Hili bango karibu na Ubalozi wa Ufaransa limenifikirisha

Hili bango karibu na Ubalozi wa Ufaransa limenifikirisha

Juzi nilipita maeneo ya karibu na Ubalozi wa Ufaransa nikaona bango moja limeandikwa "Kifo cha Imam Husain kinatukumbusha umuhimu wa Uhuru". Huwa nina kawaida nikiona mabango ya dini napendaga kufuatilia zaidi maandiko yale hasa kama kuna ujumbe ambao umenigusa wakati huo.

Ila kuna kitu zaidi kilinigusa pale. Miaka kama 2 iliyopita kuna jamaa mmoja aliyejulikana kama "Hamza" alizua taharuki maeneo yale akarushiana risasi na polisi hadi akauawa. Hili tukio huwa nalikumbuka kila nikipita maeneo yale.

Baadae nilivyotulia nikasema embu ngoja nigoogle kama nitapata maarifa yoyote kuhusu maandiko yale na nimejifunza machache ya kunipa mwanga kidogo:

"Iman Hussein alikuwa mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Imam Hussain (as) aliyeuawa Karbala, Iraq , siku ya Ashura."

"Alisimama kidete dhidi ya mtawala dhalimu wa wakati ule, Yazid bin Muawiya, akatoa fundisho la kukataa kumpigia magoti mdhalimu huyo, Ndipo akajitolea maisha yake, akauawa ili kunusuru ubinaadamu na utu."

"Imam Hussein (a.s) hakujitoa Muhanga yeye na familia yake kwa ajili ya Ummah wa Kiislam tu, bali alijitoa muhanga kwa ajili ya manufaa ya Ummah wote duniani."

Sasa mimi sina shida na maandiko hayo wala ndugu zangu wenye imani tofauti na mimi. Nimewaza tu busara ya kuweka bango lile mahali pale ukizingatia kumbukumbu ya tukio lililotokea mazingira yale na hapa simaanishi kama tukio lile lina uhusiano wowote wa masuala ya imani maana sidhani kama tuliwahi kuambiwa hivyo.

Kwa kumalizia, natamani kujifunza Uislamu. Naomba mwongozo naweza kuanzia wapi.
Team picha
 
Vipi msimamo wako kuhusu maulid? Maana kuna watu wanatoka povu hadi kuandaa munaqasha. Mimi sio muisilamu ila huko mitandaoni huwa nashuhudia malumbano si ya kitoto kuhusu maulidi, wengine wakisema ni ushirikina
Wanaofanya wafanye wasiofanya wasifsnye.

Mie nikikuta pilau naipiga tu, siasa zao watajuwana wenyewe.
 
Hiyo mitaa si ndio pia wafia dini walijilipua kwenye ubalozi wa Marekani....kuna vingine nadhani huwa havitokei kwa bahati mbaya...
 
somo limeeleweka, umeandika kwa hekima na busara kubwa sana, tena bila jazba na munkari. Na mimi naandika, hilo bango halikuwekwa pale hivi hivi tu, kuna ujumbe zaidi ya huo ulioandikwa hapo linatoa. Akili akilini katika kufikiria
 
Hiyo mitaa si ndio pia wafia dini walijilipua kwenye ubalozi wa Marekani....kuna vingine nadhani huwa havitokei kwa bahati mbaya...
Ndiyo hapo hapo mkuu, upande mmoja tukio katika ubalozi wa ufaransa, upande wa pili ubalozi wa Marekani
 
Back
Top Bottom