Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

Hapo amefungulia mbwa kwani askari watawaua watu waliobeba fedha na madini kwa kutumia mwanya wa 'kuruhusiwa kunyang'anya silaha'. Rejea mauaji ya wafanyabiashara wale wa Morogoro pale ukuta wa Posta, unaambiwa jinsi polisi walivyonyang'anyana fuko la fedha, ilikuwa aibu
 
Dah wewe nawe ni shida tupu. Kwa hiyo una maana kuwa IQ ya huyu mgeshimiwa ndo top. Mimi nafikiri una shida kubwa ya uelewa ndo maana hukumwelewa pasco. Kwa maoni yangu raisi anapaswa kuwa makini katika kauli zake asije zua sintofahamu ya uelewa inayoweza kuwafanya askari wetu watumia agizo hilo vibaya. Unahitaji IQ ya wastani tu kuelewa kuwa kwa matamko kama haya usalama wa raia na wananchi unabakia kuwa nadharia tu. Ushauri wangu ni kwamba askari wafanye kazi zao kwa kuzingatia sheria au sheria zibadilike ili kuendana na matamko ya mkuu wa nchi.
 
Sina U hakika na namna ambavyo watafanya kuwanyang'anya kama walikuwa wakadhindwa kuwsnyang'anya mapanga na marungu kwenye vituo vyao. Labda kama kuna maana tofauti
 

Mkuu, ndio maana kuna askari kanzu, CID na wengine mabarabarani ili kusaidia "smooth operation".

Hivyo kama eneo fulani umetokea ujambazi basi polisi watafanya response kulingana na situation ya mahala husika.

Hivyo hatuwezi jua IGP Mangu amejipanga vipi.

Miaka ya 80 wakati wa IGP Solomon Riyani, D'Vaz na Mahundi kulikuwa na strategy inayoeleweka, ndio maana naona kama Mangu hana siku nyingi vile maana mkulu kaweka KPIs kila ofisi.
 


Raisi Magufuli anatumia metaphor hivyo wahusika wameshamuelewa alichomaansiha na ambao hawajamuelwa ni kwamba IQ haitoshi, ni rahisi kihivyo tu!
 
Ni wakati wa kutekeleza sheria ipasavyo kwa wanaovunja sheria! Watanzania tumelea uzembe kwa muda mrefu wakati huohuo kila mtu analalamikia utekelezaji hata wanaowajibika kutekeleza nao wanalalamika.

Rais Alichokisema na kuagiza ni sahihi kabisa. Mwisho wa kuunda kamati za kuchunguza uovu umefika, ni wakati wa vyombo vilivyoundwa Kikatiba na kisheria kutekeleza wajibu wao bila kigugumizi.
 
Kwani waliowafuga hao majambazi ni akina nani? Utawala ulikuwa chini ya chama gani? Nadhani kuna haja ya kuwa wawazi na pale inapogundulika kwamba tulikosea ni vyema tukili tu ili yaishe
 
Raisi Magufuli anatumia metaphor hivyo wahusika wameshamuelewa alichomaansiha na ambao hawajamuelwa ni kwamba IQ haitoshi, ni rahisi kihivyo tu!



Wewe tetea utumbo tu siku yalikukuta ndo utajua metaphor

Hujui polisi wa kibongo wewe
 
Kuna kitu inaitwa wrong time at the wrong place!au misinformation ukakuta mmelimwa shaba hata msiohusika hapo ndo shida itapokuwepo.askari wenyewe sio waelewa wanataka sifa wataua hadi wasiousika kwa ukiraza wao wa std7
 

Paul Alex nadhani wewe ni mmoja wa wale wa Barbosa. JPM anaongozwa na Katiba ya nchi. Matamushi yake (ambayo ni maagizo) ni kusisitiza uwajibikaji ndani ya sheria.

Tuamini Jeshi la Polisi linaongozwa na binadamu na siyo Robot.

Waliokuwa wakitenda uhalifu kana kwamba hakuna mkono wa sheria mwisho wao sasa.
 
Enzi za akina Mussolin naona zinarudi kwa kasi sana hapa Bongo. Dah! Tuombe Mungu yasitukute ya kule Kuwait sijui Iraq, aaah! Kumbe ni Libya.
 
Kauli ikiotolewa ni ahueni kwa walengwa ila wasiojua maana ya kauli ile mtajua nikumfata jambazi umbusu akuoe bunduki lahasha, ndio tofaut ya ccp na ifm.
Ndugu yangu mimi najua na nina minafahamu na nina mambo mengi ya police international na hapa kwetu polisi ukifika
wanaangalia uko vp maswali mengi wakijua wewe mambo yako safi
Ni kweli uongo wa polisi unakubalika. Ukweli wa raia haukubali.
 
Kwakuwa hauna ndugu au jamaa yako wa karibu alieuawa na majambazi utaona kama JPM anakosea,

Jambazi anaekuja na silaha ana nia moja tu ya kukudhuru, sasa mtu kama huyo sio wa kumuacha
Vile vile haufahamu ugumu wanaokutana nao askari pindi akikabiliana na majambazi.
Polisi akiua jambazi anasimama mahakamani, akimuaacha anakufa yeye.
 
Mwambie Pasco aache fitina juu ya magu. Kama hakukuelewa Basi tu
 
Ndugu yangu mimi najua na nina minafahamu na nina mambo mengi ya police international na hapa kwetu polisi ukifika
wanaangalia uko vp maswali mengi wakijua wewe mambo yako safi

Ni kweli uongo wa polisi unakubalika. Ukweli wa raia haukubali.
Sawasawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…