ANGALIZO KWA WANAO AGIZA BIDHAA TOKA NJE YA NCHI
- Nimeagiza mzigo toka USA na umesafirishwa na hawa TNT
- Ghalama zao walizonipa ili mzigo utoke, zimenishangaza, ni kubwa kuliko makampuni yote niliyowahi kutumia kuagiza mzigo toka nje ya nchi.
- Nimefanya mazungumzo na mhusika kwa njia ya simu na akasisitiza hata kama ni mzigo wenye thamani ya DOLA 1 hizi kwenye picha ndio ghalama nitakazopaswa kulipia. Tazama picha
Kwa Ufupi
- Mzigo nilio agiza una thamani ya dola 162.97
- Shipping cost dola 44
Je ni sawa kweli?
Ndugu
Brakelyn tafadhali nipe uzoefu wako mzigo wako ulipo kuja kwa TNT ghalama zilifanana na hizi nilizopewa?
Bado natafakari nini cha kufanya kuhusu hatma ya huu mzigo
Nawakilisha
pole sana
[HASHTAG]#Mwl[/HASHTAG].RCT ,
hili ni jambo muhimu sana kuzingatia wakati wa kuagiza mzigo kutoka nje. Mimi pia nilishapatwa na wakati huu mgumu kama wako na nikagundua yafuatayo. Mpaka sasa nina uzoefu wa miaka 6 kufanya online shopping kupitia website mbali mbali zinazouza bidha mbali mbali.
Njia za usafirishaji ninazotumia kusafirisha mizigo yangu kutoka nje
Mara nyingi kuwa nachagua mizigo yenye njia ya usafirishaji ninayopendelea zaidi otherwise huwa nawaomba sellers wanitumie mizigo kupitia Courier companies ninazotaka. Mimi huwa ni mvumilivu, naweza kusubiri hata siku 45 ilimradi nipokee mzigo kwa gharama kidogo. Mizigo mingi napendelea itumwe kwa USPS, Royal Mail, EMS, Austr.Post, Singapore Post, China post (baadhi zinaangukiwa kwenye economy Int'l na Standard Int'l Shipping) etc (hizi zote huniwezesha mimi nipokee mizigo kwa njia ya sanduku langu la posta ). Huko posta mzigo ukifika tu, nitakacholipa ni ushuru pekeyake tena kwa mizigo ambayo iko subjected to Customs Duty. Hii inanipa unafuu kwasababu kuna mizigo mingi midogo hailipiwa ushuru, vile vile naokoa gharama za clearing, sjui tbs, clearing etc. ambazo zinaongeza gharama ya mzigo wako. Vile Vile naweza kuongea na muuzaji huko nje akapunguza value ya invoice kwenye parcel na ikanipunguzia gharama ya ushuru pale itakapofika posta (japo ni illegal).
Uzoefu wangu na hizi express shipping companies (DHL-FedEx-UPS-TNT etc)
Mpaka sasa nimeshatumia DHL,FedEx na UPS.
Experience na FedEx.
FeDeX niliitumia kuingiza simu yenye thamani ya $200 mwaka juzi na sikulipishwa ushuru. Sijawahi kutumia tena FedEx hivi karibuni.
Experience na UPS
UPS nimepokea mzigo mara moja tu na sintorudia tena kutumia UPS kwa sababu zifuatazo. Mzigo ulikuwa na thamani ya $65 na bei ya usafirishaji ilikuwa $420.22 labda sababu ya uzito wa mzigo (Nilinunua kwasababu hata jumla ya gharama haikufikia bei ya dukani huku Arusha).
baada ya mzigo kufika JKN Int Airport Dar, customer service wa UPS wakanipa computation za kufanya clearance ya mzigo wangu na ilikuwa kama ifuatavyo:
1. Ushuru 112,000/=
2. Handling 30,000/= (wakaniambia eti TBS)
3. Handover fee 57,000/=
4. 80,000/=
Total ikaja kama 279,000/= hivi. Nikalipa tu sababu nilikuwa nikiuhitaji sana.
Experience na DHL
Nimepokea mizigo mara nyingi sana kupitia DHL. Hivi karibuni nimepokea mzigo wenye thamani ya $150 na nimechajiwa ushuru wa shilingi 115,000/= tu ofisi za DHL Arusha na nikapokea mzigo wangu.
Huu mwingine una thamani ya $200 na juzi dhl wanipa estimation za ushuru wa 141,800/= kutoka customs. Hivi sasa navyoReply post yako nipo njiani kuelekea DHL kuupokea.
Experiance na TNT bado ili nashukuru sana kwa kunipa experience yako. kwahyo TNT ni kama hawa UPS tu. Umenisaidia nimewaongeza kwenye blacklist yangu.
Conclusion yangu ni kwamba, baadhi ya hizi kampuni za usafirishaji za nje zimekuwa na gharama zisizo na maana kabisa. Unakuta mizigo ni ya aina moja na ina thamani, uzito, dimension za package ni hizo hizo lakini ukipokea kupitia courier companies tofauti unapata gharama tofauti za ukomboaji. Nachoamini kwa mizigo midogo midogo hakuna haja ya kulipa clearing fee, handling, sjui handover fee. Maranyingi naagiza spare mpya za magari kupitia DHL na ni nzito, thamani kubwa kuliko hiyo nilipitisha kwa UPS lakini bado napata unafuu kuingiza kwa DHL. (TBS costs bado sijajua DHL wanakwepaje) lakini so far naona ndio courier company inayoeleweka kwangu mpaka sasa kwasababu gharama nayolipa kwao ni ya ushuru tu.