Hili la Chris Brown huko Kenya ni kweli au kawaida ya majirani zetu kutafuta kiki?!

Hili la Chris Brown huko Kenya ni kweli au kawaida ya majirani zetu kutafuta kiki?!

Mr Hero

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2015
Posts
5,540
Reaction score
7,455
_91631027_ed3f85ee-27e7-44aa-9700-617a494158af.jpg


Muimbaji mashuhuri wa Marekani mtindo wa Hip Hop Chris Brown, yupo Kenya kwa tamasha la muziki mjini Mombasa eneo la pwani.

Lakini tukio ambalo halikunukuliwa kwenye kamera limegubika vyombo vya habari nchini.

Shabiki mmoja mwanamke anatuhumu kuwa Chris Brown ameivunja simu yake alipojaribu kupiga picha 'selfie' alipowasili katika uwanja wa ndege Mombasa.

Kwa mujibu wa gazeti mmoja nchini "Daily Nation,'' mwanamke huyo anasema CB alimpokonya simu kutoka nyuma alipojitayarisha kuipiga picha hiyo na kuirusha chini.

Taarifa hiyo inaongeza kuwa simu ya msichana huyo aina ya iPhone 6 iliyomgharimu takriban dola 900, haikuvunjika lakini kizuia kioo na kifunikio cha simu viliharibiwa.

Shabiki huyo aliyesema amenunua tiketi kuhudhuria tamasha hilo, ameghadhabishwa na ameamua kutohudhuria tamasha hilo.

Tuhuma zake zimesababisha gumzo kuu katika mtandao wa Twitter kupitia [HASHTAG]#DeportChrisBrown[/HASHTAG] ambapo Wakenya wanajadili iwapo muimbaji huyo nyota arudishwe Marekani.

_91631026_175ffed3-d570-4d39-994a-f758240e8a67.jpg


Hisia zimegawanyika ambapo baadhi wanamtetea Chris Brown na wengine wakitaka atimuliwe Kenya.

Kanda ya video iliyowekwa na @KinyanBoy katika twitter inaonekana kumuonyesha Chris Brown akipuuza ombi la mwanamke huyo kupiga selfie na anampita bila kumgusa.

Lakini mwanamke huyo aliyejitambulisha kama Brenda Chepkoech, amezungumza na televisheni ya NTV nchini, anasisitiza kuwa tukio hilo limetokea baada ya kanda hiyo kuwekwa kwenye mtandao na ni muda mfupi kabla ya CB kuingia garini na kuondoka.

Mnamo Julai mwanamuziki mashuhuri wa Congo, Koffi Olomide alirudishwa Congo kutoka Kenya baada ya kuzuka video katika mitandao ya kijamii akionekana kumpiga teke mojawapo ya wachezaji wake densi katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Nairobi.

Wakenya walighadhabishwa katika Twitter na kutaka atimuliwe.

Koffi aliomba radhi lakini tamasha lake lilifutiliwa mbali na alirudishwa Kinshasa kwa ndege.

Siku chache baadaye waandalizi wa tamasha lake jingine Zambia pia walilazimika kufutilia mbali tamasha hilo kutokana na shinikizo kufuatia tukio la Kenya.


NB: mpaka sasa sijaona video inayomuonyesha Brown akifanya hicho kituko,
 
Hilo tukio limetokea kweli na binafsi nimeona clip kupitia CITIZEN TV ktk kipindi cha CITIZEN WEEKEND
" Chris brown selfie storm" kilikuwa headline.
 
Atalazimishaje selfie bila mlengwa kukubali? Huyo mwanamke asitafuke kiki kwa bei nafuu.
 
Serikali ya Mombasa imekanusha. Nmeangalia hiyo habari ktk media house almost zote sijaona chochote. Nilichokiona yule demu alitokea katikati ya walinzi akatoa simu CB akam ignore. Basi kama kuna ukweli kwenye hili basi waandaaji watakuwa wametumia nguvu nyingi kulizuia cz naskia wametumia 300m Ksh kumleta CB.
 
Duuuhhhh kama vp angerudishwa tu...kwa nini ana ignore funs
 
Chris Brown ni mwanamuziki maarufu wa HipHop au RnB?
 
Wakenya bhana kwa sifa. Wanataka kujipa ujiko kwamba wanajua kuitumia twitter vizuri. Ndio maana huko walikutana na wanaigeria palichimbika kwa mitusi.
 
Uongo mtupu.. ukiona ile clip ina suggest something else...
nenda @theshaderoom uone ilivyokua
 
Kwa hiyo chris brown arudishwe kisa alikataa kupiga selfie au kwa sababu amevunja simu?... Tumeshindwa kufukuza wanaotunyonya, tunataka wasepe waliokataa selfie. Noma sana... Ningependa kujua ktk theory of evolution, tumetokea wapi.
 
Americans Wana Habit tofauti na sisi,
huyo mwanamke ashukuru Mungu ni chris brown lakini angekuwa Kanye West hehehhee sasaivi tungekuwa tunajadili jambo jingine kubwa!!
 
Hivi msanii hana legal rights za kuridhia kupiga selfie na mtu? Au anapokuwa maarufu, haki zake hupotea pia?
 
Back
Top Bottom