Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,509
- 16,734
Tuliposikia kuwa ujumbe mzito wa Saudi Arabia umekwenda Iran kuonana na akina AyatoLllah,tulifurahi na kupata tamaa kwamba sasa waislamu wameanza kuwa wamoja hasa ukijua mataifa hayo mawili kila moja lina nafasi yake kubwa katika ulimwengu wa kiislamu kidini,kisiasa na kiuchumi.
Ujumbe huo ulikuwa ni wa mwanamfalme Khalid bin Suleiman aliyetumwa na baba yake akaonane na viongozi wakuu wa Iran kushauriana nao jambo fulani muhimu.Hatimae kikao hicho kilifanyika mnamo Aprili 17 lakini kumbe ilikuwa ni ushenga na ukuwadi kwa ajili ya Marekani na Israel.
Eti alikwenda kupeleka salamu kutoka Marekani ikiwa imebaki wiki chache kwa raisi Trump kutembelea mataifa ya mashariki ya kati.Alitakiwa awaambie Iran kwamba ikubaliane na matakwa ya Marekani ya kutaka ifanye mazungumzo nayo ili kusitisha urutubishaji wa madini ya Uranium.
Mwana mfalme huyo bila aibu akaiambia Iran isipofanya hivyo inahatarisha kushambuliwa kwa vinu vyake vya nyuklia kutoka kwa Israel jambo ambalo litaiingiza mashariki ya kati yote kwenye majanga makubwa.
Sababu nyengine ya kuhofia mashambulio hayo ni kwa vile eneo hilo limeshachoka na janga linaloendelea huko Gaza..Na sijui wana kipi cha kuzungumzia na kuogopa kuhusiana na Gaza wakati hawajawahi kufanya juhudi yo maana kuingilia na kusitisha vita hivyo.
Undani wa kikao hicho haukutolewa na upande wowote kati yao,hata hivyo kutokana na kilichofuata katika mikutano ya Marekani na Iran kuhusiana na mada hivyo ambapo Iran imesimama kidete kutetea haki yake ya kubaki na vinu vyake,inaonesha siku kikao hicho kilipofanyika Iran ilimdharau sana mjumbe huyo na kumuona akifanya upatanishi na vitisho vya kishoga shoga.
Kwa kifupi kukubali kutumwa kama mtoto kwenda kumtisha mtu ambaye mwengine anamuogopa ni dalili ya upungufu wa kiakili kwa watawala wa Saudia na ni tusi kwa waislamu sote.