May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Naona baadhi ya Watu ni kama wanalazimishwa kusikiliza au kuimbishwa mapambio yanayohanikiza kwamba Simba haikufanya sahihi kujiweka mbali na hili suala lililomkuta Bw Muharami. Na hata ukiwauliza ni kwa upande upi haswa wao wanaona Simba imekosea hawana hoja ya msingi zaidi ya kung'ang'ania tu kwamba si uungwana kumtenga Mtu wakati wa matatizo. Wanachosahau ni kuwa Simba ni Kampuni ya Watu na sio Mtu. Simba sio Baba, Mama au Mjomba wa Muharami au May day. Simba ni ya kina Shemdoe, Mkude, Mgonyani, Ngeleja, Masawe n.k.
Kwanza sijui kwa nini wao wanakimbilia kuona kuwa ametengwa, wakumbuke ya kuwa kuna suala la undugu, urafiki na kuna suala la kazi au Ofisi....kama urafiki wetu unatokana na kazi, yaani ni kazi ndio ilitangulia, ni vipi tena basi ionekane urafiki huo ndio muhimu kuliko kazi hiyo?.k Kwamba kama inabidi kuiangamiza kampuni/kazi basi ni bora kuliko urafiki wetu kufa?. Kwamba baada ya Simba kujitenga na tuhuma zinazomuhusu Muharami basi ndio wamemaliza yote, hivyo kama ana Marafiki na Jamaa ndani ya Simba nao wamezuiwa kuhusiana naye?.
Kuna mmoja naye huko nikamsikia anatolea mfano wa lile sakata la Yusuph Manji, sioni hata mfanao wa haya matukio mawili...maana ingekuwa tofauti kama suala lingemuhusu Mo..
Pili tuangalie aina ya tatizo lililojitokeza hapa, nadhani isingekuwa shida sana kama ingekuwa ni jambo la kawaida tu....ni msio na akili tu ndio mnalazimisha kudhani ya kuwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya ni jambo dogo tu na la kawaida, labda ipo hivyo mtaani lakini sio linapofika kwenye Mamlaka huko.
Na tatu ni je, hicho kilichosemwa na Simba kwamba walimchukua kwa muda na hakuwa Muajiriwa sio sahihi? kama ndivyo sasa hii sintofahamu inatokea wapi au mlitamani isisemwe?.
Kuna wakati hapa Ndugu zetu hawa (ambao kwa sehemu kubwa ndio waimbaji wa wimbo huu) walipatwa na kadhia ile maarufu ya "mama J", kwa vyovyote ishu kama ile pamoja na ukakasi wake lakini halikuwa suala linaloihusu Kampuni/ofisi, lile lilibaki ni suala la kishabiki tu....sasa ni ajabu sana namna mabavyo Watu wangetamani na hili la sasa litazamwe kwa mlengo kama huo na kuchukuliwa poa.
Nimeona kwenye ukurasa wa "Bwana yule" anayetumikia adhabu kwa kuwa huongea kila anachojisikia, sasa ameshaanza kuinasibisha Timu na masula ya madawa, sasa je hapa tujiulize anaikebehi Simba Timu au anamkebehi Muaharami anayetuhumiwa? kama ni suala la uungwana kwa nini nao wasifanye huo uungwana wa kusubiri mpaka atakapothibitishwa na kuhukumiwa?.
Na kama ni suala la uungwana basi nadhani ni yeye Muharami ndiye angepaswa kujitokeza mapema(kama angepata hiyo nafasi) kuhakikisha kuwa hiki kilichomkuta kamwe kisiisumbue Timu...Ushujaa wa kweli ni pale unapoona kwamba tatizo lako wewe halimsumbui mwingine...ila kama naye atakaa chini na kulia kuwa Simba imemtenga basi wala hakufaa kuwa sehemu ya Timu.
Naunga mkono hatua ya Viongozi kuandika barua ya kujiweka mbali na hili na Timu ishughulike na majukumu yake mama ya kushinda kila mechi...na kama ingebidi basi nao hiyo Tume ya Dawa za kulevya wangeomba Club ya Simba radhi kwa kusema jambo bila kwanza kujiridhisha...hivi kama wakimkamata Mtu akasema kuwa anafanya kazi Ikulu watatoka tu mbele na kutangaza bila kujiridhisha?..au ni kuleta siasa tu kwenye kila jambo bila kujali wataharibu shughuli za wengine?.