Hili jambo ndilo ambalo lilinishtua Baada ya Kifo cha Magufuli

Hili jambo ndilo ambalo lilinishtua Baada ya Kifo cha Magufuli

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Mafisadi Nchi nzima Yalifurahi sana. Yalifanya sherehe na kushukuru. Hapa nikafunguka macho. Huyu mtu kwa nini alichukiwa na Mafisadi? Hili lilinishtua sana.

Nikaanza kujiuliza upya ni wapi nlikosea. Ndiyo....ni wapi nlikosea maana mimi mara ya kwanza sikuwa nakubaliana na mambo kadhaa ya Magufuli. Lakini hapa katika hili Check Engine taa ikawaka. Nikagundua kuna namna.

Sasa ndo naelewa. Naona jinsi ambavyo watu wamekuwa vigeu geu. Hali ya maisha imekuwa ngumu. Panya road wamechukua nchi, ajali kila kukicha, watu wanauana na kujiua kutokana na ugumu wa maisha.

Ambao HAWALALAMIKI NI WALE WANAOLAMBA ASALI TU. HIKI NI KIPINDI AMBACHO VIONGOZI WENGI WAMETULIA. SI KWA WOGA. LA HASHA. KWA KUWA WANALAMBA ASALI.

wananchi wao wanalamba Shubiri...itawasaidia wapone. Tunakoenda hali itakuwa mbaya zaidi. Magufuli hakuwa Malaika... Ila alisaidia nchi ikawa inaeleweka. Sasa inakwenda mzoba mzoba. Inchi imefunguliwa kwa mikopo isiyo na Tija.

Tozo zimekuwa kama zote na ufanisi hakuna. Hata Saa mbovu mara mbili kwa siku inasema ukweli. Job Nduga mmoja ya Spika wa hovyo kupata kutokea Nchini. Alisema ukweli.
 
 
Magufuli alikosea sehemu ndg Sana.

Kuwatesa wafanyakazi. Kuwajali bodaboda na machinga. Angemjali japo nurse na mwalimu angekuwa amemaliza. Tatizo aliwawea kwenye kapu la wenye nacho.

Polisi wanahali duni, na manurse na walimu. Hao wengine Wana posho za nyumba, simu na maji.

Hakutakiwa kabisa kuwatenga Hawa ndiyo watu wa halibya chini, angekuwa na jeshi kubwa nyuma yake.

Watumishi hawakumuunga mkono kipindi cha pili Kwa sababu alidai hawanaumuhimu kwake.
 
Magufuli was a genius, patriotic and visionary leader.

Ni aina ya viongozi wachache kutokea si kwa level ya nchi, bali Afrika kwa ujumla. Ni kundi la viongozi wachache wana mapinduzi kama Muhamar Gadafi, tukichukia mifano ya viongozi wa hivi karibuni.

Kwa jinsi dunia ilivyotawaliwa na “mabeberu” ilikuwa ni vigumu sana kwake kuongoza muda mrefu. Bahati mbaya propaganda za kumchafua zilitawala sana kwenye vyombo vya habari kwa kuwatumia wanaharakati na wapinzani. Lakini ukweli unabaki palepale, Jinsi watanzania walivyoomboleza kifo chake inadhihirisha walivyompenda.

Walimpenda kwa sababu alileta mabadiliko makubwa licha ya propaganda za kumchamfua. Mfano kwenye uchumi hakuamini kutoza kodi kubwa kwa wananchi maskini na kuwaacha matajiri wenye kuingiza vipato vikubwa. Kodi ilikusanywa sana lakini kulingana na mapato. Matajiri waliozoea kukwepa kodi walitozwa kwa mujibu wa sheria, japo baadhi walipiga kelele kwamba wanaonewa.
 
Huyo Marehemu kafanya Jambo gani la maana zaidi ya Upuuzi wa kuuwa watu na kuteka
Lete ushahidi kaua watu na kuteka.

Miaka hii tuliyonayo si umesikia kuna watu wametekwa na kuokotwa kwenye viroba pia. Kuna waliokamatwa kwa makosa feki kama kina mwenyekiti wa maisha, awamu ya 4 kuna waliomwagiwa tindikali, waliouwawa, waliotekwa, mbona hujamnyooshea mkubwa fulani kidole?

Au una maslahi upande huo kwenye asali?

Jadili mada, usimuandame aliyekuwa Rais wa mfano.
 
Magufuli alikosea sehemu ndg Sana.

Kuwatesa wafanyakazi. Kuwajali bodaboda na machinga. Angemjali japo nurse na mwalimu angekuwa amemakiza. Tatizo aliwawea kwenye kapu la wenye nacho...
Kipindi cha kwanza alipata 59% kipindi cha pili 80% kwa hiyo nini point yako hapo? Au ulitaka aongeze mshahara 23% halafu wake wakute 2.3%?
 
Magufuli was a genius, patriotic and visionary leader.

Ni aina ya viongozi wachache kutokea si kwa level ya nchi, bali Afrika kwa ujumla. Ni kundi la viongozi wachache wana mapinduzi kama Muhamar Gadafi, tukichukia mifano ya viongozi wa hivi karibuni...
Magufuli hakuwa kiongozi na wala hakuwa na uwezo wowote.

Magufuli alikuwa mwizi fulani, mwongo na DIKTETA aliyetumia UJINGA wa Watanzania walio wengi wakamuona eti ni shujaa.

Kama unataka kutawaliwa na Magufuli kufa na wewe utamkuta huko kuzimu akakupe uwaziri wa Nishati.

Midubwasha aina ya Magufuli haitokuja kupata nafasi kamwe kwa Tanzania yetu
 
Kipindi cha kwanza alipata 59% kipindi cha pili 80% kwa hiyo nini point yako hapo? Au ulitaka aongeze mshahara 23% halafu wake wakute 2.3%?
Kwa hiyo huyu aliyewawekea 2.3 ndiye mweny nafuu?? Kimsingi nchi hii inawenyeww
 
Back
Top Bottom