Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

Kwakuwa hauna ndugu au jamaa yako wa karibu alieuawa na majambazi utaona kama JPM anakosea,
Na kwa kuwa huna ndugu au jamaa wako wa karibu aliyeuawa na polisi kwa kisingizio cha kupambana na majambazi (kumbe ni njia ya kuchukua fedha au mali zake), utaona kama JPM anapatia
 
Mwengeso, hivi kwanini Magufuli anaongea kwa kiswahili na nyie mnamsaidia kutafsiri kwa kiswahili, huoni kuna shida hapo?
Sawa, kiingereza hapo tumekubali ni bilabila, atafsiriwe!
Na Kiswahili je?
 
Kwakuwa hauna ndugu au jamaa yako wa karibu alieuawa na majambazi utaona kama JPM anakosea,

Jambazi anaekuja na silaha ana nia moja tu ya kukudhuru, sasa mtu kama huyo sio wa kumuacha
Vile vile haufahamu ugumu wanaokutana nao askari pindi akikabiliana na majambazi.
Polisi akiua jambazi anasimama mahakamani, akimuaacha anakufa yeye.
Ni kweli anakuja kwa kutaka ulicho nacho na anajua kweli unacho habatishi ila ikifikia swala la polisi hapo wanakula pamoja na haki yako hauipati. Ukweli polisi na hao jamaa ni sawa na paka na samaki kila mmoja anapenda. kinacho tula sisi ni polisi wetu.
 
Inaonekana JPM hakufuatilia kesi ya kina Zombe & co. na hawajui sawa sawa polisi wetu!!! Napata woga sana!!!!
ukikopi uzi mrefu namna hii na kukomenti maneno mawili, unatuumiza sisi tunaotumia visimu vya mchina.
Samahani kwa usumbufu.
 
Unaandika maandishi meengi na marefu wakati ungeweza kuyafupisha tu, Raisi Magufuli anatumia metaphor anachokisema kina mlengwa na mlengwa siku zote huelewa raisi anamaanisha nini, nitakupa mfano Raisi alivyosema kwamba wanaotumia br. ta DART wakamatwe na magari yao yang'olewe matairi sasa hiyo ni metaphor na wahusika walielewa alichomaanisha kwamba wachukuliwe sheria kali lkn watu mkafanya ikawa ishu kuuubwa wkt ni kitu kidogo tu lkn matokeo yake leo hii wanaovunja hii sheria ni wachache na watu wameanza kustaarabika!

Hivyo raisi Magufuli ni kipimo cha IQ TanZania asiyemuelewa ni kwamba IQ yake haitoshi ni rahisi kihivyo tu ndiyo maana unaona watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri kama Mbowe, Msigwa, Sugu &Co. wanapata shida sana kumuelewa raisi anachomaanisha, watu kama ninyi mmezoea mtu awape jibu kwamba 2 +5 =7 lkn akikwambia kinyume na hapo unashindwa kupata jibu na ndiyo maana mnakuja na tafsiri zenu za ajabu ajabu lkn leo hii ukienda kuongea na wahusika wakuu wa Askari wetu watakwambia Raisi alichomaanisha, na kazi itafanyika na matokeo yataonyekana wote tutakuwa mashahidi!
kwa nn atumie mafumbo ambayo anajua wengi hawatomuelewa lengo lakuzungumza na wanachi ni nn sasa?
 
Something pigs kila kitu ni kupinga tu!! Unawatetea majambazi?? Hapa mwanza walikuwa wanaua na kupora maduka ya mpesa unamteteaje mtu kama huyo,,subiri waje wakuinamishe siku moja ndo utajua majambazi sio wenzako
 
Ukiona anaongea,alafu kuanzia waziri wa wizara husika hadi IGP wanatabasamu..we jua kuwa alikuwa anagmfurahisha jukwaa!!

Ila katika hali ya kawaida majambazi wanakera Sana,kama mwizi wa kuku mtaani anakamatwa na kutwangwa hadi kufa..iweje kwa jambazi anaekuja na kunijerui kisha kuchukua Mali yangu???
Police watekeleze huo utani waliotaniwa bila kubambikia watu makesi ya kijinga kisa kutaka vyeo..maana hawachelewi kuja na kukupa gobore kisha wakakutandika risasi za kifua na kukuburuza kwenda kupandishwa cheo!!

Kama walengwa ni majambazi wa kweli basi utani huo na ukaanze kufanya kazi..
Tumechoka kutafuta kwa jasho then yanakuja majitu yanakupora kama uliyafanyia kazi!!

Na hawa Wa huku mitaani wanaopora simu zetu tutajitahidi TUWANYANG'ANYE HARAKA HARAKA kabla hawajakimbia nazo..
 
