Hili la Prof. Assad kumaliza kipindi chake limekaa kisiasa zaidi na siyo kisheria

Kilichofanyika ni kuwa Rais anapenda watu Yes Boss.
Angalia TISS angalia CAG waliopita
 
Weka na ya kiswahili ibara ya 40 waelewe vizuri zaidi.

 

Attachments

  • 20191104_071838.png
    29.1 KB · Views: 1
Hivi huo muda Wa CAG kuongezewa ni kabla ya umri Wa kustaafu au baada? Tuanze hapo kwanza.mtoa mada umeporomosha vifungu bila kuvielewa.
CAG anaongezewa muda akimaliza miaka 5 ya awali!

Umri ambao ni lazima kwa CAG kuachia ofisi ni miaka 65. Muhimu ni kwamba, akimaliza miaka 5 ya awali, CAG "shall be eligible for renewal for one term"

Shall kwenye sheria zetu ni SHURUTI!

Na kwavile CAG akifika miaka 65 ni lazima aondoke madarakani, tuseme alimaliza miaka 5 ya kwanza akiwa na miaka 65. Hapo muda wake hauwezi kuwa renewable kwa sababu Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma inasema akifika miaka 65 LAZIMA aachie ngazi!
 
Mkuu una uhakika mtu mwenye umri wa miaka zaidi ya 65 anaweza kuteuliwa kuwa CAG pia?

Au katiba inaposema " u CAG wa mteuliwa utakoma pale tu atakapofikisha umri wa miaka 65 ikiwa atakuwa ametimiza vigezo vingine vyote ina maana gani?
 
Assad hakuwa chagua nzuri kwa watawala, waliona ni mwiba kwao, kumbukeni issue ya ndugai. hakuwa tayari kulishwa 'matango pori' alisimama ktk weledi wa kazi yake.
Kuteuliwa kwa kicheere ni kutengeneza 'utatu mtakatifu'
 
Angempa vipi wakati katiba unasema mwisho miaka 60 astaafu, wakati huohuo sheria inasema atapewa mkataba wa miaka mitano, kikatiba na kisheria umri wa cag unapaswa kuwa chini ya miaka 50 ndio twende sawa
Ingempendeza Raisi angeweza kumpa mkataba mwingine (CAG alikuwa eligible na hajafikisha 65). Raisi hana uwezo huo kama CAG anamaliza mhula wake wa pili au amefikisha miaka 65 (CAG inabidi aachie ofisi).
[/QUOTE
 
Mbowe anakazi kweli, kwahiyo hapo uneona umechambua haswa
 
Hayo ya umri wa kustaafu, mihula miwili nk. tuachane navyo. Je muda wake wa miaka 5 kwa kipindi cha kwanza umetimia?
 
Kabisa Mkuu, Dalili zilishaonekana, lakini nashangaa sasa ivi watu bado wanaona kama hii kitu ni ajabu, wakati Udhihilisho ulishaonekana.
 
Jameni rais asipangiwe, aachwe achague na kupanga timu ya kumuwezesha kutimiza ndoto ya Watanzania na Waafrika wanaojifunza kwake.
Wateule wote wa Magufuli ni wachapa kazi, na yeyote anayesuasua anawajibishwa na kutumbuliwa.
Mbona huyu CAG mpya alipokuwa TRA mzee alimtoa kwa madai ya kuvurunda,akampeleka Njombe huko,akawa DAS?
 
Angempa vipi wakati katiba unasema mwisho miaka 60 astaafu, wakati huohuo sheria inasema atapewa mkataba wa miaka mitano, kikatiba na kisheria umri wa cag unapaswa kuwa chini ya miaka 50 ndio twende sawa
Msone CAG huyu hapa Mohamed Aboud Mohamed alistaafu u CAG akiwa na miaka 65 kwa katiba hii hii iliyopo.Alizaliwa 1927 akastaafu U CAG mwaka 1987 .Akiwa katumika Kama CAG kwa miaka 30

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Mstaafu wa Hesabu za Serikali wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Bwana Mohd Aboud Mohd aliyefariki Dunia Nchini India amezikwa katika makaburi ya Wangazija yaliyopo Kisutu Mjini Dar es salaam.

Mamia ya waislamu, familia, wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania walihudhuria mazishi hayo wakati wa jioni.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wake Dr. Mohd Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere Dr. Salim Ahmed Salim na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa SMT walikuwa miongoni mwa watu waliohudhuria mazishi hayo.
Marehemu Mohd Aboud Mohd maarufu Mfaransa alizaliwa Zanzibar Tarehe 25/1/1927 na kupata elimu zake za Dini na Dunia na alipomaliza masomo yake ya sekondari aliajiriwa serikalini mnamo tarehe 1/1/1944.

Marehemu Mohd Mfaransa kwa umahiri wake wa utumishi serikalini alipata fursa ya kupandishwa daraja hadi kufikia kuwa msaidizi Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hadi mwanzoni mwa mwaka 1967.

Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume alimpendekeza Mzee Mohd Mfaransa kushika wadhifa wa Msaidizi Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 1/3/1967.

Tarehe 16/10/1967 Marehemu Mohd Mfaransa aliteuliwa rasmi Mtanzania na Mwafika wa kwanza baada ya Uhuru wa kuwa Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wadhifa aliokuwa nao hadi kustaafu kwake tarehe 25/12/1987.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Matehemu mzee Mohd Aoud Mohd {Mfaransa } mahala pema peponi amin.
 
Hicho kifungu cha CAG ulichokiandika mbona hukuweka "reference" tukisome kwa ukamilifu wake?

Soma namba 7 hapo halafu fata "reference" iliyowekwa hapo uje uweke vifungu vyake.

Huu mchezo hautaki haraka.

Katiba inampa Rais madaraka makubwa sana. Hakuna litakalobadilika. Sijui ule mchakato wa mwaka 2015 nani aliuharibu. Sasa hivi tusijilishe upepo tutapasuka bila sababu
 
Ndoto ya Watanzania ni ipi?
Wanaota mchana au usiku?
Jameni rais asipangiwe, aachwe achague na kupanga timu ya kumuwezesha kutimiza ndoto ya Watanzania na Waafrika wanaojifunza kwake.
Wateule wote wa Magufuli ni wachapa kazi, na yeyote anayesuasua anawajibishwa na kutumbuliwa.
 
Katiba inampa Rais madaraka makubwa sana. Hakuna litakalobadilika. Sijui ule mchakato wa mwaka 2015 nani aliuharibu. Sasa hivi tusijilishe upepo tutapasuka bila sababu
Nimewahi kuandika humu sifahamu kama watu walinielewa "Rais wa Tanzania ana mamlaka makubwa ndani ya Tanzania kuliko Rais wa USA ndani ya USA".
 
naona unamavyeti mengi,Je mahela vp?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…