Ni kweli kabisa mkuu, nakubaliana na wewe kuwa wamewahi kuibua mambo mengi ya kweli huko nyuma kama hilo la enzi za Mwendazake. Lakini hoja hapa si kuwabeza au kuwakatisha tamaa.
Hapa wengi tunachokifanya siyo kumkatiza tamaa bali ni kumkumbusha ajiangalie sana na hizo taarifa anazozipata sasa hivi. Uaminifu wake ni mtaji mkubwa, hivyo asipochuja vyanzo vyake anaweza kulishwa vitu vya uongo ili aonekane hana credibility.
Pia kuna suala kubwa la kiusalama hapa ambalo watu hawalioni: Haohao wanaompa hizo taarifa ndiyo wanaoweza kutumika kumjua alipo au nyendo zake. Wabaya wake wakitaka kum-track, njia rahisi zaidi ni kutumia na kudokeza watu wanaowasiliana na Maria Sarungi.
Kwa hiyo, ushauri wa yeye kujitathmini ni kwa ajili ya kulinda uaminifu wake na usalama wake binafsi, siyo kumvunja moyo