kwa miaka 5 tu basi!! baada ya miaka 5 utakuwa na akiba ya kukutosha kufanya vitu vya kimaendeleo. Lakini usipokuwa na mikakati hiyo utajikuta unalazimika kukopa ili kupeleka watoto shule, kununua kiwanja na kuanza ujenzi wa nyumba!! Ukikwepa mikopo utaokoa mamilioni ya riba ambazo wakopaji hulazimika kulipa. Utafanikiwa kupata vitu walivyopata wenzio bila gharama ya riba.

Lakini ukijiingiza kwenye mikopo, utajikuta unakuwa mkopaji muda wote uwapo kazini. Unakopa marejesho kwa miaka 8 kabla hujamaliza unapata shida nyingine unafanya top up, na mchezo huo huendelea hadi mtu anastaafu. Hutakwepa kukopa kama hutafanya mkakati wa ku-save pesa from day one!!
Safi sana mkuu kam ningepata ushauri kama huu mwaka 2014 sijui ningekuaje
 
1. Mkuu inamaana huko ulipo hamna NMB au CRDB?

2. Halafu wewe ni mwalimu wa Aina gani? Inamaana hukuambiwa makato ni kiasi gani Kwa mwezi?

Ukakopa tu?

Pathetic

Wakati wenzio Kwa makato hayo wanakopa zaidi ya Milioni 20.
Umeongea kama vile muelewa kumbe hamna kitu,

Sasa Apo NMB na CRDB ndo unadhani mkopo kwa kipindi cha miaka 8 utakua tofauti?

Nenda bank nyingine waombe waununue mkopo wako na ubadilishe vigezo uombe kulipa ndani ya miaka miwili au mitatu. Riba itakua ndogo ila makato yatakua makubwa

Mfano, ukitaka kuilipa deni lote ndani ya mwaka, utalipa makadirio ya 16,240,000 utakua umeshamaliza kila kitu. Ila ndo ujue kila mwez marejesho yatakua mil 1 laki 3 na ushee..

Ongea na afisa mkopo wako akupe elimu zaidi na huduma zingine za mikopo zilizopo.
 
Back
Top Bottom