Hili la Bandari zetu kubinafsishwa kwa muda na 'conditions' ambazo hazijulikani, tuviachie vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama

Hili la Bandari zetu kubinafsishwa kwa muda na 'conditions' ambazo hazijulikani, tuviachie vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama

Burkinabe

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2023
Posts
2,354
Reaction score
4,024
Asalaam Aleykum wana jamvi,

Ama baada ya salamu hizo nidondoke kwenye mada tajwa hapo juu.

Kiukweli suala la kubinafisha (??!kumilikisha) Bandari zetu, ni suala ambalo limeibua hisia za Watanzania wengi wazalendo wa dhati (na wasio na uzalendo wa dhati).

Ni suala ambalo kwa kweli kwa kila Mtanzania anayejielewa, lazima ahoji au awe na maswali mawili matatu ( hata kama ni ya kujihoji au kujiuliza mwenyewe; kikubwa hoja au maswali).

Hili suala linakuwa tata zaidi hasa kutokana na usiri unaoambatana na mkataba wenyewe na terms and conditions ambazo haziko wazi. Mojawapo ya vipengele ambavyo binafsi naona kingekuwepo, basi kingenipunguzia maswali na wasiwasi, ni kipengele cha muda wa kubinafsisha (kumilikisha) itakuwa ni miaka mingapi?

Maana wanaotetea wamekuwa wakiwashambulia wale ambao wanasema tunaenda kumilikisha/kubinafsisha kwa miaka 100 (karne!) kwa madai kwamba hicho kipengele hakipo kwenye mkataba. Sasa swali langu na Watanzania wenzangu wenye mtizamo kama wangu tunahoji, Je, tutamilikisha/kubinafsisha kwa miaka mingapi? Au ndo tunawapa waimiliki milele (kwa muda usio na kikomo)?

Swali la pili, ukiupitia kwa makini mkataba, utagundua tayari ulishasainiwa, Je, bungeni umepelekwa ili kupewa tu baraka za wabunge? Swali la nyongeza, wabunge watakataaje mkataba ambao tayari ulishasainiwa toka mwaka jana; 2022?

Je, usalama wetu kama nchi utakuwa katika hali gani endapo jamaa wakiamua hakuna Mtanzania yeyote kutia mguu wake kwenye himaya yao?

Kwa nini huo Mkataba uhusu tu Bandari za ukanda wa bahari na maziwa ya Tanzania bara tu na wala siyo Tanzania visiwani (Zanzibar).

Anyway, hayo ni maswali machache ambayo nimeamua kujiuliza binafsi.

Pamoja na hayo, nawaomba Watanzania wenzangu, tuviamini vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.

Tanzania ni moja ya nchi zenye vyombo bora kabisa duniani katika medani za Kiulinzi na Usalama. Hii huenda ni kwa sababu ya misingi imara waliyoiweka waasisi wa Taifa hili.

Kwa hiyo,, kutokana na ubora huo, na uzalendo wa viongozi wanaoviongoza na viapo walivyoapa kulinda na kutetea maslahi ya nchi hata ikiwezekana kwa kulipia gharama ya maisha (kifo), nina imani kabisa kwamba tuko katika mikono salama.

Ee, Mwenyezi Mungu, naomba kwa niaba ya Watanzania wenzangu, uwaongoze na uwape hekima viongozi wetu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Wape ujasiri wa kukabiliana na wanasiasa wenye tamaa. Wape uwezo wa kutambua kwamba, wamewekwa kwenye nafasi zao kwa ajili ya kuwalinda wananchi wenzao pamoja na nchi yao na wala siyo viongozi waliowateua tu.

Nawapenda sana Watanzania wenzangu. Nina amini Mungu anaipenda sana nchi yetu na kamwe hawezi kuruhusu kutupeleka tena Utumwani. Hata hivyo Tanzania imechangia kwa kiasi kikubwa sana kuleta uhuru wa nchi nyingi za Kiafrika. Ee, Mwenyezi Mungu, tunaomba fadhila hata kwa hilo tu.

Ahsanteni sana.

AMIN.
 
Attachments

Tatizo viongozi wote wa hivi vyombo vya ulinzi na usalama wanateuliwa na hawahawa matapeli waliopuiga mnada bandari , na wengi wa viongozi wa mihimili wameteuliwa kwa fadhila , sifa za hivyo vyeo hawana ,
 
Hapo ndo changamoto zinapoanzia, kupewa nafasi kwa sababu Mzee wako alikuwa mtu fulani!!
 
Hao DP nao wanapaswa kuwa na wasiwasi. Kuna mada humu kuwa wana makesi kibao na nchi nyingine halafu wanakuja kuweka hela zao kwenye nchi ambayo raisi ajaye anaweza tuma kikosi maalum kudhibiti bandari halafu wakafungue kesi nyingine.
 
Sidhani, havina historia hiyo. Zaidi, tumeshuhudia vikitumia mabavu na vitisho kuhakikisha CCM inabaki madarakani.
 
Historia inaonesha hawawezi kufanya lolote. Uhuni wa namna hii ulishafanyika hapo kabla na hakuna walichofanya.
 
Hao DP nao wanapaswa kuwa na wasiwasi. Kuna mada humu kuwa wana makesi kibao na nchi nyingine halafu wanakuja kuweka hela zao kwenye nchi ambayo raisi ajaye anaweza tuma kikosi maalum kudhibiti bandari halafu wakafungue kesi nyingine.
Wenzetu weupe (wazungu, waarabu, wahindi, wachina n.k), huwa wana kitu kinaitwa, 'taking calculated risks', ambacho kwa kweli huwa kinawasaidia sana.. Wanakuwa na uhakika wa faida watakayoitengeneza ndani ya miaka miwili au mitatu inakuwa kubwa kuliko walichokuwa wamewekeza!
 
Mkuu Usalama wa Taifa umewekwa siku hizi chini ya Rais Nani amuhoji mwajiri wake.
 
Installation tu ya vifaa itachukua zaidi ya hiyo miaka 2. Wanabakiwa na less than 4 years za kufanya kazi kabla raisi mpya hajaja ambaye hawajui atakuja na mipango gani. Unless sheria mpya ya usalama wa taifa iwe na kipengele cha kumdhibiti raisi.
 
Mkuu Usalama wa Taifa umewekwa siku hizi chini ya Rais Nani amuhoji mwajiri wake.
Hivi kwa nini Hii Idara nyeti isingeachwa huru?
I mean haikutakiwa kuwa chini ya Muhimili wowote iwe Utawala/Bunge/Mahakama.
Itabidi ili nalo litazamwe upya..
 
Hapa ndipo nilipokuwa nampenda Magufuli asielewa somo alikuwa asuburi mtakutana mbele ya safari.

Miradi yake ambayo inaelekea kuisha watu ndio wanaanza ielewa leo impact zake kwenye uchumi huko baadae. Na mawaziri wa hizo wizara ambao bado wanamtukana baadhi ya hiyo miradi leo ni wasimamizi wanashangazwa na ukubwa wake.

Ndio kama hili la bandari, watanzania wengi wameonyesha lack of imagination kuona huo uwekezaji unalenga nini kiuchumi; ni mambo ambayo watakuja kuyaelewa mbeleni.
 
Back
Top Bottom