Hili la Makonda kuwataja hadharani anaowatuhumu kumtukana raisi mtandaoni, linaweza kumletea matatizo makubwa ya kisheria

Hili la Makonda kuwataja hadharani anaowatuhumu kumtukana raisi mtandaoni, linaweza kumletea matatizo makubwa ya kisheria

Kwa nini atumwe? Kwani hao jamaa hawawezi kuchukuliwa hatua za kinidhamu au za kisheria bila kwanza kutajwa hadharani? Huo ni utaratibu wa nchi gani duniani?
Lugha rahisi tunaweza kusema ni propaganda za kisiasa .
 
Katika hafla ya kumbukizi ya siku ya kifo cha Sokoine leo, Makonda amesema tarehe 15 April atawataja hadharani anaowatuhumu kufadhili wanaomtukana rais mtandaoni. Kwamba anawajua na baadhi yao ni mawaziri.

Hili inaweza kumletea matatizo makubwa ya kisheria. Linaweza hata kupelekea kuwekwa tena benchi.

Alishawahi kufanya hivyo huko Dar es Salaam akiwa mkuu wa mkoa huo alipowataja hadharani watuhumiwa vigogo wa madawa ya kulevya. Madhara yake tuliyaona.

Kwa mtindo wa aina hiyo, tulishuhudia Musiba kuhukumiwa kumlipa waziri mstaafu Membe mabilioni ya pesa. Ni vizuri Makonda akashauriwa kuyapeleka hayo majina kwa vyombo husika badala ya kuyatoa hadharani.
Alipotaja wauza ngada nlwalikaa kimya sembuse hii ya kutukana. Ngoja wataachia simu zao siku sio nyingi kumpa legitimacy Makonda.
 
Naamini Samia kamtuma Makonda aseme vile
Sidhani kama ni hivyo,hao mawaziri ni Rais mwenyewe ndiye kawateua na kuwaapisha kama ana taarifa kuwa wanawalipa watu wanaomtukana anashindwaje kuwawajibisha hadi amtume Makonda kuwatisha? Ina maana Samia anawaogopa watu aliowateua mwenyewe? Na kama ni hivyo basi hatuna Rais.
 
Kwa nini atumwe? Kwani hao jamaa hawawezi kuchukuliwa hatua za kinidhamu au za kisheria bila kwanza kutajwa hadharani? Huo ni utaratibu wa nchi gani duniani?
Tanzania, Bongo Land. Ndio utajua hii ni nchi ya kipekee, iliyobarikiwa. Nchi ya ahadi.
 
Sidhani kama ni hivyo,hao mawaziri ni Rais mwenyewe ndiye kawateua na kuwaapisha kama ana taarifa kuwa wanawalipa watu wanaomtukana anashindwaje kuwawajibisha hadi amtume Makonda kuwatisha? Ina maana Samia anawaogopa watu aliowateua mwenyewe? Na kama ni hivyo basi hatuna Rais.
Mbinu tofauti za kiuongozi. Kila kiongozi ana mbinu zake.
j. Nyerere alikuwa anakufungia kizuizini kijijini kwako mpaka utubu. Mwinyi alilivunja baraza zima la mawaziri. Mkapa aliwapa miradi wale zaidi, mkizidi mnapigwa mabomu mpaka mnatafuta ukimbizi. Kikwete anakuita Ikulumnagonga kahawa, usipomuelewa magazeti yatakushughulikia mpaka mwenyewe ujiuzuru. Magufuli ukimzengua alikuwa anakupoteza kabisa/wasiojulikana wanakushughulikia. Mama ni mama anakulea na kukubembeleza bembeleza, kukulea. Kama bado humuelewi anakutumbua.

Chagua mwenyewe mbinu unayaoiona sahihi. Ila Hakuna 100% sahihi.
 
Hizi tabia za kusema nitawataja wanaokusema ni tabia za akina Hadija na na Mariam tena wale wa tandale!
Mwanaume mwenye akili timamu huwezi kuongea ujinga wa kiasi kile tena hadharani! Shame!
 
Back
Top Bottom