Naona unazidi kujivuruga mwenyewe na kuonyesha jinsi usivyo kuwa makini. Hii ni kwa sababu uhitimu wako ni wa chuo cha 'google'!Hizo hospitali unazosifia hazina maajabu yoyote, tatizo lako umekariri. Ndio maana wadau wengi humu wanakushangaa. Na muda mrefu nilikwambia kuwa viongozi wenyewe wa India hawaendi hizo hospitali wanaenda kutibiwa nje ya India. Kama mwenyeji anafanya hivyo basi ujue kuna shida
Mtu mwenye uelewa hawezi kudai kama unavyo fanya hapa kuwa "...viongozi wenyewe wa India hawaendi hizo hospitali, wanaenda kutibiwa nje ya India". Sasa nikueleze kuwa mtu mwenye uelewa wa mambo na elimu ya kutosha hawezi kuweka madai kama hayo unayo yafanya wewe hapa, kwa sababu ukiulizwa ulewte ushahidi unao onyesha hivyo; sehemu pekee unayo kimbilia ni 'google' kwenda kupata mfano mmoja au miwili ya viongozi waliofanya hivyo. Na isitoshe, hutajisumbua kutafuta sababu kwa nini walikwenda kutibiwa kwingine badala ya kwenda kwenye hospitali zao huko India!
Kwa mtu mwenye ufinyu wa uelewa, kama unavyo onyesha wewe hapa toka mwanzo, hiyo inatosha kabisa kujigamba kuwa unajuwa unacho kisemea.
Hali kadhalika, tazama hao wenzako unao waita wewe "...wadau wengi humu wanakushangaa"; wengi wangapi, na wamenishangaa kivipi? Huoni nilipo waita "walevi wenzako" kumbe hukuelewa maana niliyo kuwa nimeilenga? Hao hawana tofauti yoyote na wewe katika ufahamu wa maswala haya.
Unarudia yale yale, eti "hospitali ninazo zisifia hazina maajabu yoyote", kwani nilikwambia popote humu tokea tujibishane kuwa hizo hospitali zina "maajabu"? Hizo hospitali kuwa tofauti na zile za "Public Health Service" ndiyo unataka yawe maajabu? Kwa mara nyingine hii inaonyesha ufinyu wa fikra ulizo nazo kuhusu maswala ya namna hii
Unataka maajabu yawe yapi? Kila mgonjwa anaye kwenda kutibiwa humo atoke akiwa mzima? Hayo wewe uli yaona wapi?
Kiujumla naona sina la ziada kujadili na wewe kuhusu hili la hospitali maalum za India wanako kwenda kutibiwa baadhi ya waTanzania, siyo viongozi pekee; najuwa hata waTanzania wengine huenda huko kutibiwa na wengine hupona na baadhi yao hufariki. Hospitali hizo ni tofauti na zile zinazo toa huduma katika mfumo wa kijamii wa Afya unao tumika India.
Sina la zaidi na wewe.