Hili jina la "Mwamba" limekaa kimagumashi sana, ni sifa za kimchongo na kipuuzi

Hili jina la "Mwamba" limekaa kimagumashi sana, ni sifa za kimchongo na kipuuzi

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Mimi siku zote nimekuwa nikifahamu "mwamba" ni mtu jasiri, mwenye kuweza kupambana katika hali ngumu sana na mambo ya kutisha au kugofya, sasa huwa nashangaa hata watu midebwedo kabisa wanaitwa au wanaitana mwamba.

Yani yule mtu ambaye hata akisikia mbwa koko anabweka ghafla anaweza kuanguka kwa presha au kutimua mbio unakutwa anaitwa mwamba!
 
Usipende kufanya kila kitu kuwa complicated, vitu vingine vinasemaka just for fun na sio kimkakati zaidi.

Take it easy man
 
Acha makuzi Basi

Yani upo siriasi kabisa mwamba na huu uzi wako?
 
Utaskia Mwamba huyu apa...
Ukiskia hivyo ujue walikua wanakusema either kwa uzuri ama kwa ubaya
 
Haina tofauti na watumiaji wa JF kuitana wakuu / mkuu wakati anayeitwa mkuu hajawahi kuwa kiranja shule ya msingi.
 
Back
Top Bottom