Hili la bei ya mafuta kupanda lina ukakasi

Hili la bei ya mafuta kupanda lina ukakasi

Subira the princess

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2018
Posts
3,474
Reaction score
3,744
Salaam,

Inashangaza bei ya mafuta ya petroli nchini Zambia kuwa nafuu kuliko hapa Tanzania.

Inaeleweka Zambia hawana bandari hivyo wanapokea shehena ya mafuta kutoka Bongo, ifike wakati serikali ya CCM iwe na huruma itende haki.

Hapa anaeumia sio mwenye pesa, ni mnyonge masikini wa hali ya chini.
 
Bado wanafikiria kodi kwa kila anayepata hewa ili apumue kwa uhuru.
 
Tatizo wakuu wetu ni waroho sana. Wanaongeza kodi kwa wanyonge huku wenye kipato cha chini badala ya wao wenyewe kujipunguzia mishahara ili pesa iende kwenye hiyo miradi.

Mshahara wa rais, mawaziri, wabunge na viongozi wengine wa ngazi za juu ni kufuru. Mbali na mishahara hiyo minono bado wanalishwa na kununuliwa mahitaji mengine ya kila siku kwa kodi za wanyonge wenye kipato kidogo kabisa na waliojibana bana na kununua gari kwa ajili ya usafiri maana gari ni hitaji muhimu kwa kila familia.
 
Kwao huo ni mwanzo tu hata mkose nguvu ya kudai katiba mpya kuondosha mapungufu ya ile ya sasa.
 
Salaam

Inashangaza bei ya mafuta ya petroli nchini Zambia kuwa nafuu kuliko hapa Tanzania.

Inaeleweka Zambia hawana bandari hivyo wanapokea shehena ya mafuta kutoka bongo, ifike wakati serikali ya CCM iwe na huruma itende haki.

Hapa anaeumia sio mwenye pesa, ni mnyonge masikini wa hali ya chini.
Mkuu Burundi petrol 1700
 
Hili suala la kodi gumu sana. Ukilinganisha kodi tunazilipa watanzania bado hata hatulipi vizuri. Wengi wetu tunatengeneza pesa na hatulipi kodi aka sekta isiyo rasmi.. Tungekuwa tunalipishwa kodi ipasavyo basi wote tungehama nchi.
 
hivi ile ishu ya bomba la mafita kigamboni imeishia wapi

naona kimya kabisaaaa

hii nchi ni shamba la bibi
 
hivi ile ishu ya bomba la mafita kigamboni imeishia wapi

naona kimya kabisaaaa

hii nchi ni shamba la bibi
Unakula,ukishiba waachie na wengne.Just simple usifanye mamb kuwa magumu sana[emoji848][emoji17]
 
Back
Top Bottom