Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

Mkuu, kinachoongelewa ni majambazi kutumia silaha na kupora kwenye mabenki na majumbani mwa watu.

Rejea lile tukio la Salasala ambapo raia mwema mwenye fedha zake alipigwa risasi kama nguruwe pori na kisha begi la pesa zake kuchukuliwa.

Tunazungumzia "serious organised crimes" wa kutumia silaha na sio wizi wa kuku.
Mkuu kama ni organized crime anawafanya police kuwa target kwa majambazi. Hawa wanaofanya hizo organized crimes they are well trained, wengi ni ex police or para military officers na wao wamemsikia nao watajiandaa kukabiliana kujilinda na mauti. Mimi wasiwasi wangu uko kwa police wetu. Uelewa wao katika hili, Wengi wasivyowaelewa wanaweza kutumia fursa hii kuuwa innocent people kwa kisingizio cha ujambazi ili wapande vyeo.
 
Tungeombwa na sisi kuongeza nguvu katika jeshi la polisi
 
Mkuu Ahsante Kwa uzi mzuri,
Swali linabaki, hivi kweli IGP Mangu aliwahi sema sheria imekuwa kikwazo Kwa wao kutekeleza majukumu yao?
Na Kama ni hivyo kwanini wasiandae muswada wa kuwaruhusu polisi"kunyanganya silaha Mara moja"?
Matukio yenye maswali mengi ya vitendo "vya kutisha" "visivyothibitishwa" mahakamani(kumbuka hata ya Zombe iliyeyuka) juu ya uadilifu wa jeshi letu dhidi ya raia zinaibua wasiwasi na hofu kuu dhidi ya kauli ya Mh. RAIS,
Hivi tuna haja ya kuendelea na mfumo huu wa jeshi la polisi? Kwanini lisibadilike ili kuongeza ufanisi?
Was "kunyanganya silaha" the only best option????
 
Massenberg, sasa naanza kuelewa kwanini Marais wastaafu hawakauki Ikulu.

Mkulu ataleta shida kubwa sana kwa haya matamko yake.
Inapaswa mtu awe anamkumbusha kuwa yeye ni Rais.
Ajue kuwa kutoa order zenye utata na ambazo hazitekelezeki kunashusha hadhi yake!
 
Mkuu kama ni organized crime anawafanya police kuwa target kwa majambazi. Hawa wanaofanya hizo organized crimes they are well trained, wengi ni ex police or para military officers na wao wamemsikia nao watajiandaa kukabiliana kujilinda na mauti. Mimi wasiwasi wangu uko kwa police wetu. Uelewa wao katika hili, Wengi wasivyowaelewa wanaweza kutumia fursa hii kuuwa innocent people kwa kisingizio cha ujambazi ili wapande vyeo.

Hapana hao criminals wanajulikana, hii Tanzania mkuu huwezi jua hata raisi JPM anayo list.

Kuna watu wapo tayari kutaka kuleta vurugu nchini na TISS na polisi wanafahamu hilo.

Pia huwezi kujua kama hii PR ya leo inamaanisha nini.

Fikiria "outside the box" mkuu.

Kama wewe ni raia mwema una hofu gani kiasi cha kuweka silaha nyumbani, na ni nani amekutishia maisha?
 
Bwana Pasco
Nimejua kwamba wewe sio mtumishi wa idara za ulinzi na usalama na ndio maana kauli hii kidogo imekua ngumu kuielewa..
Maana ya kauli ile kwa walengwa yaani polisi na vyombo vingine nya ukinzi na usalama, tayari wameelewa maana iliopo ndani ya maana halisi ya kauli.
Kwahyo nikuambie tu tafsiri ulioipata sio hiyo iliomaanishwa, that statement is beyond the focus to interpret to an ordinary citizen.
Lakini kwa wapiganaji unasema "Tutatekeleza afandeeee".
Over and out
 
mkuu sana Pasco baada ya kusoma maelezo yako, nimegundua bado haujajua ugumu wanaokutana nao polisi wakati wa kupambana na majambazi wenye silaha. Kwenye mapambano yeyote anaweza kuuawa jambazi au askari. Kauli ya kuwanyang'anya majambazi silaha, lengo lake ni kuwaondoa hofu askari. Lakini majambazi wanaoua watu bila hatia, wakinyang'anywa silaha hata wewe utakua na amani kwa usalama wako.
Askakari wanawajua hao wote. but its one deal wangapi wanatoa taarifa kwa polisi lakini mambo hayafuatiliwi. hao wanakula polisi wetu kijumla .
 
Bwana Pasco
Nimejua kwamba wewe sio mtumishi wa idara za ulinzi na usalama na ndio maana kauli hii kidogo imekua ngumu kuielewa..
Maana ya kauli ile kwa walengwa yaani polisi na vyombo vingine nya ukinzi na usalama, tayari wameelewa maana iliopo ndani ya maana halisi ya kauli.
Kwahyo nikuambie tu tafsiri ulioipata sio hiyo iliomaanishwa, that statement is beyond the focus to interpret to an ordinary citizen.
Lakini kwa wapiganaji unasema "Tutatekeleza afandeeee".
Over and out

Mkuu, kauli imeeleweka vizuri kwa walengwa wa pande zote mbili, ila Pasco na kundi lake wanatumwa kupotosha.

