Hiki ni nini? Naombeni ushauri nachanganyikiwa. Nimekopa Milioni 14 natakiwa kurudisha Milioni 39

Kwa kifupi hapo huna Cha kufanya,umesaini mkataba na hela umewekewa,ukirudi kwao ukasema unataka kulipa yote sahizi kwa mkupuo watakukwambia tupe 39m,unachotakiwa ni kujifunza tu kutokana na makosa
Sio kweli mkuu. Akitaka kulipa leo ataomba barua inayoonesha "Outstanding loan" deni halisi bila riba atapewa haizidi 14M na faini kidogo
 
Milioni 14 ya Leo ni kubwa kuliko milioni 39 kwa miaka hiyo nane ijayo.


Pambana na hali yako
 
Mwl. Nyerere
Mwl. Magufuli
Mwl. Majaliwa
Mwl. Ndalichako
Mwl. Kitila Mkumbo
Mwl. Doto Biteko
Mwl. Jenister Mhagama
Mwl. Mwinyi
Mwl. Seif Sharif
Orodha ni ndefu sana
 
Hazina usiri, mara nyingi mkopaji hatafuti/hasomi taarifa za kutosha bali hulenga pesa tu na jambo analikopea pesa humsukuma....
Basi loan ofisa anapiga hesabu anakuambia kwa pesa yako utauwezo wa kukopa sh mil 20 ambayo mkononi utapata mil 12....ukishasema tu tawire mpunga unaingia deni linasoma mil 40 kwakweli hicho kipengele namie huwa sijakielewa
 
Mkuu Early settlement fee kawaida inatakiwa isizidi kiasi gani?
Maana kuna loan officers janjajanja sana
Kila bank ina fees zake lakini ni around 5%-10% ya principal amount iliyobaki. Hata hivyo kama una settle from your cash unaweza kusettle for free ukiongea nao.
 
Tatizo ni kutojirizisha kabla ya kufanya maamuzi ya kuchukua mkopo !!

Usipokuwa mdadisi usitegemee utapewa maelezo ya kutosha !!! Hiyo ni sawa na 23% FLAT INTEREST RATE kwa Mwaka (Au 32.85% REDUCING BALANCE INTEREST RATE kwa mwaka). Yote hayo ungeyajua kama ungekuwa mdadisi, maana gharama sio riba tuu bali zipo na nyinginezo ambazo hukatwa kabla ya kuingiziwa pesa kwenye akaunti yako kutegemeana na aina ya Benki/Mkopo !!

Hapo dawa ni kulipa tuu !!!
 
Umeelewa kilichoandikwa na ulichoandika vina tofauti gani?
 
Ccm mbere kwa mbere
 
Mkuu fafanua hizo rate zinakujaje?
 
Kwa kifupi hapo huna Cha kufanya,umesaini mkataba na hela umewekewa,ukirudi kwao ukasema unataka kulipa yote sahizi kwa mkupuo watakukwambia tupe 39m,unachotakiwa ni kujifunza tu kutokana na makosa
Hi si sahihi, ukweli ni unarusiwa kufuta au kuhamisha deni muda wowote kwenye hizi bank. Wanangalia mpaka Siku unafuta au kuhamisha bado unadawai Kiasi gani kwenye Ile principal (14Mil Kwa hii kesi) na penalty kama ipo, kumbuka kila mwezi unaporusha pesa unalipa sehemu ya principal+riba. Hii unaweza kuwa katika mtindo wa flat au reducing rate.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…