Hilda Newton: Nimepokea taarifa kuwa Mohamed Issa amefikishwa Mahakama ya Uhujumu Uchumi

Hilda Newton: Nimepokea taarifa kuwa Mohamed Issa amefikishwa Mahakama ya Uhujumu Uchumi

Kutoka account ya X ya Hilda Newton:



Nimepokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bavicha Taifa Wakili Advocate Mahinyula

Anasema kwamba leo Mohamed Issa amefikishwa Mahakama ya Uhujumu Uchumi upande wa Jamhuri wakasema kwamba hawana nia ya kuelendele kesi hivyo Mohamed akaachiwa lakini cha kusikitisha akakamatwa tena na Polisi na sasa wanampeleka Mahakama ya Kisutu

NB: Enzi za Magufuli Mwaka 2019 Mohamed Issa akiwa kaimu Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Pwani alikamatwa na Polisi wakambambika kesi ya Uhujumu Uchumi. Kwasababu kesi yake haikuwa na dhamana so akapelekwa gereza la Segerea ambako amekuwa akiishi kama Mahabusu mpaka leo.

Katika kipindi chote iko cha miaka 7 leo ni mara ya tatu upande ya Jamhuri wanasema hawana nia ya kuendelea na kesi wanamwachia halafu wanamkamata tena na kumshtaki kwa kosa hilo hiloHuu uonevu lazima ufike mwisho, mwachieni kijana wa watu kama ni kumtesa basi mmeshamtesa vya kutosha.
Wakati wa Lissu kuonesha umwamba wake, alisema yeye sio Mbowe laini laini. Hatokubali mwanachadema kuonewa
 
Alipowekwa ndani kwa miaka yote hiyo Mbowe alikuwa wapi?! Mbona hamkumlilia Mbowe amsadie? Leo mnaleta maneno maneno ya nongwa?!
Mbowe alilamba asali…. Tunawataka mashujaa akina Lissu wamtoe kinguvu
 
Kamata peleka ushahidi ahukumiwe bas! Si vinginevyo
Haya mambo yana utaratibu wake, kazi ya kutafuta ushahidi sio rahisi, wape nafasi, justice hurried is justice burried
 
Alipowekwa ndani kwa miaka yote hiyo Mbowe alikuwa wapi?! Mbona hamkumlilia Mbowe amsadie? Leo mnaleta maneno maneno ya nongwa?!
Mbowe kashindwa ndio maana akapewa lissu, cha ajabu Lissu yupo hotel bagamoyo habari za maandamano ya kumtoa kijana hayapo
 
Back
Top Bottom