macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 29,500
- 61,451
Hii account ya ''Tanzania Leaks'' ni bomu na mimi huwa siamini chochote wanachoandika. Ni mtu anatumia sensational rumours kuandika na anaokoteza chochote. Mimi kusma ukweli Mange huwa nampa credit kuhusu credibility za anachoandika. Huwa ni makini sana kwenye kuchambua vyanzo vyake na inaonekana ana vyanzo vya uhakika.Kuna siku akaunti ya Twitter ya "Tanzania Leaks" waliandika Jaji Warioba amefungiwa nyumbani kwake chini ya ulinzi.
Nilikuwa naona haya maneno yanajirudiarudia nikawa nayapuuzia tu, lakini, siku hiyo nikasema nisije kuwa napuuzia tu halafu kuna kitu kinatokea sijui.
Nikaamua kuitolea uvivu habari. Nikavunja mwiko wangu wa kuzungumzia siasa za Bongo na mwanangu mmoja wa familia.
Nikamcheki mtu wa familia, akaniambia mbona mzee yuko poa tu hana shida.
Nikasema kwenye sheria kuna kanuni ya "innocent until proven guilty", lakini kwa hawa wanaharakati naigeuza hii kanuni, inakuwa "guilty until proven innocent".
Kauli zao siziamini mpaka nithibitishe.
Naam,ni Bora tujue tunasafari ndefu lakini tuwe katika mchakato sahihi..Na moja ya nyezo za mchakato sahihi ni taarifa sahihi ..Lakini Hawa wanaharakati ni kama wana ajenda Yao nyingine
Walishakimbiaga hapa hawaji wamejazana Instagram na Twitter. Ukiwakosoa wanaku block. Mimi nilisha blokiwa hata na mange kosa langu lilikua siamini kama kumwambia Trump aje abomu Tanzania ni njia nzuri. Akani blockJe humu JF wamo hawa watu?
ID zao zipi tuwa tag?
Hapo nani mwehu zaidi?Nikweli mkuu , yaani mtu unajipanga kusherekea kifo cha mkwere. Ghafla unamuona eti anatoa speech..Maamae zao
Swala ni trust, aliamini akipost taarifa za kifo cha jk wafuasi wake watashangilia..So Kuna haja Gani ya yeye kutoa taarifa za uongo.Hapo nani mwehu zaidi?
Hakika mkuuMaria Sarungi ni hot head. Ni rahisi sana kutumika na madhalimu kwa ajenda zao bila yeye kujua. Bahati mbaya ana wafuasi watiifu mno, alipaswa awekwe kando kwa muda hadi ajifunze kuchunga mihemko yake.
Wewe MWEHU endelea kuzifungia tu KENDE waache Madada wa TAIFA waikimbize sirikali ya SAMUYA.vidume coconut tukiwa tumezifungia kende zetu baridi ndani,
Ni kweli inaonekana hivyo maana alisema wazi ni mzima, baadaye mwenzake akaja kusema sio mzima na ametumia taaluma yake ya uandishi kuwa anaumwa. Masaa machache baadaye mzee anaonekana hewani.Hii account ya ''Tanzania Leaks'' ni bomu na mimi huwa siamini chochote wanachoandika. Ni mtu anatumia sensational rumours kuandika na anaokoteza chochote. Mimi kusma ukweli Mange huwa nampa credit kuhusu credibility za anachoandika. Huwa ni makini sana kwenye kuchambua vyanzo vyake na inaonekana ana vyanzo vya uhakika.
Ni kweli kabisa mkuu, nakubaliana na wewe kuwa wamewahi kuibua mambo mengi ya kweli huko nyuma kama hilo la enzi za Mwendazake. Lakini hoja hapa si kuwabeza au kuwakatisha tamaa.Pamoja na uongo wao lakini pia wameibua madudu mengi sana ya kweli
Nakumbuka enzi za Mwendazake waliibua anaumwa sana lakini jiwe akaibuka kuapisha watu na baada ya hapo akapotea mazimaa
Umenena vyema sana, hapa ni kukumbushwa awe makini na vyanzo vyake, kwa kilichotokea atakuwa ameelewa vyanzo vyake vinampotosha kwa sababu wanazojua wao.Ni kweli kabisa mkuu, nakubaliana na wewe kuwa wamewahi kuibua mambo mengi ya kweli huko nyuma kama hilo la enzi za Mwendazake. Lakini hoja hapa si kuwabeza au kuwakatisha tamaa.
Hapa wengi tunachokifanya siyo kumkatiza tamaa bali ni kumkumbusha ajiangalie sana na hizo taarifa anazozipata sasa hivi. Uaminifu wake ni mtaji mkubwa, hivyo asipochuja vyanzo vyake anaweza kulishwa vitu vya uongo ili aonekane hana credibility.
Pia kuna suala kubwa la kiusalama hapa ambalo watu hawalioni: Haohao wanaompa hizo taarifa ndiyo wanaoweza kutumika kumjua alipo au nyendo zake. Wabaya wake wakitaka kum-track, njia rahisi zaidi ni kutumia na kudokeza watu wanaowasiliana na Maria Sarungi.
Kwa hiyo, ushauri wa yeye kujitathmini ni kwa ajili ya kulinda uaminifu wake na usalama wake binafsi, siyo kumvunja moyo