Hili la Muharami Viongozi waSimba mpo sahihi

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Naona baadhi ya Watu ni kama wanalazimishwa kusikiliza au kuimbishwa mapambio yanayohanikiza kwamba Simba haikufanya sahihi kujiweka mbali na hili suala lililomkuta Bw Muharami. Na hata ukiwauliza ni kwa upande upi haswa wao wanaona Simba imekosea hawana hoja ya msingi zaidi ya kung'ang'ania tu kwamba si uungwana kumtenga Mtu wakati wa matatizo. Wanachosahau ni kuwa Simba ni Kampuni ya Watu na sio Mtu. Simba sio Baba, Mama au Mjomba wa Muharami au May day. Simba ni ya kina Shemdoe, Mkude, Mgonyani, Ngeleja, Masawe n.k.

Kwanza sijui kwa nini wao wanakimbilia kuona kuwa ametengwa, wakumbuke ya kuwa kuna suala la undugu, urafiki na kuna suala la kazi au Ofisi....kama urafiki wetu unatokana na kazi, yaani ni kazi ndio ilitangulia, ni vipi tena basi ionekane urafiki huo ndio muhimu kuliko kazi hiyo?.k Kwamba kama inabidi kuiangamiza kampuni/kazi basi ni bora kuliko urafiki wetu kufa?. Kwamba baada ya Simba kujitenga na tuhuma zinazomuhusu Muharami basi ndio wamemaliza yote, hivyo kama ana Marafiki na Jamaa ndani ya Simba nao wamezuiwa kuhusiana naye?.

Kuna mmoja naye huko nikamsikia anatolea mfano wa lile sakata la Yusuph Manji, sioni hata mfanao wa haya matukio mawili...maana ingekuwa tofauti kama suala lingemuhusu Mo..

Pili tuangalie aina ya tatizo lililojitokeza hapa, nadhani isingekuwa shida sana kama ingekuwa ni jambo la kawaida tu....ni msio na akili tu ndio mnalazimisha kudhani ya kuwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya ni jambo dogo tu na la kawaida, labda ipo hivyo mtaani lakini sio linapofika kwenye Mamlaka huko.

Na tatu ni je, hicho kilichosemwa na Simba kwamba walimchukua kwa muda na hakuwa Muajiriwa sio sahihi? kama ndivyo sasa hii sintofahamu inatokea wapi au mlitamani isisemwe?.

Kuna wakati hapa Ndugu zetu hawa (ambao kwa sehemu kubwa ndio waimbaji wa wimbo huu) walipatwa na kadhia ile maarufu ya "mama J", kwa vyovyote ishu kama ile pamoja na ukakasi wake lakini halikuwa suala linaloihusu Kampuni/ofisi, lile lilibaki ni suala la kishabiki tu....sasa ni ajabu sana namna mabavyo Watu wangetamani na hili la sasa litazamwe kwa mlengo kama huo na kuchukuliwa poa.

Nimeona kwenye ukurasa wa "Bwana yule" anayetumikia adhabu kwa kuwa huongea kila anachojisikia, sasa ameshaanza kuinasibisha Timu na masula ya madawa, sasa je hapa tujiulize anaikebehi Simba Timu au anamkebehi Muaharami anayetuhumiwa? kama ni suala la uungwana kwa nini nao wasifanye huo uungwana wa kusubiri mpaka atakapothibitishwa na kuhukumiwa?.

Na kama ni suala la uungwana basi nadhani ni yeye Muharami ndiye angepaswa kujitokeza mapema(kama angepata hiyo nafasi) kuhakikisha kuwa hiki kilichomkuta kamwe kisiisumbue Timu...Ushujaa wa kweli ni pale unapoona kwamba tatizo lako wewe halimsumbui mwingine...ila kama naye atakaa chini na kulia kuwa Simba imemtenga basi wala hakufaa kuwa sehemu ya Timu.

