Hili la Prof. Assad kumaliza kipindi chake limekaa kisiasa zaidi na siyo kisheria

Hili la Prof. Assad kumaliza kipindi chake limekaa kisiasa zaidi na siyo kisheria

Maoni ya Profesa

1572856645386.png
 
Kaka hata mimi ndio wasiwasi wangu huo ameshindwa kuperform TRA halafu anapewa tena ofisi nyeti
Labda huku atapaweza kwasababu ni kukagua matumizi wakati TRA ilikua apimwe kwa kukusanya mapato ya serikali. Ukishindwa kimoja sio lazima na kingine kikushinde. Tunamutakia kazi njema
 
Tunajiumiza vichwa bure! Magu ni siku nyingi tu alishaonyesha kuwa HAMTAKI huyu Bwana. Angeshamtoa siku nyiiiingi, akaiingiza sumu mpaka Bungeni kwa kumtumia Ndugai, akakwama. Sasa, ametumia huo upenyo kufanya hiyo DHAMIRA YAKE OVU KWENYE FEDHA ZA WATANZANIA.
Jamani tusikasilike sana. Ni kama wewe kulazimishwa uendelee kuishi na mke wako wakati unaona moja wenu hapendi tena hiyo ndoa. Basi nasisi tuwekewe sheria hakuna cha kutoa TALAKA uone kama hiyo ndoa itakua na amani.
 
Naomba nitumie mfano wa Rais.

1. Article 33(1) inasema There SHALL BE a president of United Republic. 'Shall be' ikikaa peke yake maana yake ni lazima Rais wa Jamhuri awepo.

2. Article 40(1) inasema President SHALL BE ELIGIBLE for re-election. Ukiona eligible imekaa mbele ya 'shall be', maana yake inampa haki Rais aliyepo madarakani kuchaguliwa kwa mara pili lakini siyo lazima achaguliwe kwa mara pili.

Sasa tukija kwa CAG, Public Audit Act inasema CAG shall be eligible for renewal, kitendo cha kuweka 'eligible' mbele ya 'shall be', maana yake CAG ana haki ukiteuliwa mara ya pili lakini siyo lazima achaguliwe.

AsanteniView attachment 1253281View attachment 1253282View attachment 1253283

Hujasoma Sheria nzima wewe.
Sheria inasema kama rais hatamuongezea CAG miaka mitano basi lazima masharti yote ya ibara ya 144 yanayohusu namna ya kumuondoa CAG yazingatiwe, Kwa hiyo ni dhahiri uteuzi wa CAG mpya haukuzingatia sheria

Soma kifungu hiki cha sheria ambacho hata profesa Shivji amekizungumzia.

Img-1572853035577.jpg
 
Nimewahi kuandika humu sifahamu kama watu walinielewa "Rais wa Tanzania ana mamlaka makubwa ndani ya Tanzania kuliko Rais wa USA ndani ya USA".

Kwahiyo hata hili ni kufuata katiba. Hajakosea. Hakuna namna uamuzi wake ukabadilishwa.
Namtakia mema yote Kicheree. I hope the lesson he learned when at TRA will be his guiding principle
 
Hujasoma Sheria nzima wewe.
Sheria inasema kama rais hatamuongezea CAG miaka mitano basi lazima masharti yote ya ibara ya 144 yanayohusu namna ya kumuondoa CAG yazingatiwe, Kwa hiyo ni dhahiri uteuzi wa CAG mpya haukuzingatia sheria

Soma kifungu hiki cha sheria ambacho hata profesa Shivji amekizungumzia.

View attachment 1253648
Na sheria inayompa madaraka Rais inasemaje? Nchi zetu maskini zina shida moja....hizi sheria hazijaunganishwa in the sense that they create a balance. Zimeundwa as if CAG is very independent. Kumbe ni mteuliwa na Rais na kama anateuliwa, kwanini asiondolewe? Maana baada ya kumteua, hakwenda bungeni for approval.
 
Kuondolewa anaondolewa lakini kwa utaratibu maalum uliowekwa kisheria.
Haondolewi kama Rais anavyojisikia kuwaondoa mawaziri wake, wakuu wake wake wa mikoa n. k

Utaratibu wa kumuondoa upo katika ibara ya 144 ya katiba na sheria iliyotungwa na bunge kama hiyo subsection 3 inavyoeleza. Kwamba usipomuongezea CAG muda wa miaka mingine mitano, basi sababu za kutomuongezea ziwe ni kwa mujibu wa ibara ya 144

Soma vizuri hii subsection 3.

