Uchaguzi 2020 Hili la kurudia kupiga kura ukikosea na Vitambulisho Mbadala, kwanini uchaguzi huu?

Kama ni hivyo basi wangeruhusu hata ambao hawajajiandikisha kituo husika wapige kura maana kwa hili maana yake kutakua na karatasi nyingi za kutosha,wangeweka kifaa/computer ambayo itamwezesha msimamizi wa uchaguzi kituoni kuaccess data base ya NEC kuhakiki wapiga kura ambao hawakujiandikisha kituo husika.
 

Tume wanasema kila mtu apigie alipojiandikisha maana karatasi zilizoko kwenye vituo vya kura zipo kwa idadi ya wapiga kura tu. Je hizo za watakaokosea zinatoka wapi. Unaoongea utoto wa kushindwa huku mnatumia mbinu za kizee!
 
Nani anaihakiki kwamba hii imekosewa, rudia na hii ni sahihi tumbukiza? kama zinahakikiwa kabla ya kutumbukizwa basi kura sio siri tena, na mtu akishapiga kura anaondoka zake, kuona makosa ya kura zilizopigwa ni wakati wa kuhesabu je, aliyekosea atakuwa wapi wakati huo?
 
CCM wanajua hawashindi kwa hiyo figisu kila kona...ni wakati wa wananchi kusimama na kiwakemea hawa jamaa na NEC yao kwa nguvu zote!!
 
Kwahiyo kwenye kituo kutakua na karatasi za ziada za kufa mtu. Maana assume kila mtu anakosea mara 5.
 
Naomba kufahamu juu ya kupga kura sehemu ambayo sijajiandikshia kwakura ya rais
 
29/10 tutakuwa mlangoni kwa lissu na viboko tukampakie kwenye ndege arudi kwao uzunguni
 
Jamaa wanatafuta Huruma tu
Kushindwa lazima watashindwa tu
 
Wapuuzi sana hao Tume, wanajaribu kutengeneza mazingira kura zipigwe kwa wingi iwezekanavyo, na hapo ndipo wanapoweza kuingiza mambo yao ya goli la mkono wajinga kabisa.

Unaweza vipi kukosea kupigia kura? yani ushindwe kuweka tiki kwa unaempenda kisa unawaza nini?!
 
Watanganyika ! Hila ya Tume ya Uchaguzi kuja na mpango kwa Wapiga kura , kupiga kura zaidi ya mara moja ! Siyo sahihi na ni batili kama siyo zoezi la wizi au ushirikina.

Watanganyika msije mkathubutu kuukubali mpango huu unaletwa na tayari umeshatangazwa ktk vyombo vya habari nchi nzima. Muhimu. kwa vyama vyote vya upinzani na wananchi kupiga na kuukata mpango huu wa Tume kwa nguvu zote Usitumike.
 
Mawakala watafanya kazi hiyo na kuichana ile iliyoharibika. Kumbuka ninadhani karatasi ya kura siyo controlled stationary ni kama karatasi za kutolea na kuweka pesa bank
 
Utatumia vitambulisho mbadala kama cha kupigia kura kimepotea,hilo la kurudia unaweza kufafanua? Maana unaandika kama unaharisha.
 
Mimi nipo Russia,nilipoteza kadi yangu ya kupigia kura na wakati wa uandikishaji/uhakiki mpya sikuwepo Tz.
Kama wangefanya uamuzi huo mapema,ningejitahidi nirudi nije kutumia haki yangu ya kuchagua kiongozi bora,sasa uamuzi unakuja wiki moja kabla ya uchaguzi!
Wenye utimamu wa afya ya akili lazima tujiulize,kulikoni sasa kama zimamoto?
 
Ugonjwa alionao mleta mada ni hatari sana! Kuona uovu katika kila jambo....tatizo la ugonjwa huu haliishii kwenye siasa hata masomo, chakula, jamii unayoishi nayo, nk!
Unajua serikali inasomesha watu wake kwenye nyanja mbalimbali,na ambazo zote lengo lake ni kufanikisha kumfanya Mtanzania awe salama na apate maendeleo. Je,ni kosa kutumia elimu yangu kwa maslahi mapana ya Tanzania na Watanzania wote!?
 
Utatumia vitambulisho mbadala kama cha kupigia kura kimepotea,hilo la kurudia unaweza kufafanua? Maana unaandika kama unaharisha.
Una elimu gani?
Una umri gani?
Yaani maandishi rahisi namna hiyo umeshindwa kuelewa!? Utaweza kuelewa nini sasa wewe!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…