Hili la Prof. Assad kumaliza kipindi chake limekaa kisiasa zaidi na siyo kisheria

Hili la Prof. Assad kumaliza kipindi chake limekaa kisiasa zaidi na siyo kisheria

Taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Prof.Mussa Assad amemaliza kipindi chake cha miaka mitano kwenye nafasi hiyo. Lakini Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (ambayo ndio sheria mama) haelezi hicho kinachoitwa "kipindi cha miaka mitano"
_
Katiba inaeleza kuwa CAG atakoma utumishi wake atakapotimiza umri wa miaka 60. Yani akifikisha umri wa miaka 60 anapumzika bila kujalisha ametumikia nafasi hiyo kwa muda gani. Iwe miezi miwili, miaka nane, au miaka kumi.

Ndio maana maCAG wote waliotangulia wameongoza ofisi hiyo kwa vipindi tofauti. Mzee Mohamed Aboud aliongoza kwa miaka 27 tangu 1969 hadi 1996. Thomas Kiama akaongoza kwa miaka 9 tangu 1996 hadi 2005. Ludovick Utouh akaongoza kwa miaka 8 tangu 2006 hadi 2014. Sasa hii kauli ya kusema Assad amemaliza kipindi chake cha "miaka mitano" imetoka wapi?

Matakwa ya kikatiba ni umri wa miaka 60, unless aondolewe kwa kushindwa kutimiza majukumu yake. Na ikitokea hivyo Katiba imeweka utaratibu wa kumuondoa kwa kuunda tume.

Lakini taarifa ya Ikulu inaeleza Assad amemaliza kipindi chake cha miaka mitano. Je hiki kipindi cha miaka mitano Ikulu wamekitoa wapi? Kwenye sheria ipi? Kama ipo sheria hiyo ipo ni batili maana inapingana na katiba.

Na kwa kawaida unapotokea mgogoro kati ya sheria na katiba, basi Katiba ndiyo inayoshika hatamu (When a state law conflicts with a Constitution, then constitution prevails because constitution rules supreme above all state laws).
_
Prof.Assad amezaliwa tar.06 October mwaka 1961. Kwa sasa ana umri wa miaka 58. Atafikisha umri wa miaka 60 October 06 mwaka 2021. Hivyo kwa mujibu wa KATIBA alipaswa kustaafu nafasi yake ya CAG akifikisha umri huo, na si kwa hiki kinachoitwa "miaka mitano". I stand to be corrected.!
2202390_IMG-20191103-WA0063.jpeg
 
You must be the first one in the list..I can assure you
logic fails you miserably. does he believe in everything the present government says? if no, then you must be a hopeless imbecile. you have written to let us know that there's one nincompoop in the name of Babel!
 
Hii kitu imekaa vibaya. Kwa kifupi ni kwamba JPM kamtumbua Assad kwa sababu anazozijua mwenyewe. CAG hajastaafu kwani bado hajagonga 60 years. Inaleta ukakasi sana kama JPM ana nia ya dhati kabisa ya kupambana na wizi wa fedha za Umma
 
Naona haya ni mazito itakua ameogopa kama anaweza asiteuliwe 2020
 
Kisheria CAG anatumikia miaka 5, na yuko open for reappointed kwa miaka 5 mingine ila akifikisha miaka 60 ndio amestaafu

Kwenye reappointiment, rais halazimishwi kum reappoint, hivyo Rais Magufuli yuko right kumteua mtu mwingine yoyote na CAG Prof. Assad is sent to early retirement. Ataendelea kulipwa mshahara na marupurupu yote ya CAG hadi atakapotimiza umri wa miaka 60, ndipo atastaafu rasmi na kulipwa mafao yake na kiinua mgongo cha 80% ya the current CAG.
P
Je kulikuwa na sababu za msingi kumng'oa Assad?
 
Prof. Assad amezaliwa tarehe 06 October mwaka 1961. Kwa sasa ana umri wa miaka 58. Atafikisha umri wa miaka 60 October 06 mwaka 2021. Hivyo kwa mujibu wa KATIBA alipaswa kustaafu nafasi yake ya CAG akifikisha umri huo, na si kwa hiki kinachoitwa "miaka mitano". I stand to be corrected!

Kazi zote za kuteuliwa YOU SERVE AT THE PLEASURE OF THE APPOINTING AUTHORITY!! Assad lazima alijua kuwa contract yake ikiisha lazima angeondoka; kutokana na kufichua matumizi mabaya ya Serikali [ wizi wa shs 1.5 trillion] na matumizi mabåya ya Ofisi ya Spika[ Ndugai amekomba mabillioni ya fedha kwa matumizi ya safari za India}!! Contract ya Assad imefikia ukomo hivyo Jiwe ametumia mwanya huo kumtema.
 
Umeandika pumba tu me nilijua utaweka hicho kifungu cha sheria kutoka kwenye katiba lakini umeandika taarab tu
 
Back
Top Bottom