Kilichobakia ni kitu kimoja tu ama unaungana na jitihada za raisi au unazipinga kwa kutumia mbinu mbalimbali.
 
Huyu jamaa bora awe anakaa kimya kila siku anakuja na jambo la kukera hivi hana mshauri.
 
Mkuu, hoja imeeleweka vizuri ila Pasco na kundi lake wanatumwa kupotosha.

Kilichobakia ni kitu kimoja tu ama unaungana na jitihada za raisi au unazipinga kwa kutumia mbinu mbalimbali.
Mkuu mimi sio allie wa siasa ila nimejaribu kumuambia akiwa kama raia wa kawaida hawezi elewa raha na utamu wa kauli jinsi itakavyorahisisha kazi.
 
Bwana Pasco
Nimejua kwamba wewe sio mtumishi wa idara za ulinzi na usalama na ndio maana kauli hii kidogo imekua ngumu kuielewa..
Maana ya kauli ile kwa walengwa yaani polisi na vyombo vingine nya ukinzi na usalama, tayari wameelewa maana iliopo ndani ya maana halisi ya kauli.
Kwahyo nikuambie tu tafsiri ulioipata sio hiyo iliomaanishwa, that statement is beyond the focus to interpret to an ordinary citizen.
Lakini kwa wapiganaji unasema "Tutatekeleza afandeeee".
Over and out
Maneno na vitendo ni vitu viwili tofauti kuitikia sio kutenda.
 

Wanabodi,

Wewe kama mwana JF, unapata an added advantage to be the first to know, ambapo leo katika tukio la maboresho ya jeshi la polisi, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais, Dr. John Pombe Magufuli, ametoa kauli kwa kutumia fasihi, ambapo ameliamuru jeshi la polisi, kukabiliana na majambazi wenye silaha kwa "kuwanyang'anya silaha kwa kutumia mbinu za medani, (kivita) (MM) ambazo hutumiwa na majeshi wakati wa vita, ambapo kazi huwa ni moja tuu, kumteketeza adui!.

Amri hiyo kwa Jeshi la Polisi, inamaanisha, Polisi hawahitaji tena kuwakamata majambazi wanaotumia silaha, bali kukabiliana nao kwa kuwaua papo kwa papo, na polisi wataofanya mauaji hayo ya kuwauwa majambazi hayo papo kwa papo bila kuwapeleka mbele ya vyombo vya sheria, hawatafikishwa tena mahakamani, kama zamani, bali sasa watapandishwa vyeo!.

Agizo hilo limepokelewa kwa shangwe na makofi kwa kila aliyekuwe pale.

Rais huku akisema kwa msisitizo kwa kutumia fasihi ya "kuwanyanganya silaha", kwa vile majambazi wanatumia silaha, zenye risasi kufanya ujambazi, na jeshi la polisi nalo wanazo silaha zenye risasi, haoni kwa nini majambazi hayo yasinyang'anywe silaha zao!. Namna pekee ya kunyanganya silaha jambazi mwenye silaha, ni kumalizana nao, papo kwa papo!.

Sina shaka kabisa na nia ya dhati ya rais Magufuli, kutoa amri, hiyo, kufuatia nchi na wananchi kuchoshwa na vitendo vya ujambazi kuongezeka, hivyo majambazi wakijua kuwa wakikamatwa watauwawa right away, then, amri hii badala ya kupunguza ujambazi wa kutumia silaha, ndio kwanza utaongeza impunity kwa majambazi wanaotumia silaha, na wakati huo huo kuligeuza jeshi letu la polisi kugeuka Gestapo!.

Sio majambazi wote wanaotumia silaha, zile silaha zao zina risasi!, wengine huzitumia kutishia tuu, lakini hawana nia ya kufanya mauaji, na kuna wengine hubeba silaha ambazo hazina risasi, na wengine hutumia toy pisto!, lakini kufuatia amri hii, polisi ndio kwanza wamekuwa licenced to kill!.

Tanzania ni nchi ya kidemokasia inayofuata katiba yenye kuzingatia haki na utawala wa sheria!, amri kuu ya kwanza ya haki, ni "no one is condemned unheard", yaani hakuna mtu atakayehukumiwa bila kusikilizwa!. Amri hii ya rais, imewapa mamlaka polisi, sio tena kuchunguza, kukamata na kuwapeleke majambazi wanaotumia silaha, mbele ya sheria, bali sasa polisi hawana tena haja ya kukamata na kufanya uchunguzi, bali kukitokea tuu tukio la uhalifu wa kutumia silaha, polisi wamepewa mamlaka kuwa ni wachunguzi, prosecutors, mahakimu tena kwa kutoa "capital punishment", na hakuna tena haja ya kumsubiri rais kuzisaini hizo hati za capital punishment, bali, wao wenyewe kutumia MM, kuitekeleza adhabu ya kifo, na baada ya hapo kusubirria kupandishwa vyeo!. Just imagine mashindano ya kupanda vyeo miongoni mwa polisi wetu!.

