Hili jambo limenitatiza na kufanya niwe na wasiwasi za vijana wa iPhone

Hili jambo limenitatiza na kufanya niwe na wasiwasi za vijana wa iPhone

6321

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2016
Posts
649
Reaction score
1,117
Nawasalimu kwa JMT

Katika mizunguko ya duniani nikichomwa n jua maeneo ya magomeni mwembechai, nikiwa dukani alikuja rafiki yangu niliyesoma nae O'level akiwa na mwanamke wa umri kidogo kuliko yeye, niliwahudumia vitu vya jumla kama 100k+.

Basi tukabadilisha mawasiliano, akaniambia yeye anaduka la iphone makumbusho. Tukawa tunawasiliana pia nilifanikiwa kufika kwenye hilo duka. Tulikaa pale kama saa 1 n ushee, kulikuwa n vijana 3 n mabinti 2 ukijumlisha na sisi wa 2 tulikuwa 7. Kwa nilivyoona hapakuwa n mteja na mabox yaliopangwa sikuona lenye simu hata moja.

Miez ikapita kadhaa, jamaa akaja dukani tukapiga story sana, akaniambia mzigo wake umekwama bandari hivyo hela imepelea kama 200k, kwa kuwa ni mwana nilifika alipodai ni duka lake, nikamwambia nitakukopesha 150k ndio ipo ya chap. Kilichofata ni kalenda, chenga kwa wingi hadi leo hii ni mwezi wa pili hela hajaleta, nilifika dukani washkaji wakaniambia ukweli maana nilienda na barua ya wito kutoka polisi.

Hiki ndio walichoniambia "Wote unaotuona hapa +huyo unaemdai wote ni mawinga" Nikauliza winga ni nani? Nikaambiwa ni madalali.

Kwa roho moja niliamua kusamehe.

Kama umewahi kukutana na maksa kama huu njoo tujikumbushie.
 
Mzee nielekeze ulipo tuifuatilie hiyo pesa. Mimi utanipa 50K tu. Amekudhulumu pesa nyingi sana.
Pesa sijashindwa kuifatilia, ila nilivyoenda na barua ya wito, nikapewa maelekezo niiache hapo dukani. Wale wenzake waliniambia ukweli nikaelewa hali halisi yao. Sikuona haja
1. Polisi walianiambia nilichokosea sikuandikishana nae, maana sina ushahid
2. Kwa uapnde wangu busara nikatumia baada ya kusikia m dalali yani n hohe hahe
 
Huyo kitaalam sisi makocha wa mpira tunamuita LWF left wing forward sana sana huwa wanaatumia miguu yote ila wenye nguvu ni mguu wa kushoto kwaajili ya kupiga cross akiingia kwenye box akakupiga chenga 1 ukikubali ndo tayari umelia mpira utaukuta kwenye nyavu Jamaa kajiajiri huyo katumia mbinu nzur tu akiwapata watu 10 kama wewe tayar ana 1.5M
 
Pole Sana kiongozi,watu sio watu siku hizi we waone tu walivyo. Ila kuna siku mtakutana tu na hapo ndo utamwambia hukutegemea hakufanyie vile.
 
Jamaa kajiajiri huyo katumia mbinu nzur tu akiwapata watu 10 kama wewe tayar ana 1.5M
Ndugu pesa ya namna hiyo haiwezi kukufikisha popote sana sana ni hela ya kula na kudanganyia wanawake lakini sio hela ya kukuinua na kukuendeleza.
 
Ndugu pesa ya namna hiyo haiwezi kukufikisha popote sana sana ni hela ya kula na kudanganyia wanawake lakini sio hela ya kukuinua na kukuendeleza.
Sure mkuu.

Maana hauwezi kua na constant supply ya hiyo 1.5M as hauwezi kuwarudia watu na huwezi kuwawin kila siku.
 
Back
Top Bottom