Hiki ni nini? Naombeni ushauri nachanganyikiwa. Nimekopa Milioni 14 natakiwa kurudisha Milioni 39

Usikope utakuwa desparate ,usikope ni dhuluma ya mifumo ya bank .

Usikope achana na riba utafilisika hapa duniani.

Usikope ni mtego jaribu kubangaiza kuishi ndani ya bajeti kuwa na watoto hata wawili wanatosha.

Mikopo unapewa ukiwa na ndoto ambazo hautotimiza kabisa.

Mikopo ni hatari sana.
 
Benki gani hizo
 
Huo ni unyonyaji wa hali ya juu, ukisikia watu wanatumia shida zako kama fursa kwao ndiyo hivi sasa. Hebu turudi kwenye mada Ina maana na wewe shida zilikufanya ukawa kipofu mpaka ukashindwa kusoma mkataba wa makubaliano baina Yako na bank? Hapo huna wa kumlaumu yakupasa kuvumilia TU na kujifunza kupitia makosa
 
Kila siku tunatoa ushauri humu acheni kukopa kwenye taasisi uchwara za kifedha hamsikiii..hawa ABC,Platinum sijui..Bayport ni kausha damu haswa..
Nakubaliana na wewe hayo majamaa yanaitwa PLATNUM CREDIT ni matapeli haswa. Yana kauli ya kuvutia wateja ukiingia kwenye 18 zao utajua hujui. Nawaombeni ndugu zangu msije mkaingia kwenye mkenge wa kukopa haya matapeli.

Mfano yanakwambia hv gari lako mkopo wako. Yatakusainisha mkataba wa maajabu. Ukipitisha rejesho la mwezi kidogo wanakuja kukukamatia gari popote hata kanisani hayajali. Baada ya wiki yanatangaza kwenye magazeti gari inauzwa kwa mnada

Wapumbavu sana hao matapeli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…