MakinikiA
JF-Expert Member
- Jun 7, 2017
- 5,840
- 8,202
Faili za Epstein zinaibua kumbukumbu ya 'nyakati za uchungu mwingi katika ndoa yangu' - Melinda Gates
Chanzo cha picha,AFP via Getty Images
Bilionea Melinda French Gates amesema mumewe wa zamani, mwanzilishi mwenza wa Microsoft Bill Gates, aliyetajwa katika faili mpya zinazohusiana na marehemu Jeffrey Epstein, kunanikumbusha "nyakati za uchungu mwingi katika ndoa yangu".
Aliambia kipindi cha NPR kwamba "amehuzunishwa sana" na madai ya Epstein na kwamba watu waliotajwa akiwemo mumewe wa zamani, wanahitaji kuwajibishwa.
"Ninafurahi sana kuwa mbali na uchafu huu," alisema. Wanandoa hao walitalikiana mwaka wa 2021 baada ya miaka 27 ya ndoa.
Rekodi zilizotolewa na idara ya sheria ya Marekani zinajumuisha madai ya Epstein kwamba Bill Gates aliambukizwa ugonjwa wa zinaa ambaye ameyaita madai hayo "upuuzi mkubwa".
"Madai haya - kutoka kwa mwongo mkubwa na mwenye chuki - ni ya kipuuzi na ya uwongo kabisa," msemaji wa Bill Gates amejibu kuhusu madai hayo. BBC imewasiliana na wawakilishi wake kuhusu maoni ya mke wake wa zamani.
Bill Gates hajashutumiwa kwa makosa na yeyote kati ya waathiriwa wa Epstein na jina lake kujumuishwa kwenye faili haimaanishi kuhusika kwa vyovyote na matendo ya uhalifu. Katika mahojiano na podikasti ya NPR ya Wild Card, Melinda French Gates alisema: "Kwangu mimi binafsi, ninakuwa hali ngumui kila maelezo ya namna hiyo yanapojitokeza, sivyo? Kwa sababu yanarudisha kumbukumbu za nyakati zenye uchungu mwingi katika ndoa yangu."
Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kwamba kabla ya kutengana kwao, Melinda French Gates alikuwa amekasirika juu ya uhusiano wa mumewe na Epstein. Baada ya kutengana kwao kutangazwa, Bill Gates alikiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mfanyakazi wa Microsoft mnamo 2019.
Madai hayo kuhusu Bill Gates yalijumuishwa katika zaidi ya hati milioni tatu zilizotolewa wiki iliyopita na Idara ya Sheria ya Marekani.