Uchaguzi 2020 Hili la kurudia kupiga kura ukikosea na Vitambulisho Mbadala, kwanini uchaguzi huu?

Uchaguzi 2020 Hili la kurudia kupiga kura ukikosea na Vitambulisho Mbadala, kwanini uchaguzi huu?

Mh Kuna ya kurudia ukikosea kweli.
Kama hiyo ipo haijakaa sawa. Maana hapo zikiharibiwa zilizokosewa. Kuna uhakikia gani hakutakua na njama za kujaribu za mgombea Fulani na kuhesabiwa Kama zilizokosewa.

Au je Kama mtu akipiga Mara mbili au zaidi kwa kisingizio Cha kukosea Kisha kujumlishiwa kwa mchaguzi wake?

Utaratibu wa hizo rejects umekaaje?

Idadi ya Kura iwe moja kwa mmoja. Suluhisho la kukosea liwe elimu ya upigaji kura kabla ya kupiga.

"Kama kweli Kuna hiyo yakurudia" kwa mtu mmoja.

Utarudia kabla hujatumbukiza karatasi husika kwenye box... utamjulisha msimamizi wa kituo kuwa umekosea na karatasi lazima awaoneshe mawakala kuwa umeharibu kwa bahati mbaya na itahesabika imeharibika na utapewa karatasi nyingine la kupigia kura!

NB hii ni kabla hujatumbukiza karatasi kwenye box kama ukigunduavumekosea
 
Kura ni ile iliyopigwa na kudumbukizwa kwenye sanduku la kura baada ya hapo hakuna kiachoweza kusahihishwa wala kurudiwa.

nadhani tume imetoa nafasi kwa mpiga kura akigundua amekosea aombe karatasi nyingine ili aanze upya- cha kuangalia ni mawakala kuhakikisha hiyo karatasi inachanwa basi. MKUU USIWE MUUGA WA KUSHINDWA MAANA MTASHINDWA TU
He hee heeee....
 
Na je kama mambo yashaongezeka hvo je watu wataruhusiwa kupiga kura sehmu yoyote?
 
Kwamba idadi ya karatasi vituoni inapelekwa kulingana na idadi ya waliojiandikisha.

Mkuu hili hapana siyo kweli ni uongo na uzushi
Hoja hiyo ilijibiwa baada ya kuhoji kwanini Rais asipigiwe kura sehemu yoyote mtu anapokuwepo maadam ana vigezo vyote vya mpiga kura.
 
Tume imeruhusu vitu viwili vya ajabu.
Mosi ni kuruhusu watu kutumia vitambulisho mbadala (Pasi ya kusafiria na leseni ya udereva).
Pili ni kuruhusu mpiga kura kurudia kupiga tena kura iwapo alikosea.
Je,huu sio mwanya wa "ushindi wa kishindo"!?

Hii ya kuruhusu vitambulisho mbadala nakubaliana nalo,lakini kwa nini huu uamuzi uje wakati huu?
Hili la kurudia kupiga kura,hapana kwa kweli.
Kukosea kupi kunaruhusiwa kurudia?
Kwa hili Tume inafanya kosa la jinai. Kwa wasimamizi dhaifu wasioweza kudhibiti wapiga kura, hiki ni chanzo cha kupigwa kura zaidi ya mara moja. ni chanzo cha mtu kutumbukiza kura na kurudi kushinikiza apewe nyingine sababu ya kwanza amekosea. Ni wakati wa watu kupiga kura, kufuta wino na baadaye kurudi na NIC kwa kisingizio kapoteza kadi kati ya kupigia kura. Lazima watoe muongozo wa kina kwa hili.
 
Kama mshindi wanaye tayari watwambie tu ili tusipoteze muda wetu, tuhangaike na foleni wakati mshindi wao yupo mfukoni wanatembea naye .
 
Kwa maana hyo kutakua na karatas za ziada kwaajili ya marekebisho kwa waliokosea/kubadili mawazo,kwann wasituruhusu tupige kura kituo chochote kwa sisi tuliohama makazi...maana kila kituo kitakua na karatas za ziada tuzitumie izo izo
 
Back
Top Bottom