Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

Hapo hapo jambazi anakimbia njiani polisi wanakutana na ndugu yako wanamfananisha na jambazi waliyemuona bila kuhoji wana mshuuti au sio
 
Inahitaji ujasiri uliopitiliza kiwango kutetea mambo ambayo yanaliingiza gizani taifa. Unaona sasa hapa unajaribu kupotosha hata ukweli ambao mheshimiwa rais amezungumza kuhusu mikutano ya siasa, na sijui unafanya haya kwa maslahi ya nani. Hivi ulisikia alizungumza nini kuhusu polisi na mikutano ya siasa jana? Eti wenye IQ ndogo hawawezi kumwelewa, kwa hiyo rais anaongea na watu asioelewa uwezo wao wa kuelewa, siyo? Unamaanisha rais ameshushwa kutoka sayari tofauti kabisa na kupewa aongoze watu asiowaelewa? Hivi kwanini mmechagua kutomsaidia rais, au mmetumwa kumpotosha ili ashindwe mapema?
 
Kwa uelewa wako mdogo unafikiri kazi ya rais ni kutunga mashairi? Rais hapaswi kutumia metaphor! Kwa hiyo Mbowe, Msigwa,... wanauwezo mdogo wakufikiri ila polisi wanauwezo mkubwa wa kufikiri? kila mtanzania anajifanya anajua! Hii ni element za umasikini hasa wa kichwani! Watanzania shidaaaaaaaa!!
 




Inaonesha tayari umeshamuongeza "mkuu wa kaya" kwenye Ritania za watakatifu kwamba sasa kwenye sala zako unatamka "Mtakatifu Baba J utuombee"........,Ni jambo la kizalendo kuwa na imani kwa kiongozi wako,lakini ni uzalendo uliotukuka kwa mtu kuhoji na kutaka kufahamu mustakabali wa Taifa lake.

Kumlinganisha mwanadamu mwenye " mizuka ya ajabu"na Mitume na Manabii wa Mungu yaweza kuwa dhambi isiyosameheka mbele za Mungu wetu aliye hai.Pole sana.
 
Ukiwa na IQ ndogo huwezi kumwelewa anachosema Mr President ila wenye IQ pana wanamuelewa vizuri nia yake. Kumbuka IQ huwezi kupata darasani ni kipaji anachoumbwa nacho mwanafamu ni zawadi kutoka kwa Mungu. IQ siyo degree au diploma au cheti
 
Pamoja na kwamba unaonekana Unajua Sana sheria lkn brother kuna mengine umeongeza kutokana na tafsiri zako tu. Rais ameongea kwa umakini mkubwa, majambazi wanyang'anywe silaha kabla hawajazitumia. Hata ikatokea Siku kuna kundi la watu watakaotafsiri kama wewe wakataka kumpeleka boss The Hague atashinda, hajasema polisi waue, wewe ndio umeandika kwamba amemaanisha hivo kitu ambacho not necessarily kwamba uko correct. Kwahiyo brother Acha kupotosha watu.
 

Reasonable force inaeleweka tu, wala usiogope kama umebeba silaha haina risasi na umevamia mali za watu subiri tu uone reasonable dhidi ako. Hakuna siasa apa viacheni vyombo vya ulinzi na usalama vifanye kazo zao
 
Tafsiri ya Pasco ni sahihi na Msemaji hakutumia metaphoric language. Metaphor ni kulinganisha mtu au kitu au jambo na kitu kingine bila kutumia neno la kulinganishia. mfano rais ni Simba. au Pasco ni Jembe. neno lingingine ni "simile" hutamkwa "similii" ambapo hulinganishwa kwa kutumia kilinganishi "kama" mfano rais ana nguvu kama simba.
Tamko la rais is so direct na wala IQ unayosema siui ni ipi!
 
Kwani sifa ya kuwa na uwezo mkubwa mpk uongoze watu wangapi? Au wewe ni moja wao waliyoambiwa wannyang'anywe silaha?
 
Ukiwa na IQ ndogo huwezi kumwelewa anachosema Mr President ila wenye IQ pana wanamuelewa vizuri nia yake. Kumbuka IQ huwezi kupata darasani ni kipaji anachoumbwa nacho mwanafamu ni zawadi kutoka kwa Mungu. IQ siyo degree au diploma au cheti
Swali langu ni kwamba: rais anazungumza na hadhira asiyoielewa? Kwanini mnaanza kumdhalilisha rais kwa kiwango hiki; nani anawatuma?
 
KATIKA YOTE TUSIBIRI KWANZA MZIGO HUO UANZE NDUGU ZANGU TUKIPATA MAJIBU YA HILO KUWA LINA FAIDA AU HASARA TUTAHAILISHA KAMA VILE ULE MZIGO WA MSOSI MUHIMBILI SIMPLE TU.SERIKALI NI SIKIVU SANA NAAMINI HIVYO NA INAJALI WANANCHI WAKE.PIA MSIMLAUMU SANA MTOA MADA...AMETOA HISIA NA MAWAZO YAKE KAMA VILE MKUU WA KAYA ALIVYOSEMA KWA HISIA.ILA SASA"UKIONA MAJAMBAZI WAMEVAMIA SEHEMU,UKAAMBIWA LALA CHINI..LALA HARAKA SAANA NA USIJE JISHAURI WALA KUJIFANYA MASTER"HIKI NI KIPIMO KIKUBWA SANA,TUTAJUA KUWA USAHIHI UPO WAPI PINDI TU MATUKIO YAKIANZA.NAMALIZIA PIA UKISIKIA TENA KUNA MAJIBIZANO YA RISASI BAINA NA NDUGU HAO NA ASKARI WETU PIA JIFUNGIE HARAKA SANA.SIOMBI NACHOWAZA KITOKEE ILA KILA KINACHOBANWA SAANA SANA KINA NAFASI PIA YA KUJIACHIA."KILA KITU NI SAWA TU"
 



Mkubwa kujaribu kupambana kihoja na watu waliowekewa mpaka wa ukomo wa fikra zao(rejea tamko toka kwa viongozi wa ngazi za juu wa chama na serikali ya ccm kwa wabunge wa ccm watakaopinga hoja za serikali bungeni)ni kujipotezea muda,hawa watu wameshafungiwa ndani ya box,hawawezi kuwa na fikra huru tena.Ni watu wa kupuuzwa tu kama Mh.Jussa Radhu anavyoendelea kumpuuza Mpanju.
 
Hizo hela za kufanyia maandamano ,nawashauri chagadema wajenge ofisi yenye hadhi ya chama kikuu cha upinzani nchini.

Hii tabia ya kuandamanisha watoto wa wenzenu na kuwashindisha juani ikome Mara moja. @ Nyumbu




Shangata ubongo wako uko sawasawa kweli? Mbona unaleta mada tofauti na iliyomezani? Unatumia ubongo kufikiri au umejaa uji kichwani?
 




Ndiyo maana ukaitwa jingalao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…