Naunga mkono hatua ya Viongozi kuandika barua ya kujiweka mbali na hili na Timu ishughulike na majukumu yake mama ya kushinda kila mechi...na kama ingebidi basi nao hiyo Tume ya Dawa za kulevya wangeomba Club ya Simba radhi kwa kusema jambo bila kwanza kujiridhisha...hivi kama wakimkamata Mtu akasema kuwa anafanya kazi Ikulu watatoka tu mbele na kutangaza bila kujiridhisha?..au ni kuleta siasa tu kwenye kila jambo bila kujali wataharibu shughuli za wengine?.
 
Hizi mbamba ni za kipuuzi tu!!.

1.Simba haikuwa ma kocha wa makipa?
2.Mtumishi wa taasisi lazima ahusishwe na taasisi husika na kama suala ni lake binfsi uchunguzi utaamua Ila inajulikana ni mfanya kazi wa simba. Je kama alichokuwa anafanya ni sehemu ya kazi na majukumu yake katika taasisi husika?. Simba lazima wasaidie kutoa majibu toshelezi.
3.kitendo cha kumkana mtu ambaye kafanya na alikuwa bado anatambulika Kama mfanya kazi wa simba ni udhaifu na Kuonesha kwa namna fulani taasisi hiyo unahusika na Hilo saga.
4.kwahiyo ukiwa na mfanyakazi wa muda katika taasisi yako hatambuliki kama ni mfanya kazi?.
 
Mleta bandiko usifikiri mbumbumbu fc wenzako wanao jitambua kukaa kimya kwamba hawataki kuitetea klabu.
Wameona klabu imekosea ku shughulikia Ili jambo, Bosi wa madawa ya kulevya hakuzipata taarifa hewani na kazi ya kumkamata haikufanywa na taasisi Moja, maelezo aliyo yatoa boss ameyapata kutoka Kwa mtuhumiwa ndugu kocha wa Makipa.
Upo ushahidi usio na shaka wa kimazingira na uhalisia unao onyesha mwalami ni mwajiliwa wa Simba. Iwe mwajiliwa wa muda au wakudumu.
Simba hawakutakiwa kumkana Mwalami, walichotakiwa kutounga mkono tuhuma za vitendo alivyo fanya kwakua havihusiani na klabu.
Walitakiwa kumsimamisha mpaka ufumbuzi wa kisheria utakapo patikana na ikiwa itathibitishwa mahakamani basi watatoa taarifa nyingine kutokana na maamuzi ya mahakama.
Kitendo Cha wao Simba ku mkana Mwalami ndio kinaongeza wasiwasi wa namna uongozi unavyo shughulikia mambo.
Mwalami sikuzote anaonekana akiwa na Simba Sasa Leo ku salitiwa kwake kume shangaza wanamichezo wengi wanao fahamu mausiano yake na klabu.
 
Naona baadhi ya Watu ni kama wanalazimishwa kusikiliza au kuimbishwa mapambio yanayohanikiza kwamba Simba haikufanya sahihi kujiweka mbali na hili suala lililomkuta Bw Muharami. Na hata ukiwauliza ni kwa upande upi haswa wao wanaona Simba imekosea hawana hoja ya msingi zaidi ya kung'ang'ania tu kwamba si ungwana kumtenga Mtu wakati wa matatizo. Wanachosahau ni kuwa Simba ni Kampuni ya Watu na sio Mtu. Simba sio Baba, Mama au Mjomba wa Muharami au May day, Simba ni ya kina Shemdoe, Mkude, Mgonyani, Ngeleja, Masawe n.k.

Kwanza sijui kwa nini wao wanakimbilia kuona kuwa ametengwa, wanachosahau ni kwamba kuna suala la undugu, urafiki na suala la kazi au Ofisi....kama urafiki wetu unatokana na kazi (kwamba kazi ilitangulia) ni vipi tena basi ionekane urafiki huo ni muhimu kuliko kazi hiyo hiyo?, kwamba kama inabidi kuiangamiza kampuni/kazi basi ni bora kuliko urafiki wetu ufe?. Kwamba baada ya Simba kujitenga na tuhuma zinazomuhusu Muharami ndio wamemaliza yote, hivyo kama ana Marafiki na Jamaa ndani ya Simba ndio wanaachana naye?.

