Hili jani lina kazi gani?

Hili jani lina kazi gani?

Kubangua mkorosho kwa maana ipi Chief? Kama ni magome, akishayabangua anatafuna ama kuchemsha?
Nimesahau kumalizia

Unabangua then unayachemsha kama chai na maji. Kisha unayaacha yapoe. Unayaweka kwenye chupa kama ya uhai hivi. Unakuwa unasukutua mara kwa mara. Huwezi amini zile magome ninayo zaid ya ten years. Kwanza nishayatumia mara nne hivi. .
 
Habari za mchana wandugu,

Nyumbani kwangu kumeota mmea flani hivi. Kuna mshikaji alikuja home kunisabahai akaniambia linaitwa Kongwa huko Zanzibar. Akasema huko kwao Tanga linaitwa msharifu. Anadai kuwa huu mmea unatumika kuua nguvu za uchawi na waganga wengi sana.

Sikutaka kumuliza maswali huyu jamaa kwa sababu ni dereva nimempatia bodaboda. Binafsi sikutaka kuweka mazoea ya karibu kupitiliza. Ila nimebakiwa na maswali kichwani na najua huku jamiiforums hakukosi wajuzi.

Je, una idea na hiii kitu? Je, kama kweli linatumika kuua uchawi napenda kujua limatumikaje.

View attachment 2550648
Wewe naona roho ya wale Wabrazil inakutafuta ili utetemeshwe na Jehovah Nissi.
 
Wewe naona roho ya wale Wabrazil inakutafuta ili utetemeshwe na Jehovah Nissi.
Kwani kuuliza kuna ubaya mbona mnatafsiri sana🤣🤣 Hili jani Mungu kaliumba kama majani mengine na tunayatumia kutengeneza dawa nyingi tu. Je kuna ubaya kuuliza?
 
Msharifu au Mchawi hana akili ni majani hayo hapo,
Kwa mimi naijua kama Dawa nzuri sana ya Sikio nimeshuhudia watu wengi wakitumia na kupona hasa watoto wadogo, ambao kuwapa madawa ya hospital sio nzuri sana kwa umri wao,
Lakini wengine wanaisifia kwa kufukuza wachawi, kutoa nuksi na mikosi, kichaa cha kurogwa na hedhi ile ya kurogwa,
Na wengine wanaitumia kwa kushusha sukari, mawe kwenye figo, kikohozi kikali na kikavu, kidonda sugu na miguu inayowaka moto, n.k

Msharifu ni mti mzuri kua nao nyumbani, kwanza unapendeza machoni (kwa mapambo) pili ni dawa hasa kwa huduma ya kwanza (tiba) tatu rahisi kulipanda (jani lake ukiliweka kwenye udongo au unyevu
linaota)

Screenshot_20230319-112711_Google.jpg
Screenshot_20230319-112649_Chrome.jpg
 
Kwa kua napenda kukaa na wazee kupata busara zao, basi nitawauliza kuhusu hilo jani lako nitakurejeshea majibu,
Uwe na subira tu
 
Alichoshindw kujua nimeuliza ili kupata maarifa mapya. Hata wakati watu wanatengeneza vidonge kutoka kwemye mimea kuna watu walisema Tiba ya kweli ni Yesu pekee. .
Na wana ndugu zao wametundikiwa drip kibao za kwinini mahospitalini wangali wakijua yesu yupo.
 
Back
Top Bottom