Hili la Luaga Mpina ni pt2 ya Vita ya Musiba na Membe. Nani yuko nyuma ya pazia?

Hili la Luaga Mpina ni pt2 ya Vita ya Musiba na Membe. Nani yuko nyuma ya pazia?

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2017
Posts
458
Reaction score
1,280
Wakuu kumekua na sintofahamu nyingi juu ya sakata la madai ya wanakijiji kudai kutapeliwa ardhi yao na muwekezaji Mbunge wa kisesa Luaga Mpina kuhusu ardhi yenye Ukubwa wa ekari 1000.

Mengi yanazungumzwa na mwisho lililoongeza mjadala ni kuwa Waziri wa Fedha Dr Mwigulu Nchemba ndiye Yuko nyuma ya pazia juu ya sakata zima la sekeseke hilo kwani Mpina amekua akiibua hoja nyingi dhidi ya Wizara ya Fedha BUNGENI hivyo anatafuta njia ya kumnyamazisha wengine wakienda mbali kwa kusema kuwa Mkuu wa Wilaya anatumika pasipo kujua juu ya sakata hilo.

Wanazengo wanatahadharisha kuwa isije ikawa Kama Yale ya Membe na Musiba bora suala hilo kumalizwa kwa uweledi mkubwa kwa Mustakabali mpana wa Watanzania na Tanzania kwa ujumla.Tahadhari hii I akuja baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kutoa kauli ifuatayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji Cha dalla 29.5.2023 nanukuu

"Namuagiza Luhaga Mpina huko aliko kama yeye amesema hiki ni kikao cha harusi basi MWALI atakuwa yeye MPINA"

Akizungumza na wananchi hao mara baada ya kupokelewa kwa mabango yanayoshinikiza kumkataa mwekezaji huyo LUAGA MPINA wananchi hao wamelalamika kukosa ardhi ya kilimo kwakuwa asilimia kubwa wamekuwa wakitegemea kilimo kuendesha maisha yao ya kila siku.

Aidha wameiomba serikali kupima ardhi yote inayoshikiliwa na mwekezaji huyo pamoja na mipaka ili kujua ukubwa halisi wa ardhi anayoikalia kwa njia za udanganyifu tangu mwaka 2009.

Kufuatia malalamiko hayo,mkuu wa wilaya ya Morogoro REBECA NSEMA amelazimika kuunda timu ya wataalamu watakaofanya kazi ya kupima eneo lote linalokaliwa na mwekezaji huyo ndani ya siku kumi na nne ili kuweza kutoa haki kwa pande zote mbili.

Aidha mkuu huyo wa wilaya ametaka mwekezaji Luaga Mpina kutoa ushirikiano kwa timu hiyo na kuwasilisha nyaraka zote zinazompa uhalali wa kumiliki aradhi hiyo inayolalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu.
 
Back
Top Bottom