Kama wanasheria wetu, hawatashitushwa na amri hii ya rais, nitaamini sasa Watanzania wameanza kumwelewa rais wetu, na ukiisha elewa, huna haja ya kuhoji!.

Angalizo: Sitetei vitendo vyovyote vya uhalifu wa aina yoyote, bali natetea utoaji wa haki!, hata jambazi anayetumia silaha, anastahili kutendewa haki!. Natolea mfano wa nchi mbili za Maekani na Uingeeza. Miaka ya nyuma nchi zote hizi zilikubwa na vitendo vingi vya mauaji. Uingeeza ikafuta adhabu ya kifo!, vitendo vya mauaji, vikapungua kwa kiasi kikubwa!. Maekani ikaendelea na adhabu ya kifo, vitendo vya mauaji bado vimeongezeka!.

Amri ya kuwaua majambazi papo kwa papo, haitapunguza ujambazi, bali itawafanya hao majambazi ndio kugeua wauwaji wakuu, kwa hoja za "ama zao, ama zetu" na kwenye tukio lolote la ujambazi wa kutumia silaha, polisi wakitokea, sasa sio tena kutuliza amani bali kufanya a blood bath!, hivyo polisi sasa pia watakuwa ni target ya majambazi!.

Kwetu sisi waandishi, ikitokea polisi wakakutana na gun mike, au boom mike, au hata kamera wakaiona ni kama sihaha!, kama ilivyotokea mwa Daudi Mwangosi!, askai mhusika, atapandishwa cheo!. Kama wale vija wa Zombe, sasa watawadiwa vyeo!.

Huko nyuma niliwahi kushauri, kama katiba ni kikwazo, rais Magufuli, aiweke pembeni katiba na badala yake atawale kwa kutumia 'presidential decrees' tuu!. Hivyo kwa amri hii ya polisi kuua majambazi papo kwa papo, kama mahakama ni kikwazo, pia anaweza kuiweka pembeni, na kuwatumia polisi kutoa hukumu za kifo cha papo kwa papo, tena hili litaokoa fedha nyingi sana, maana majaji wa mahakama zetu, wanahudumiwa kwa gharama kubwa sana!.

Wasiwasi wangu kwa amri kama hizi, sio ili kuokoa maisha ya majambazi wanaotumia silaha, au kuwaacha tuu majambazi wanaotumia silaha kuua, lakini wao kuuliwa tuinawatetea!, no!, wasiwasi wangu ni utekelezaji wa amri za aina hii, zisije kuwa kwa majambazi ni mwanzo tuu, baadae amri kama hizi za 'kinyemela' zikaelekezwa kwa makundi mengine, yanayoonekana ni kero!.

Hata Adolfu alipoanza, alianza hivi hivi kwa kushangiliwa na umati wa watu!, ni baadae sana, ndipo watu wakajuta!, chonde chonde twendeni taratibu jamani tusije kujuta!.

Jumamosi Njema.

Pasco[/QUOTE]

Mtu hayawani kama huyu ambaye anafahamu kuwa eti majambazi wengine hutumia silaha zile bila risasi eti na wengine huwa hawana lengo la kuua. Huyu mzandiki anafahamu vipi mipango hiyo ya majambazi na anafahamu vipi malengo hayo ya majambazi kama yeye sio jambazi. Ashughulikiwe huyu na aseme hiyo mipango yao ya matumizi ya silaha yakoje
 
Nitangulie kusema nimestushwa na kauli ile hadi nikasahau kuianzishia mjadala. Asante Pasco kwa kuniwahi.
Barbarossa utuambie, toka lini baba yako akakupa assignment ya kufanya through metaphor? Labda hukuishi na baba ndio maana hutojibu. Rais ni baba, tena mkali. Akisimama kusema jambo tunatakiwa kuwa very attention kusikiliza maneno yote bila kuacha. Na akisema anamaanisha. Na hii no amri ambayo uliagizwa kuitekeleza huwezi kumkatisha kauli na kumwambia hapo siwezi.
Hili LA kutuambia polisi akikuona na toy LA silaha akumalize halijakaa njema hats kidogo. Ni hatari Sana kwa usalama wetu. Hebu fikiri MNA bifu na polisi itakuwaje akiamua kuumaliza ugomvi huo kwa staili ya kuua jambazi? Ni kweli hawajui polisi wetu na visa vyao huku mtaani. Watatumaliza. Hugo anayesema habari za metaphor hajui Maana ya kauli za rais. Kwa matamko haya tutakwisha kwa risasi nyingi za polisi.
 
Maneno na vitendo ni vitu viwili tofauti kuitikia sio kutenda.
Kauli ikiotolewa ni ahueni kwa walengwa ila wasiojua maana ya kauli ile mtajua nikumfata jambazi umbusu akuoe bunduki lahasha, ndio tofaut ya ccp na ifm.
 
Back
Top Bottom