Hili bunge limejaa washenzi na wahuni sijapata kuliona toka tupate uhuru, Rev. Mtikila

Hili bunge limejaa washenzi na wahuni sijapata kuliona toka tupate uhuru, Rev. Mtikila

Nasikia kuna mjumbe katinga na wife wake.
na kuna mwingine anawakilisha wachawi

hili bunge la ajabu sana
nasikia kuna akita mwita wawili wanatumia jina moja wote wamelamba posho

na wote wako Dodoma wanatafutiwa ukwel yupi ni yupi ?
 
Nasikia kuna mjumbe katinga na wife wake.
na kuna mwingine anawakilisha wachawi
Na yeye amejitetea eti mke wake ni mwanachama halali wa NLD hivyo ana haki ya kuchaguliwa na kuwaambia wale wa Zanzibar walizembea hawakupeleka jina ndio maana kwenye chama chake wakachaguliwa wawili toka bara bila mwakilishi wa Zanzibar. Ila patamu hapo maana machungu ya posho hayaonekani hapo kwani wana-share room ala posho inayobaki inaingia kwenye income generating activities (hivi vyama wakati mwingine ni kama SACCOS za watu flani maana hata kama ni mwanasiasa inatakiwa uwe na shughuli nyingine inayokuingizia kipato lakini wanasiasa wetu ni tofauti kabisa na ndio maana wakiingia huko wanawaza kuongeza posho)
 
Tatizo lake baniani mbaya kiatu chake kizuri......(POSHO) kama ni kweli angekataa uteuzi....
 
DUH, KUNA SIKU MKULU atajilaumu kkwa nini alikubali kufanya uteuzi badala ya wajumbe kuchaguana wenyewe bila mkono wake, yakitokea mambo ya kihuni kama anayosema Mtikila lawama itaepukwaje kwa mteuzi?
 
Inategemea sana nani aligharamia hicho kikao cha wanaoitwa wasomi na alitaka kitoe msimamo gani! Ajabu ni kuwa kwa nini hawakupendekeza na kutetea kwa nguvu Serikali moja wakati tume inakusanya maoni na kuandika rasimu?
Nakubaliana nawe kwa hili kwani akulipae ndio akuchagulie nyimbo ya kuimba. Sasa nakubaliana na kauli ya Mtikila.
 
tatizo ukimshtaki kwa hiyo maneno anakushinda na fidia unamlipa yeye LOL
 
Back
Top Bottom