Kuna mmoja naye huko nikamsikia anatolea mfano wa lile sakata la Yusuph Manji, sioni hata mfanao wa haya matukio mawili...maana ingekuwa tofauti kama suala lingemuhusu Mo..

Pili, pia tuangalie aina ya tatizo lililojitokeza hapa, nadhani isingekuwa shida sana kama ingekuwa ni jambo la kawaida tu....ni msio na akili tu ndio mnalazimisha kudhani ya kuwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya ni jambo dogo na la kawaida, labda ipo hivyo mtaani lakini sio linapofika kwa hao wahusika huko.

Na tatu ni je, hicho kilichosemwa na Simba kwamba walimchukua kwa muda na hakuwa Muajiriwa sio sahihi?...kama ndivyo sasa hii sintofahamu inatokea wapi au mlitamani isisemwe?.

Kuna wakati hapa Ndugu zetu hawa (ambao kwa sehemu kubwa ndio waimbaji wa wimbo huu) walipatwa na kadhia ile maarufu ya "mama J", kwa vyovyote ishu kama ile pamoja na ukakasi wake lakini halikuwa suala linaloihusu Kampuni/ofisi, lile lilibaki ni suala la kishabiki tu....sasa ni ajabu sana namna mabavyo Watu wangetamani na hili la sasa litazamwe kwa mlengo kama huo na kuchukuliwa poa.

Nimeona kwenye ukurasa wa "Bwana yule" anayetumikia adhabu kwa kuwa huongea kila anachojisikia, sasa ameshaanza kuinasibisha Timu na masula ya madawa, sasa je hapa tujiulize anaikebehi Simba Timu au anamkebehi Muaharami anayetuhumiwa?..kama ni uungwana kwa nini nao wasifanye huo uungwana na kusubiri mpaka atakapothibitishwa na kuhukumiwa?.

Na kama ni suala la uungwana basi nadhani ni yeye Muharami ndiye angepaswa kujitokeza mapema(kama angepata hiyo nafasi) kuhakikisha kuwa hiki kilichomkuta kamwe kisiisumbue Timu...Ushujaa wa kweli ni pale unapoona kwamba tatizo lako wewe halimsumbui mwingine...ila kama naye atakaa chini na kulia kuwa Simba imemtenga basi wala hakufaa kuwa sehemu ya Timu.

Naunga mkono hatua ya Viongozi kuandika barua ya kujiweka mbali na hili na Timu ishughulike na majukumu yake mama ya kushinda kila mechi...na kama ingebidi basi nao hiyo Tume ya Dawa za kulevya wangeomba Club ya Simba msamaha kwa kusema jambo bila kwanza kujiridhisha...hivi kama wakimkamata Mtu akasema kuwa anafanya kazi Ikulu watatoka tu mbele na kutangaza bila kujiridhisha?..au ni kuleta siasa tu kwenye kila jambo bila kujali wataharibu shughuli za wengine?.
KARMA.
Kabwili, mama J.
SeMBe Gufu moya. Onjeni ladha ya kugeneralize kila baya linalofanywa na mtu wa upande msioupenda.
 
Hao wengine walio kamatwa kwa makosa mbalimbali hawana taasisi? Ni wadhururaji? Wakulima? Vibaka? Wapigadebe?
 
Kauli taasisi ya Rushwa iliyowataja na taasisi zao za kazi.