View attachment 1253663

I think sheria mama ndio inahitaji kuangaliwa. Kwa hili Rais ana nguvu zake tusidharau
 
Ingempendeza Raisi angeweza kumpa mkataba mwingine (CAG alikuwa eligible na hajafikisha 65). Raisi hana uwezo huo kama CAG anamaliza mhula wake wa pili au amefikisha miaka 65 (CAG inabidi aachie ofisi).
Rais hawezi kutushawishi kuwa anachukua rushwa kwa kuuacha kumuongezea muda mtu aliyeibua ufisadi wa Ths 2.4 Bilioni na kutuletea mtu ambaye alitudhihirishia mwenyewe kuwa ni dhaifu katika kusimamia TRA.
 
Nimejiita ifrs sababu nimebobea kwenye ifrs, nina Diploma in Ifrs inayotolewa na ACCA, nina Certificate in Ifrs for SME's inayotolewa na Acca now nasomea Diploma in IPSAS inayotolewa na bodi ya wahasibu ya Ireland CIPFA hawa ndio Watabe wa ipsas duniani.
Kama unamchongo wa kampuni inataka consultation ya ifrs nishtue mwana.
Mpuuzi kama wewe hata dual concept huijui
Acha kuudhalilisha uhasibu/ukaguzi
Hujui chochote kuhusu field,badilisha hilo jina kanjanja wewe
 
Ungeanza na tofauti kati ya "AJIRA YA KUDUMU" na "AJIRA YA MKATABA WA MUDA MAALUMU"

Ukishafahamu tofauti utagundua kuwa ajira ya mkataba wa muda maalumu inafuata muda ulioainishwa kwenye mkataba wa ajira na siyo umri wa huyo mwajiriwa
Ushawahi kuisoma katiba wewe?!!
Sheria ya utumishi wa umma?!!
Acha ujinga basi
 
Kisheria CAG anatumikia miaka 5, na yuko open for reappointed kwa miaka 5 mingine ila akifikisha miaka 60 ndio amestaafu

Kwenye reappointiment, rais halazimishwi kum reappoint, hivyo Rais Magufuli yuko right kumteua mtu mwingine yoyote na CAG Prof. Assad is sent to early retirement. Ataendelea kulipwa mshahara na marupurupu yote ya CAG hadi atakapotimiza umri wa miaka 60, ndipo atastaafu rasmi na kulipwa mafao yake na kiinua mgongo cha 80% ya the current CAG.
P

Interesting perspective. Amestaafishwa kwa manufaa ya umma! Mjadala huu umejikita kwenye katiba na sheria. Je, katiba na sheria zinasemaje kuhusu hili!
 
Hajatumbuliwa ila amenyimwa nafasi ya kurenew miaka mingine mitano.

Kumbuka wateule wa mtangulizi wanatakiwa kuondolewa.

Na sasa tunajaza nafasi kwa kutumia vijana wa tanroad au kanda ya ziwa.

Tanroads! There must be something very special about Tanroads!
 
Sasa mibunge ya Sisiem na watanzania wagumu kuelewa wanajua nani alikuwa nyuma ya spika Ndugai kwenye sakata na Assard!
 
Hii kitu imekaa vibaya. Kwa kifupi ni kwamba JPM kamtumbua Assad kwa sababu anazozijua mwenyewe. CAG hajastaafu kwani bado hajagonga 60 years. Inaleta ukakasi sana kama JPM ana nia ya dhati kabisa ya kupambana na wizi wa fedha za Umma

Sawa. Lakini katiba imeweka utaratibu wa CAG kusumbuliwa. Hapo ndipo utata ulipo. Kwa mjadala huu inaelekea kuna muungano kati ya katiba na sheria na kwambà mamlaka amechagua kutumia sheria!
 
Nimewahi kuandika humu sifahamu kama watu walinielewa "Rais wa Tanzania ana mamlaka makubwa ndani ya Tanzania kuliko Rais wa USA ndani ya USA".

Awamu ya 5 ya uongozi wa nchi yetu ni mpango wa Mungu wenye lengo mahsusi kwetu. Misahafu inatufundisha kushukuru kwa kila jambo. Tushukuru kwa kupata nafasi ya kutafakari juu ya katiba ya nchi yetu. Jambo jema sana.
 
Back
Top Bottom