Ha ha ha ha ha, mkuu nayaona maumivu nafsini kwako, mtaani kwetu kuna Mzee mmoja alishawahi kuibiwa baiskeli miaka ya nyuma, yeye akisikia kelele za mwizi cha kwanza anatafta lungu lake, pili lazima aje na kiberiti na tatu lazima aje na nyasi zilizokauka za kutosha!
 
mh, mbona mi naona sawa tu.

just imajin, mtu anakuvamia akiwa na silaha,anakuweka chini ya amri zake, anachukua anachotaka na ukifanya masihara anakutoa maisha mm kwa upande wangu sioni sababu za kuwachekea watu kama hawa.

kuhusu kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu, i don't think so, watuwamechishwa na hali ya kutokaa kwa amani.
Wewe hujaelewa anachomaanisha pasco watanzania ni wavivu wa kusoma na kutafsili hebu ludia kusoma uzi ukishindwa kuelewa anachomaanisha njoo jamvini useme tukueleweshe
 
mkuu sana Pasco baada ya kusoma maelezo yako, nimegundua bado haujajua ugumu wanaokutana nao polisi wakati wa kupambana na majambazi wenye silaha. Kwenye mapambano yeyote anaweza kuuawa jambazi au askari. Kauli ya kuwanyang'anya majambazi silaha, lengo lake ni kuwaondoa hofu askari. Lakini majambazi wanaoua watu bila hatia, wakinyang'anywa silaha hata wewe utakua na amani kwa usalama wako.
Akina zombe &co waliua majambazi? Sio kila kauli ni ya kushabikia siku akiuawa ndg yako kisa katembea na demu wa askari utashelehekea?
 
Unaandika maandishi meengi na marefu wakati ungeweza kuyafupisha tu, Raisi Magufuli anatumia metaphor anachokisema kina mlengwa na mlengwa siku zote huelewa raisi anamaanisha nini, nitakupa mfano Raisi alivyosema kwamba wanaotumia br. ta DART wakamatwe na magari yao yang'olewe matairi sasa hiyo ni metaphor na wahusika walielewa alichomaanisha kwamba wachukuliwe sheria kali lkn watu mkafanya ikawa ishu kuuubwa wkt ni kitu kidogo tu lkn matokeo yake leo hii wanaovunja hii sheria ni wachache na watu wameanza kustaarabika!

Hivyo raisi Magufuli ni kipimo cha IQ TanZania asiyemuelewa ni kwamba IQ yake haitoshi ni rahisi kihivyo tu ndiyo maana unaona watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri kama Mbowe, Msigwa, Sugu &Co. wanapata shida sana kumuelewa raisi anachomaanisha, watu kama ninyi mmezoea mtu awape jibu kwamba 2 +5 =7 lkn akikwambia kinyume na hapo unashindwa kupata jibu na ndiyo maana mnakuja na tafsiri zenu za ajabu ajabu lkn leo hii ukienda kuongea na wahusika wakuu wa Askari wetu watakwambia Raisi alichomaanisha, na kazi itafanyika na matokeo yataonyekana wote tutakuwa mashahidi!
Tunashukuru kwa ufafanuzi ila mwandiko wako kama wa Jesykah
 
Ha ha ha ha ha, mkuu nayaona maumivu nafsini kwako, mtaani kwetu kuna Mzee mmoja alishawahi kuibiwa baiskeli miaka ya nyuma, yeye akisikia kelele za mwizi cha kwanza anatafta lungu lake, pili lazima aje na kiberiti na tatu lazima aje na nyasi zilizokauka za kutosha!
Mkuu,wezi ni wato wabaya Sana na hawafai kabisa kujumuika na jamii..hebu fikiri huyo mzee alitumia muda gani kupata usafiri mwingine???

Nilipata kuwa katika kijiji flani kuna mzee kidogo yuko na uwezo pale,walivamia kwake wakamtaka awape hela za walijua anazo maana alitoka kukusanya kodi zake huko..mzee alikuwa ameshaweka bank..hawakuelewa walimtandika risasi za kichwa na kufuani akafa pale pale..

Sasa katika hali kama hiyo naanzia wapi kuwatetea watu kama hao???

Watu tumewahi kukoswakoswa kuuliwa na haya majitu..Leo nitoe wapi ujasiri Wa kuyatetea!!

Watu WAOVU kama hawa ni WAKUPOKONYWA SILAHA HARAKA HARAKA!!

Wakati mwingine wanapora na kuuwa watu..hata hawafungwi!!

Dawa ni KUWAPORA SILAHA HARAKA HARAKA!!

Angalizo ni kwamba,hii iwahusu MAJAMBAZI TU!!
 
Back
Top Bottom