Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?





Kweli akili zakuambiwa changanya nazako!! Hapo ndy umeandika madudu gani?
 
Well said kiongozi
 
Wafafanuzi wa Rais naona mpo wengi. Mbona ameeleweka vizuri tu?
 
Yaelekea ndivyo ilivyo maana hata hotuba yake ya kukabidhiwa ripoti ya uchaguzi na NEC, tumeambiwa na msajili wa vyama vya siasa kwamba Rais alikuwa anaongea 'metaphor' kwa hiyo alieleweka vibaya, na akajitolea kutoa 'tafsiri' ya alichomaanisha Rais. naona ni vema tupewe hizo codes, au tuambiwe kabisa watoa tafsiri wa Rais ni kina nani siyo mara Msajili, mara Lizaboni, jingala, Barbarosa, sijui nani yule anayelia bungeni...
 
Imagine siku mfanyabiashara ambaye ana mali amevamiwa na askari wakamtwanga risasi na kupora, kisha waka-stage mazingira kuwa alikuwa jambazi na wamemwua kwa sababu alikuwa na silaha na alianza kupambana nao? nani atahakikisha na path to the court imeshafungwa kwa kauli ya Rais?
 
IQ yako imetulia uko sawa....wenye uwezo mdogo ndo wanasumbuka....wao direct means ndo wanaelewa....indirect haelewi kitu.
 
mh
aisee sikuyafikiria yote haya......
ila nchi inahitaji wataalam na washauri wazuri ili iweze kwenda.
 
mh
aisee sikuyafikiria yote haya......
ila nchi inahitaji wataalam na washauri wazuri ili iweze kwenda.
Ni kweli. Kuna watu ni opportunists. Nafasi kama hii ikitolewa, wanatengeneza mazingira ya kuitumia kujinufaisha. Mwisho wa siku wanaweza kumdhulumu mtu asiye na hatia MALI zake, SIFA yake njema na UHAI wake na kumgeuza kuwa MAREHEMU JAMBAZI SUGU.
 
Sikuamini nilikuwa kama naota vile. Kauli hii itakuwa ni kinyume kabisa na matakwa ya katiba, naona giza mbele kinene, MUNGU a tuepushe na matokeo ya MM, sijui!!!!!!!!!????
 
Mkuu, clearly our commander in chief ameendelea kutoa matamko ambayo yanaweza kutafsiriwa kuwa ni maagizo ambayo yapo kinyume cha sheria na hata mfumo wa kidemokrasia tunaoufuata kwa sasa kama nchi. I personally believe that he is overstepping his legal and authoritative bounds, completely undeterred.

Ila nikurekebishe kidogo kwenye mifano yako: hakuna causal relationship kati ya ongezeko la ujambazi Marekani na kuendelezwa kwa capital punishment Marekani. Kumbuka pia, kuna majimbo Marekani ambayo yalishapiga Marufuku capital punishment. Hivyo, kuna majimbo ambayo yana sera ya kutokuua waliokutwa na hatia ya kuua sawa na Uingereza, ila bado kwenye miji ya hayo majimbo kuna crimes nyingi kuliko miji mingi tu ya Uingereza; kwasababu kuna factors nyingine zinasababisha. Kwa mujibu wa high profile studies nyingi, crime Marekani inachangiwa zaidi na tofauti kubwa kati ya mwenye nacho na asiye nacho; i.e. kwenye poor populations USA, hasa zile za rangi isiyo nyeupe, kuna crimes nyingi kuliko kwenye rich populations. Pia sheria legevu zinazoruhusu kumiliki silaha ya moto kirahisi mno zimechangia ongezeko la crimes USA.
 
Halafu mi Niko against Sana politicians kujikita kutoa solutions za maswali magumu yanayohitaji wataalamu wabobezi. Hatuwezi Kuwa nchi Ya Kuwa na majibu Ya mtu mmoja kutokana nafasi zao ni lazima tuwe na majibu yenye record Ya analysis za kutosha. Tunafurahia tu tunaposikia watawala wakitamka Kwa jazba lakini maendeleo hayawezi kuja kwa style Hiyo otherwise watu waachane na kuchimba elimu tusikilize wakuu wanasemaje. SI ajabu hiyo MM ikawa si solution Kabisa ila dawa ikawa inahitajika kujenga jamii Kuanzia grassroots . Tunahitaji kuendelea na Hakuna shortcut.wenzetu hata hata kuweka vigae vya chupa juu ya uzio ni offence kwani vitahatarisha maisha Ya jambazi. Hawafanyi hivyo kumfurahisha jambazi bali inaweza ikawa I naongeza civilization kwa jamii na jambazi mwenyewe Kwani Hata jambazi akiwa civilized ataacha bunduki na kufanya kazi zenye tija. Tunahitaji kufanya zaidi Ya kujikita Kwenye solutions zinazotolewa jukwaani kama kweli tunataka maendeleo plus civilization
 
Raisi wetu naamini anaamini Kwenye research kupata majibu Ya maswali magumu .sitaki kwenda mbali ila naamini hivyo.
 
Magufuli ataliharibu jeshi la police kwa maagizo yake, bahati nzuri jeshi la police ni moja ya taasisi ambazo zinaendeshwa kwa kanuni sana hasa kwenye upandaji wa vyeo.

Sasa sijui magufuli anafikiria nini kwa sababu hata yule trafic aliye msimakisha mke wa waziri mkuu wa police alimwambia lazima akidhi vigezo kwanza ndio apande cheo.

Pia mh rais akiendelea hivi kutoa order zisizo tejelezeka baadae atadhafauliwa.

Anahitaji kushauriwa jinsi ya kusema unapo kua kongozi.

Pia aachane na kuwa juu ya sheria kwa sababu police itabidi wamwulize kwanza juu ya kutekeleza jambo kabla ili wasimkwaze
 
Ni lazima tuheshimu sheria na tukiwa na askari wasioheshimu sheria tumekwisha. Naanza kuogopa. Ujambazi haujalishinda jeshi letu mpaka tufikie hatua hiyo. Kila kazi Ina discipline yake .tutajuta kujenga jeshi lisilo Tumia psychology ku solve matatizo yetu
 
Kwa hiyo wee unataka polisi wawanyanganye majambazi silaha kwa kuwaomba na kuwapigia magoti sio?

Dawa ya moto ni moto,usitake kujifanya mpenda haki wakati unasahau haki za watu wengine,mtu yeyote anayetumia silaha vibaya anapaswa kunyanganywa tu hakuna kubembelezana hayo mambo yako ya haki za binadamu peleka UN hapa kazi tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…