Hili la kulipia kibao cha namba za Makazi Watanzania wenzangu na ninyi ujumbe umewafikia?

Hili la kulipia kibao cha namba za Makazi Watanzania wenzangu na ninyi ujumbe umewafikia?

King Kisali

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2019
Posts
1,041
Reaction score
1,349
Nimetumiwa ujumbe na mtendaji wa kata nifuate kibao cha namba za makazi niende na shilingi 5000 ya kulipia , ilipo nyumba nyingine mtendaji kanitumia meseji niende nikalipie 5500 , hivi, hivi vibao vya namba za anuani ya makazi vinalipiwa tena?

Serikali ya awamu ya sita jamaniiiii mbona hivyo , yaani Waziri atembee juu kwa helikopta ya gharama ya juu halafu sisi tulipie vibao vya namba za anuani ya makazi kweli?

Tena kila kata na gharama yake tofauti ?

Hivi hii Serikali jamani mbona makato kila kona .
 
Acha siasa za kichoko wewe, lengo lako ni kueneza chuki kuhusu zoezi la anwani za makazi
 
Nimetumiwa ujumbe na mtendaji wa kata nifuate kibao cha namba za makazi niende na shilingi 5000 ya kulipia , ilipo nyumba nyingine mtendaji kanitumia meseji niende nikalipia 5500 , hivi, hivi vibao vya namba za anuani ya makazi vinalipiwa tena? . Serikali ya awamu ya sita jamaniiiii mbona hivyo , yaani waziri atembee juu kwa helikopta ya gharamu ya juu halafu sisi tulipia vibao vya namba za anuani ya makazi kweli? Tena kila kata na gharama yake tofauti ? . Hivi hii serikali jamani mbona makato kila kona .
Usiwaze, nunua Cha kwako kiweke hapo. Vitu vingne ni vidogo tu Hasa ukiwa huku mjini. Kibao Cha kwako unataka serikal ikuwekee jombi.
 
Acha siasa za kichoko wewe, lengo lako ni kueneza chuki kuhusu zoezi la anwani za makazi
Hana lengo hilo labda wewe umemuelewa vibaya

Harafu mbona unaandika kwa hasira sana mkuu!?

Yote kwa yote makato mpaka kieleweke
 
Acha siasa za kichoko wewe, lengo lako ni kueneza chuki kuhusu zoezi la anwani za makazi
Mkuu ni kweli,baadhi ya viongozi wa serkali za mitaa wanatumia fursa hi kula kwa urefu wa kamba yao.
Mfano,baadhi ya viongozi hawa wanawalazimisha wakazi kuwa vibao vimetengenezwa na wanatakiwa kulipia pesa hiyo.Hapo elimu ni muhimu ipite kwa wananchi!
 
Na wao wameona wajipigie vielfuelfu
Maana hko juu wenzao wamekura mamilion
Kila mtu anajiongeza kwenye nafasi yake

Ova
 
Back
Top Bottom