Au nikuletee nganda 🤣
 
Walitakiwa wakubali kuwa MWAMBA ni mfanyakazi wao, ila alilolifanya siyo la Simba..!! Sasa wao wamemkana na kwenye ajira..!! Kumkana kwenye ajira na hapohapo unarudi kusema ilikuwa ajira ya mwezi tu, ni ujinga. Tena ujinga unaoweza kufanywa na MAMBUMBUMBU na WAUZA NGADA tu..!!
 
KARMA.
Kabwili, mama J.
SeMBe Gufu moya. Onjeni ladha ya kugeneralize kila baya linalofanywa na mtu wa upande msioupenda.
1668598562888.png

Sema nayo hii we mwana NGADA FC
 
Hizi mbamba ni za kipuuzi tu!!.

1.Simba haikuwa ma kocha wa makipa?
2.Mtumishi wa taasisi lazima ahusishwe na taasisi husika na kama suala ni lake binfsi uchunguzi utaamua Ila inajulikana ni mfanya kazi wa simba. Je kama alichokuwa anafanya ni sehemu ya kazi na majukumu yake katika taasisi husika?. Simba lazima wasaidie kutoa majibu toshelezi.
3.kitendo cha kumkana mtu ambaye kafanya na alikuwa bado anatambulika Kama mfanya kazi wa simba ni udhaifu na Kuonesha kwa namna fulani taasisi hiyo unahusika na Hilo saga.
4.kwahiyo ukiwa na mfanyakazi wa muda katika taasisi yako hatambuliki kama ni mfanya kazi?.
Ndiyo maana mimi naihusidha Yanga na ushoga kwa ishu ya Ramadhan Kabwili aliyekiri kuwa ni kweli anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja na alikiri pia kuwa aliwaacha wenzake saba hapo Yanga wanaofanya uchafu huu. Ukichanganya na picha hizi huwezi kuitenga Yanga na ushoga.
JamiiForums-1290500738.jpg
JamiiForums-1379199085.jpg
 
Ndiyo maana mimi naihusidha Yanga na ushoga kwa ishu ya Ramadhan Kabwili aliyekiri kuwa ni kweli anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja na alikiri pia kuwa aliwaacha wenzake saba hapo Yanga wanaofanya uchafu huu. Ukichanganya na picha hizi huwezi kuitenga Yanga na ushoga.View attachment 2418552View attachment 2418553
FB_IMG_16685882695832169.jpg

😅😅😅😅😅 Hawa Wala ngada wenzako walikuwa wanafamyaje.
 
Mleta bandiko usifikiri mbumbumbu fc wenzako wanao jitambua kukaa kimya kwamba hawataki kuitetea klabu.
Wameona klabu imekosea ku shughulikia Ili jambo, Bosi wa madawa ya kulevya hakuzipata taarifa hewani na kazi ya kumkamata haikufanywa na taasisi Moja, maelezo aliyo yatoa boss ameyapata kutoka Kwa mtuhumiwa ndugu kocha wa Makipa.
Upo ushahidi usio na shaka wa kimazingira na uhalisia unao onyesha mwalami ni mwajiliwa wa Simba. Iwe mwajiliwa wa muda au wakudumu.
Simba hawakutakiwa kumkana Mwalami, walichotakiwa kutounga mkono tuhuma za vitendo alivyo fanya kwakua havihusiani na klabu.
Walitakiwa kumsimamisha mpaka ufumbuzi wa kisheria utakapo patikana na ikiwa itathibitishwa mahakamani basi watatoa taarifa nyingine kutokana na maamuzi ya mahakama.
Kitendo Cha wao Simba ku mkana Mwalami ndio kinaongeza wasiwasi wa namna uongozi unavyo shughulikia mambo.
Mwalami sikuzote anaonekana akiwa na Simba Sasa Leo ku salitiwa kwake kume shangaza wanamichezo wengi wanao fahamu mausiano yake na klabu.
Kinachomkuta kitahusika na Wanasimba na si Klabu ya Simba. Klabu haihusiki. alafu ni Muharami sio Mwalami.
 
Back
Top Bottom