Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

Mayalla na ubaguzi wa kikanda,unamtetea magufuli kwa lipi?yeye ndiye aliyeruhusu hao wateule wake kuwa hivyo na hata wakitoa matamko ya kuhatarisha amani ulishaona anawakemea au kuwafanya lolote???sasa unawezaje kutofautisha hizo kauli mbili??kiujumla magufuli hana uchungu na tanzania na target yake kubwa ni kuifanya tanzania ichafuke na analitekeleza vzr kupitia kwa mshauri wake mkuu kagame.
Magufuli si msukuma mayalla simamia ukweli.
 
Mtu kabisa na utashi wake anakaa upande wa jambazi....!!!
Nilikuwa najiuliza hata wakati YESU anataka kusulubiwa watu walikuwa radhi afunguliwe jambazi BARABA lakini YESU asulubiwe, hii mentality mbaya sana!
Kumbe ndo maana huwa tunasikia kuna vigogo wanamiliki na kufadhili makundi ya majambazi, kidogo kidogo wanaanza kujinasibu
 
Mayalla is very intelligent sema sasa"ukabila-usukuma " umemshinda, yaani kidogo tu aungane na "praise team" ya ibada ya kwanza
 
Mkuu Pascal Mayalla tofauti ni muda na mahali zilipotolewa..lakini zote lengo ni moja..
2+2=4
3+1=4
Haha 😂 Mkuu ukweli huwa ni mchungu.
Kweli umesema kitu cha maana. Magufuri ndiye aliyeagiza kuwa polisi waue majambazi. Hata vile vifo vya watu kwenye viroba na watu waliouliwa MKIRU ni maagizo yake.

Hamna namna unaweza kumtenga JPM kutoka kwenye kauli na vitendo vya watu wake. Huyu RC Mbeya ni kichaa kabisa na JPM mwenyewe alisha kiri hadharani kuwa yeye mwenyewe ni kichaaa na ndiyo maana anachagua vichaa wenzie kama yule Luhaga Mpina waziri wa mifugo. Tuendelee kupiga goti kwa imani ya dini zetu ili Mungu atuepushe na utawala huu wa kifedhuli.

Ila naamini Mungu atatenda 2020, huyu mtu JPM hatufai.
 
YAMETIMIA maneno yako hapo juu
 
Wanabodi, katika bandiko hili, niliilaumu amri hii ya JPM, lakini tukio la leo, la kichaa mmoja kutuulia polisi wetu 3 na mlinzi mmoja, leo sasa ndio nimegundua JPM aliona mbali.

Ningekuwa mimi ndio kiongozi wa operation ile, ningetumia snipers kumshoot strategic areas to destabilize him, ili abaki hai kwanza, and they make him talk before they are done with him ili tujue the motive and the ring. Kitendo cha kumalizana nae, there and then, then police have lost everything.

RIP askari wetu wa polisi, RIP Mlinzi wa kampuni binafsi, na pia RIP Jambazi, Gaidi, besides everything, he was a human being, he deserves some dignity!. Na kwa msio jua, hata Osama, pamoja na ufirauni wake wote aliofanya kwenye September 11, baada ya kuuwawa kikatili, mwili wake ulioshwa Kiislamu na kuswaliwa na Sheikh, kisha alizikwa Kiislamu na kutazamishwa kabila!.

Japo JPM, haupo nasi, lakini uliona mbali, amri yako ndio imeanza kutekelezwa, nakuomba Rais Mama Samia, ili kumuenzi JPM, wapandishe vyeo askari hao mashujaa.

P
 
Hili la polisi kuua panya road, Maelezo ya Polisi kuhusu Panya Road hayaeleweki. Kwanini wanaua na siyo kukamata? Je, ni yale yale ya akina Zombe yanajirudia?
watu wanapiga kelele utadhani haya mauaji ya polisi with impunity hawa polisi ndio wameanza leo!, hawakuanza leo, huu sio mwanzo, na wala huu sio mwisho unless something is done kuzifuta amri batil al-halal kama hii ya kwenye bandiko hili Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?
P.
 
Polisi waliruhusiwa kuua!, sasa wanasubiri kupandishwa vyeo.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…